Nimeangalia filamu ya Royal Tour. I was not impressed. Itawakera sana baadhi yenu

Nimeangalia filamu ya Royal Tour. I was not impressed. Itawakera sana baadhi yenu

Huyo bi mkubwa namshangaa sana, vitu vimepanda Bei na Wala hana hata mpango navyo, mambo aliyotakiwa kufanya waziri wa utalii anafanya yeye, nchi za nje Kuna mabalozi Kila nchi ambapo wanaweza kufanya kazi izo anazokwenda yy lkn bado anaend mwenyew nazn tunachekwa Sana uko nje, wazungu washenzi Sana wanampa mama kichwa huku wanampoteza mwishowe wanatamuacha peke yake pakiwa pameshaharibika, ndo watanzania tulivyo.
 
Mimi bado sijaangalia.
P

Afadhali usiiangalie utapoteza muda wako bure, bora muda huo uchukue rozari tu usali, maana tulitarajia sehemu kama kitulo ziwemo, utalii wa chakula hasa vyakula vya pwani pwani na bara, ruaha, wangetupia na madini mengi tuliyonayo, Nadhani dhana ya utalii hawaielewi vizuri mtalii haji kupumzika tu wengine anakuja na kuangalia fursa za hapa na pale
 
Afadhali usiiangalie utapoteza muda wako bure, bora muda huo uchukue rozari tu usali, maana tulitarajia sehemu kama kitulo ziwemo, utalii wa chakula hasa vyakula vya pwani pwani na bara, ruaha, wangetupia na madini mengi tuliyonayo, Nadhani dhana ya utalii hawaielewi vizuri mtalii haji kupumzika tu wengine anakuja na kuangalia fursa za hapa na pale

..wamezungumzia Tanzanite na wamefika mpaka mgodini.

..bahati mbaya mbuga kama katavi, kitulo, burigi-chato, gombe,...hazikuonyeshwa.
 
Labda lengo ni kuvutia sehemu ambazo accessible to many and can accommodate large crowds at once.

Kwenda kutangaza maajabu ya bonde gani huko sijui Mbeya wakati wakipata watalii 3000 kwa week kuwasafirisha shida, hakuna tour operators wa kutosha, wala mahala sahihi pa kuwalaza wote at once.

So nadhani lengo ni kuwaonyesha vivutio muhimu vya kitaifa inaweza kuwa mundane kwetu, lakini kwa watu wanaongalia kwa mara ya kwanza it’s an awe.

Otherwise sitegemei bi tozo aonyeshe story ya wanyamapori hizo documentaries ni for nature programme lovers na hawa ni automatic watalii bila ya kuangalia sinema, kama ilivyo kwa wale wazungu wenye ambitions za kutembelea nchi nyingi duniani kabla ya kufariki.

Hayo makundi mawili juu ni wachache, wanaobaki wengi ni wale ambao they need convincing on what to expect kuona wakija tanzania nadhani ndio lengo la hiyo documentary.

As for nature documentary lovers Simba hana jipya, anaishi kwenye pack, Simba jike akijichuza kubeba mimba ya mwanaume nje ya pack anafukuzwa, akiwa peke yake jamaa wengine wakimsarandia kama ana watoto wanaviuwa, mara nyingi Simba jike akifukuzwa akikutana na mkiwa mwenzake wanaungana, au kama alikuwa na rafiki wa kike au dada kwenye kundi atampigania harudi kwenye kundi kwa kumtafutia bwana ndani ya pack, akirudishwa atawinda huyo kuwafurahisha Simba wenzake in return anakuwa hana hofu ya usalama wa watoto wake akiwa ndani ya pack etc na drama za akina Simba.

Chui, tembo, fisi, nyati na wengine wote wana story zao, tofauti ya nature documentaries kuna dramatisations of events (enhe itakuwaje sasa hapo simba kafukuzwa). Hii ya bi tozo ni promotion documentary so it should be boring; compared to other documentaries aimed to educate on everyday life of wild animals.
 
Mleta mada na wakenya wako waliokutuma kuja kuandika ujinga huu mmebanwa pabaya, tena katikati ya makalio. Mlikuwa mshazoea kwenda kuihadaa dunia kuwa mlima Kilimanjaro upo Kenya, na kwamba ziwa Nyasa linamilikiwa na Malawi. Dunia ya sasa sio ya kudanganyana tena. Andikeni hata thread 10000 na IDs tofauti tofauti, kikubwa dunia imeshafahamu vivutio vyetu halisi ni vipi na mwenye kutaka kuthibitisha anakaribishwa. Wenye akili tulijua tu kwamba film hii itawaumiza wengi, hasa wale chawa wasiokuwa na moyo wa utaifa, na mabwanyenye wao.
Angalia wewe usivyoelewa mambo ya dunia yanavyokwenda.

Juzi hukusikia maafikiano yaliyofikiwa katika kuwafungulia 'tour guides' wa Kenya kuleta watalii kwenye mbuga za Tanzania?

Sasa mlima Kilimanjaro wa nini kuwa Kenya, kama wanaweza kufaidika nao wakenya maradufu. Watalii wanatua JKIA, wanalala kwenye hotel za Kenya, asubuhi wanasafirishwa kwenye magari ya Kenya kwenda kuangalia utalii uliopo Tanzania. Jioni au kesho yake wanarudi Nairobi.

