Nimeangalia filamu ya Royal Tour. I was not impressed. Itawakera sana baadhi yenu

Nimeangalia filamu ya Royal Tour. I was not impressed. Itawakera sana baadhi yenu

..wamezungumzia Tanzanite na wamefika mpaka mgodini.

..bahati mbaya mbuga kama katavi, kitulo, burigi-chato, gombe,...hazikuonyeshwa.

Kuna dhahabu, ruby, tanzanite, ganets kibao zote wangegusia lakini pia yale manyani na sokwe ya gombe yangewekwa humo ili yaingize pesa maana Rwanda wana hayo tu lakini wanapiga pesa ndefu tu
 
Kwa ujumla haivutii.
Tone ya film imejaa ukakasi,
 
..wamezungumzia Tanzanite na wamefika mpaka mgodini.

..bahati mbaya mbuga kama katavi, kitulo, burigi-chato, gombe,...hazikuonyeshwa.
Tuna Nyerere na Ruaha
 
Paskali! Siku zimekuwa nyingi huko ughaibuni mshauri arudi. Andika "KWA MASLAHI MAPANA KWA TAIFA RUDI MAMA"
Mkuu nguvu , wewe utakuwa hunitakii mema!. Kwa kawaida muda wa safari huwa determined na shughuli iliyompeleka, uzinduzi wa filamu yake ya The Royal Tour, New York, Los Angeles California na Washington DC, mikutano ya IMF na World Bank, vocation kidogo, health check, costumes design from designed collection kama Gucci, Louis Vuitton, Yves Saint Laurent, bila kumsahau Cartier etc etc, two weeks hazitoshi!.
P
 
Nafasi hiyo, Rais na hata serikali haijaweka katazo la kutengeneza filam zingine ambazo zitangaza Tanzania na vivutio vyake.

Hakuna fanani ambae awezi kukosolewa, hiyo ni kawaida sana, hivyo basi nawashauri mliona mapungufu andaeni filam zingine kwa jina tofauti, naona niwapeni wazo hili, mkifanya hivyo faida zitaptikana kwenu binafsi kwa kuungiza kipato na kwa Taifa kwa ujumla katika kuitangaza Nchi pia.
naunga mkono hoja
P
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Mkuu nguvu , wewe utakuwa hunitakii mema!. Kwa kawaida muda wa safari huwa determined na shughuli iliyompeleka, uzinduzi wa filamu yake ya The Royal Tour, New York, Los Angeles California na Washington DC, mikutano ya IMF na World Bank, vocation kidogo, health check, costumes design from designed collection kama Gucci, Louis Vuitton, Yves Saint Laurent, bila kumsahau Cartier etc etc, two weeks hazitoshi!.
P
Daah! Basi sawa
 
We jamaa na familia yako inaonekana hata mtaani kwenu hamuishi na watu vizuri sababu mnaujuaji mwingi wa kipimbi sana, na inaonekana mnajiona watu wa class ya juu sana. Tatizo lilipo ni pale ambapo mnaangalia hiyo filamu wakati mna majibu yenu mfukoni tayari... wewe ulitaman mkeo aonekane kwenye filamu wakat anakaanga mihogo si ndio? kenge kweli ww
 
Nimetoka kuangalia filamu ya COUNTDOWN.....😱😱🥶🥶😰😰😰

Naogopa kwenda chumbani

Naogopa kubaki hapa sebleni mwenyewe

Naogopa kwenda maliwato na nimekunywa mvinyo mtamu kachupa kameisha....

Na kesho saa 12 alfajiri natakiwa niwe kwenye usafiri nna safari....

Eeh Mola nani alinituma kuiangalia hiyo movie....

Hata usingizi wenyewe umekata.....

Sorry sijasoma hata uzi unasemaje zaidi ya kichwa cha uzi...

Granny is scared 😧!!
Naomba anauni yako ya makazi.
 
Wewe umezowea filamu za van Damme,utapendaje filamu za wanyama!?..hawajatengeneza kukulenga wewe
Jibu mujarabu kabisaa!!!

Wameishiwa, wanahangaika hadi wanatia huruma.........mara wameshika kakipande hiki mara kile; hawaeleweki tu kwa sasa wanapinga nn wala wanaweza nn. Mama, in a very relaxed way, anawanyima usingizi kweli kweli. Mijamaa inatokwa na mimacho na mapovu huku wakati yeye akijifanyia mambo yake kwa utuuuvu mkubwa huku akitabasamu tu.

