Nimeangalia filamu ya Royal Tour. I was not impressed. Itawakera sana baadhi yenu

Nimeangalia filamu ya Royal Tour. I was not impressed. Itawakera sana baadhi yenu

Wewe umezowea filamu za van Damme,utapendaje filamu za wanyama!?..hawajatengeneza kukulenga wewe
JokaKuu amezingua sana. Royal tour ingekuwa Kwa ajili ya wabongo si ingezinduliwa hapahapa Tanzania? Ililenga kutangaza vivutio vya nchi yetu nje ya mipaka ya Tanzania, na huko nje hivo vitu kwenye hiyo filamu ni vigeni kwao. MATAGA waache kudandia vitu visivyowahusu
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Kumbe hata wewe Mkuu elvischirwa unakabiliwa na tatizo la kasumba!, everything a man can do, a woman can do!. Acha hizo stereo type kuwa kuna kazi za wanaume na Wanawake!.
Umenikumbusha shujaa huyu

Hivyo to unaweza kukuta Samia ndiye rais wa kwanza mwanamke duniani kuvua samaki, tukajikuta tumeingia kwenye the Guinness book of world records!.
P
Tangu nizaliwe ninaishi pwani ya bahari na ziwa sijawahi kuona mwanamke anavua samaki kwenye mtumbwi au ndoano labda akina mama wanaovua vidagaa kando ya ziwa au bahari kwa kutumia kanga, tuwe wakweli tusilete siasa za vyama kwani filamu hiyo si kwa wanaccm au wasio wanaccm japo wamaccm tayari wanadalili ya kuidandia.
 
Tunakusifu kwa kujitolea muda wako kuangalia 7b/- ikichomwa moto. Wengine sidhani kama tutajaribu. Tunajuwa mama na genge lake wako kule kula bata. Kumuona rihanna, kupepesa macho, kutumbuwa tozo na kodi zetu.
Tunajipanga uchaguzi. Watakiona cha mtema kuni
Hiyo 7b ilitumika kuandaa hiyo filamu, baada ya hapo huu uzinduzi wa rais kukaa ughaibuni na akina magulu ya chemba, tabasamu & co nk nk, itagharimu kiasi gani maana Hadi Sasa wanakula Bata la uzinduzi huko US.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu nguvu , wewe utakuwa hunitakii mema!. Kwa kawaida muda wa safari huwa determined na shughuli iliyompeleka, uzinduzi wa filamu yake ya The Royal Tour, New York, Los Angeles California na Washington DC, mikutano ya IMF na World Bank, vocation kidogo, health check, costumes design from designed collection kama Gucci, Louis Vuitton, Yves Saint Laurent, bila kumsahau Cartier etc etc, two weeks hazitoshi!.
P

Umenikumbusha kitabu cha An enemy of the people ambapo ilikua inafikia wananchi wanaambiwa kiongozi anaenda kuwapigania ulaya kumbe kaenda kuhudhuria sherehe za wapenzi wake
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji , hii filamu ni yao, walituomba watutengenezee, tukakubali, wametumia gharama zao, na sasa baada ya uzinduzi, wataendelea na biashara yao kurudisha gharama zao, huku sisi tukifaidika kutangaziwa utalii wetu bure bure.

Tena mbele ya safari, in future, mnaweza kuja kuwa surprised kukuta hata the main character, alilipwa tuu kama ma starring wengine wote wa movies nyingine zote!, the only difference, zile nyingine ni fiction movies, this is non fiction.

P
Sasa kama ni hivyo mkuu mbona kwenda kuizindua USA hawajatumia gharama zao kusafirisha msafara wa Rais badala yake zinatumika kodi za watanzania?
 
Mkuu kwa hiyo filamu ku base tu Kaskazini ni sawa?