Hapo unadhani ni nani anafaidika zaidi kwa utalii huo?
 
Hakuna kitu kinanikera kama alichofanya.Hivi magazeti wangekuwa wanaandika "cc" nani angenunua?Upuuzi!

..wakati mwingine " cc " ni kwa faida ya wanaJF kwa ujumla.

..kwa mfano, nikianzisha mada inayohusu sheria lazima nimuite Petro E. Mselewa na paschal Mayalla kwasababu ni wanasheria.

..kama mada inahusu masuala ya elimu lazima nimuite Kichuguu kwasababu huyu kaka yetu ni mwalimu / mhadhiri.

..mada inayohusu siasa na mahusiano ya Afrika Mashariki lazima nimuite Geza Ulole na jamaa toka Kenya MK254.

..kama ni mambo ya ubishi-ubishi lazima nimuite Kilatha kwasababu yeye ni mimi ni nadra sana kuafikiana ktk mada yoyote, but I consider him my friend.

..kama mada inahusu masuala ya kijeshi nitamuita Echolima kwasababu yeye ni veteran wa vita vya Kagera na operation Mahe / Shelisheli.

..Kuna mwanachama anaitwa Kibunango kama ni jambo linalohusu Znz na ninahitaji ufafanuzi huyo ndio mtaalamu wangu.

..mada inayomhusu Mwalimu Nyerere utakuwa unajinyima maarifa kama hutamuita Shwari.

..Wengine ninaowaita ni washikaji wa hapa JF kama Nguruvi3, MALCOM LUMUMBA ambao na wao wamewahi kuniita, au ninaamini wanaweza kuchangamsha mada niliyoiweka.

..Again, ninapom-cc mwanaJF ktk mada yoyote nia yangu ni KUCHANGAMSHA mada ili mimi mwenyewe, na wasomaji wote, tufaidike.

NB:

..kama kuna mtu sikumtaja hapo ni kwasababu ya nafasi na muda lakini mko wengi sana ambao na-appreciate michango yenu.
 
..Nimebahatika kuangalia filamu ya Royal Tour.

..Mimi binafsi haijanivutia, na hata watoto wangu wamesema hawajaona jambo jipya...

Nimependa Neno haijakupendeza wewe not the case kwa wengine, nakumbuka ni shaenda Las Vegas kwenye jambo fulani, 90% ya watu pale hawajui East African countries, leave alone Tanzania.

Hivyo vivutio featured are the best selling ones, na kuhakikishia kwako haina maana but kwa watu wengine sahihi vina maana Sana.

Mfano kuna mtu kazeeka pale Karatu hajawahi ingia ngorongoro, anaona hakuna maana, lakini kuna mtu Australia ndani Queensland Amekuja mpaka Ngorongoro kwa millions of money.

Sijaiona hiyo filamu, lakini ukosoaji wako sio sahihi, ungekosoa namna ya content labda ningekusikiliza lakini kwa uchaguzi wa attractions, no way, you are very wrong.
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji , hii filamu ni yao, walituomba watutengenezee, tukakubali, wametumia gharama zao, na sasa baada ya uzinduzi, wataendelea na biashara yao kurudisha gharama zao.
Tena mbele ya safari, in future, mnaweza kuja kuwa surprised kukuta hata the main character, alilipwa tuu kama ma starring wengine wote wa movies nyingine zote!, the only difference, zile nyingine ni fiction movies, this is non fiction.

P
Kama ni promo kwanini hii movie inauzwa, ilibidi iwe bure ili wengi tuiangalie na wangelipa platform kama youtube, TV stations, Jamiiforums etc ili iangaliwe sana, hii ya kulipa naona ni kinyume wanachokusudia ( kutangaza utalii)
 
Angalia AfRican Addios na HATARI.
Ndo utajua hujui.
Zipo Netflix na Youtube
Hasa iyo ya kwanza
 
..Nimebahatika kuangalia filamu ya Royal Tour.

..Mimi binafsi haijanivutia, na hata watoto wangu wamesema hawajaona jambo jipya...
Ikiwezekana wafanye hivyo,wachangishe pesa watafute watu maarufu Duniani washirikishwe tena wale wenye bashasha..

Ukiangalia wale waandaaji wa documentary za vipindi vya wanyama huwa wanasimulia vizuri na Wana site matukio muhimu yenye mvuto.

Kwa kuwa sio mpenzi wa filamu sitegemei kuiangalia labda wairushe NatGeo.
 
Hakuna kitu kinanikera kama alichofanya.Hivi magazeti wangekuwa wanaandika "cc" nani angenunua?Upuuzi!
Nafikiri umechukia bure tu; mwanzisha mada kumtag mtu mwingine ambaye alishaandika jambo linalofanana na mada yake ni jambo la kawaida tu kumkumbusha mtu huyo kuwa kuna mahala uliandika vile sasa mimi nimeandika hivi. Kama hukubaliani nami basi jitokeze hapa ujieleze kwa kina zaidi pamoja na watu wengine waone hoja zako.
 
Nani hasa mlengwa wa Royal Tour? Ni mgeni au mtanzania?
 
Back
Top Bottom