Wivu! Wivu! Wivu! Wanatamani hili lingefanywa na 'ntu' wao!
 
Mwanamke anavua samaki! Sasa hiyo ni siasa kwani hata ulaya wanaovua samaki kwa ndoano hakuna mwanamke.
Kumbe hata wewe Mkuu elvischirwa unakabiliwa na tatizo la kasumba!, everything a man can do, a woman can do!. Acha hizo stereo type kuwa kuna kazi za wanaume na Wanawake!.
Umenikumbusha shujaa huyu

Hivyo to unaweza kukuta Samia ndiye rais wa kwanza mwanamke duniani kuvua samaki, tukajikuta tumeingia kwenye the Guinness book of world records!.
P
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji , hii filamu ni yao, walituomba watutengenezee, tukakubali, wametumia gharama zao, na sasa baada ya uzinduzi, wataendelea na biashara yao kurudisha gharama zao.
Tena mbele ya safari, in future, mnaweza kuja kuwa surprised kukuta hata the main character, alilipwa tuu kama ma starring wengine wote wa movies nyingine zote!, the only difference, zile nyingine ni fiction movies, this is non fiction.

P
Asante pascal jibu ni zuri hata kwa wale wanaopenda kuhoji hoji kila jambo huku wakijiona kana kwamba wao ndio wana akili nyingi kwelikweli.
 
We jamaa na familia yako inaonekana hata mtaani kwenu hamuishi na watu vizuri sababu mnaujuaji mwingi wa kipimbi sana, na inaonekana mnajiona watu wa class ya juu sana. Tatizo lilipo ni pale ambapo mnaangalia hiyo filamu wakati mna majibu yenu mfukoni tayari... wewe ulitaman mkeo aonekane kwenye filamu wakat anakaanga mihogo si ndio? kenge kweli ww
Wewe utakua msanii wa bongo muvi, huko kwenu wanawake wanavua samaki! Yeye ameiona na ametoa maoni kwa mfano, wewe unabwabwaja bila mfano, usilete siasa kwenye biashara.
 
Hivi kwanini RUAHA NATIONAL PARK hawaitangazi? Na kiuhalisia ndio hifadhi ya taifa yenye eneo kubwa zaidi, na vivutio vya kutosha?
 
..Nimebahatika kuangalia filamu ya Royal Tour.

..Mimi binafsi haijanivutia, na hata watoto wangu wamesema hawajaona jambo jipya.

..Filamu imeonyesha mlima Kilimanjaro, Zanzibar, Ngorongoro, Serengeti, na hifadhi ya pembe za ndovu / nyara za taifa.

..Sasa maeneo hayo yameshaonyeshwa katika filamu nyingi zinazotangaza utalii wa Tanzania.

..Nilitegemea filamu pamoja na kuonyesha vivutio vinavyojulikana, ingetambulisha maeneo mapya ya vivutio vyetu vya utalii.

..Pia usimuliaji wa Rais Samia haukuwa wa viwango vya kuridhisha. Inawezekana filamu imeharakishwa kutolewa.

..Kuna baadhi yenu mtakereka sana na filamu hiyo. Naomba nisisema jambo hilo kwa sasa hivi.

NB:

..Nadhani tunaweza kuandaa filamu nzuri zaidi ya kutangaza utalii wetu. Wadau wa utalii wakae pamoja na kujifunza kutokana na mapungufu ya Royal Tour Tanzania.


cc Nguruvi3, Pascal Mayalla, Chige, Kichuguu, Kilatha, Phillipo Bukililo, Statesman
Filamu siyo lazima ioneshe jambo jipya kwa kila mtu! Siku zote wapo watakaoona kuwa ni kitu kipya kwao na wapo watakaoona hakuna jipya kwao! Kama kwako haina kitu kipya kuna mamilion wengi kwao itaonesha kitu kipya!!
 
Sasa mleta mada hao uliowaquote ndio unataka wachangie mada yako maana wana uwezo wa kuchangia ama la??

Sasa kama ndio hivyo si muwe mnatumiana PM.
Hii hua inanikera sana. Unakuta mtu anaandaa uzi then chini anaquote raia kadhaa. Tafsiri yake ni kwamba nyie wengine mkicomment ni shobo zenu tu lkn uzi haukulengwa kwa ajili yenu..
 
Back
Top Bottom