Dah!! Hivi unajua tuna Mbuga nyingine kubwa mbili kuizidi Serengeti?
Hii filamu imeonesha mbuga zote na kila kivutio kilichopo nchini. Sema tu kama ilivyo ada vijana wa kitanzania mara nyingi huwa tayari kutumiwa na maadui dhidi ya nchi yao wenyewe kupitia kigezo cha utofauti wa kisiasa. Nchi kama Israel, New Zealand, Rwanda nk zimesharekodi filamu hizi za Royal Tour kwa mtindo huu huu. Lakini kwa vile vijana wao wana mioyo ya utaifa, uzalendo, elimu na akili, basi ilikuwa ngumu maadui wa nchi hizo kuwatumia vijana wa mataifa hayo kuandika propaganda za ushuzi kama hizi tunazoshuhudia kwa vijana wetu. Nimeamini ni kwann mwl Nyerere alikataa siasa ya vyama vingi, maana aliwaelewa tosha vijana wa kitanzania walivyo mbumbumbu katika kuchanganua mambo, na kwamba ni rahisi sana wao kuhadaika na pengine kupelekea kuiingiza nchi yao wenyew machafukoni kwa faida ya walio/wanaowatuma. Maadui wa taifa mara nyingi wamekuwa wakipitisha ajenda zao kimya kimya kupitia huu unaoitwa uhuru wa kutoa maoni, wanasiasa uchwara nk.
 
Angalia wewe usivyoelewa mambo ya dunia yanavyokwenda.

Juzi hukusikia maafikiano yaliyofikiwa katika kuwafungulia 'tour guides' wa Kenya kuleta watalii kwenye mbuga za Tanzania?

Sasa mlima Kilimanjaro wa nini kuwa Kenya, kama wanaweza kufaidika nao wakenya maradufu. Watalii wanatua JKIA, wanalala kwenye hotel za Kenya, asubuhi wanasafirishwa kwenye magari ya Kenya kwenda kuangalia utalii uliopo Tanzania. Jioni au kesho yake wanarudi Nairobi.

Hapo unadhani ni nani anafaidika zaidi kwa utalii huo?
mkuu, kwani watalii wanaoitembelea kenya hawaruhusiwi kuja Tanzania? hao watalii kutoka kenya wakifika tz, watalipia kuangalia vivutio vyetu, by the way... wametafutwa na wakenya kwa juhudi zao, na bado na sisi tumefaidika nao...hata kenya nao wana vivutio vya utalii kama mbuga ya tsavo e.t.c.. sasa kama mtalii kashamaliza kutalii kenya..anataka kupanda mlima kilimanjaro kuna kosa? ( na akipanda atalipia) tunawalaumu tu wakenya bure, hata wakisema mlima kilimanjaro uko kenya...bado huyo mtalii hawezi kupandia kenya hakuna njia...atakuja tu tanzania na kulipia $ na nchi itafaidika.
 
Mleta mada na wakenya wako waliokutuma kuja kuandika ujinga huu mmebanwa pabaya, tena katikati ya makalio. Mlikuwa mshazoea kwenda kuihadaa dunia kuwa mlima Kilimanjaro upo Kenya, na kwamba ziwa Nyasa linamilikiwa na Malawi. Dunia ya sasa sio ya kudanganyana tena. Andikeni hata thread 10000 na IDs tofauti tofauti, kikubwa dunia imeshafahamu vivutio vyetu halisi ni vipi na mwenye kutaka kuthibitisha anakaribishwa. Wenye akili tulijua tu kwamba film hii itawaumiza wengi, hasa wale chawa wasiokuwa na moyo wa utaifa, na mabwanyenye wao.
Mkuu sikupingi ila nakuomba fanya kautafiti kadogo, ongea na wadau hasa wa utalii as tour guide, tour operators nk, waulize kuhusu hii sinema nje ya matokeo.

NOTE: Uliza kuhusu hiyo sinema na siyo matokeo ya sinema please. Alafu njoo tujadili.
 
Back
Top Bottom