Nyankurungu2020
JF-Expert Member
- Oct 2, 2020
- 4,170
- 6,757
Hii kitu niliwahi kugusia ila watu ni wagumu kuelewa..Nimebahatika kuangalia filamu ya Royal Tour.
..Mimi binafsi haijanivutia, na hata watoto wangu wamesema hawajaona jambo jipya.
..Filamu imeonyesha mlima Kilimanjaro, Zanzibar, Ngorongoro, Serengeti, na hifadhi ya pembe za ndovu / nyara za taifa.
..Sasa maeneo hayo yameshaonyeshwa katika filamu nyingi zinazotangaza utalii wa Tanzania.
..Nilitegemea filamu pamoja na kuonyesha vivutio vinavyojulikana, ingetambulisha maeneo mapya ya vivutio vyetu vya utalii.
..Pia usimuliaji wa Rais Samia haukuwa wa viwango vya kuridhisha. Inawezekana filamu imeharakishwa kutolewa.
..Kuna baadhi yenu mtakereka sana na filamu hiyo. Naomba nisisema jambo hilo kwa sasa hivi.
NB:
..Nadhani tunaweza kuandaa filamu nzuri zaidi ya kutangaza utalii wetu. Wadau wa utalii wakae pamoja na kujifunza kutokana na mapungufu ya Royal Tour Tanzania.
cc Nguruvi3, Pascal Mayalla, Chige, Kichuguu, Kilatha, Phillipo Bukililo, Statesman
👇Wazo lenye mantiki: Filamu ya Royal tour ni janja ya mabeberu kujipatia pesa kupitia sekta ya utalii, taifa letu ni kivutio kikubwa cha utalii...