Nimeangalia filamu ya Royal Tour. I was not impressed. Itawakera sana baadhi yenu

Nimeangalia filamu ya Royal Tour. I was not impressed. Itawakera sana baadhi yenu

JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Posts
34,188
Reaction score
62,952
Nimebahatika kuangalia filamu ya Royal Tour.

Mimi binafsi haijanivutia, na hata watoto wangu wamesema hawajaona jambo jipya.

Filamu imeonyesha mlima Kilimanjaro, Zanzibar, Ngorongoro, Serengeti, na hifadhi ya pembe za ndovu / nyara za taifa.

Sasa maeneo hayo yameshaonyeshwa katika filamu nyingi zinazotangaza utalii wa Tanzania. Nilitegemea filamu pamoja na kuonyesha vivutio vinavyojulikana, ingetambulisha maeneo mapya ya vivutio vyetu vya utalii.

Pia usimuliaji wa Rais Samia haukuwa wa viwango vya kuridhisha. Inawezekana filamu imeharakishwa kutolewa. Kuna baadhi yenu mtakereka sana na filamu hiyo. Naomba nisisema jambo hilo kwa sasa hivi.

NB:
Nadhani tunaweza kuandaa filamu nzuri zaidi ya kutangaza utalii wetu. Wadau wa utalii wakae pamoja na kujifunza kutokana na mapungufu ya Royal Tour Tanzania.


cc Nguruvi3, Pascal Mayalla, Chige, Kichuguu, Kilatha, Phillipo Bukililo, Statesman
 
Wewe umezowea filamu za van Damme,utapendaje filamu za wanyama!?..hawajatengeneza kukulenga wewe
Mwenzio kapewa tapishi hili na mabwanyenye ya nchi jirani, ambayo yalitaka dunia iendelee kuamini kuwa mlima Kilimanjaro upo Kenya na ziwa Nyasa ni la Malawi.

Hii film inakwenda kuwaumbua na kuwalaza njaa mabwanyenye wote. Maana dunia itaelewa ukweli kuhusu mmiliki halisi wa mlima Kilimanjaro, ziwa Nyasa nk. Hongera raisi wetu Samia.
 
Mwenzio kapewa tapishi hili na mabwanyenye ya nchi jirani, ambayo yalitaka dunia iendelee kuamini kuwa mlima Kilimanjaro upo Kenya na ziwa Nyasa ni la Malawi. Hii film inakwenda kuwaumbua na kuwalaza njaa mabwanyenye wote. Maana dunia itaelewa ukweli kuhusu mmiliki halisi wa mlima Kilimanjaro, ziwa Nyasa nk. Hongera raisi wetu Samia.

..kwa taarifa yako ziwa Nyasa halikutajwa kabisa.
 
Nimetoka kuangalia filamu ya COUNTDOWN.....😱😱🥶🥶😰😰😰

Naogopa kwenda chumbani

Naogopa kubaki hapa sebleni mwenyewe

Naogopa kwenda maliwato na nimekunywa mvinyo mtamu kachupa kameisha....

Na kesho saa 12 alfajiri natakiwa niwe kwenye usafiri nna safari....

Eeh Mola nani alinituma kuiangalia hiyo movie....

Hata usingizi wenyewe umekata.....

Sorry sijasoma hata uzi unasemaje zaidi ya kichwa cha uzi...

Granny is scared 😧!!
 
Hii filamu ni sisi tuliwaomba watuombe watutengenezee au wao walituomba tuwaombe watutengenezee?
Mkuu Mzee Mwanakijiji , hii filamu ni yao, walituomba watutengenezee, tukakubali, wametumia gharama zao, na sasa baada ya uzinduzi, wataendelea na biashara yao kurudisha gharama zao, huku sisi tukifaidika kutangaziwa utalii wetu bure bure.

Tena mbele ya safari, in future, mnaweza kuja kuwa surprised kukuta hata the main character, alilipwa tuu kama ma starring wengine wote wa movies nyingine zote!, the only difference, zile nyingine ni fiction movies, this is non fiction.

P
 
Back
Top Bottom