Nimeangusha pesa ya rambirambi 300,000/= cash mchana huu

Nimeangusha pesa ya rambirambi 300,000/= cash mchana huu

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2012
Posts
17,306
Reaction score
19,885
Wakuu, mchana huu mida ya saa saba nimeangusha Wallet ikiwa na pesa kiasi cha 300,000/= cash. Daaah, roho imeniuma sana aisee na haya maisha yalivyo magumu siku hizi huku mitaani.

Alafu ni mchango wa rambirambi ya msiba wa ndugu yetu aliyefariki kule Bagamoyo, watu 6 wamechangia ambapo kila mmoja alitoa 50,000/= na mimi nikiwa ni mmoja wao. Nikijiondoa mimi hapo ninabaki na deni la 250,000/=

Huu si ndio mwanzo wa kuonekana tapeli aisee? Wakuu, naombeni msaada wenu wa mawazo nifanyaje ili nirejeshe hizi pesa za watu?
 
Kwanza poleee

Ukifanikiwa kutoa hayo maelezo kwa wabongo na wakakuamini bila dot ya shaka
Utakua nabii asiyejijua

Hata marehemu hawezi kuamini, akisikia hayo maneno atafumbua mdomo

Kwa ufupi hata ungesema umeangusha hio 50k yako tuu hamna atakae amini, sio tu hivyo, hata ambaye hajatoa mchango ni ngumu kuamini.

Mbaya uwe na ka sura ka kisanii sanii kama ka Mtanga, huchomoi

Na kwenye msiba watu wasiposhiba, utaona vifungu vifungu vya watu vikikuangalia na kuoneshana kwa misunyo.
 
Kwanza pole kwa msiba

Ushauri wangu waeleze ukweli kuwa umepoteza, hata usipoeleweka basi mwachie Mungu , pesa yenyewe ndogo ,Pili humu JF hawawezi kupitisha rambirambi kwa sababu ya imani juu yako, kingine pia waambie kama wameshindwa kukuamini basi wakupe muda utafute na uwarudishie pesa yao , kingine hapa JF huwezi pata ushauri wakukufanya upate pesa bali utageuka TAPELI.
 
Ukifanikiwa kutoa hayo maelezo kwa wabongo na wakakuamini bila dot ya shaka...
Utakua nabii hujijui tuu..

Hata marehemu akisikia hayo maneno atafumbua mdomo, kwa ufupi hata ungesema umeangusha hio 50k yako tuu hamna atakae amini, halafu mbaya uwe na ka sura ka kisanii sanii kama ka Mtanga, huchomoi
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
[emoji23][emoji23][emoji23]
Ukifanikiwa kutoa hayo maelezo kwa wabongo na wakakuamini bila dot ya shaka...
Utakua nabii hujijui tuu..

Hata marehemu akisikia hayo maneno atafumbua mdomo, kwa ufupi hata ungesema umeangusha hio 50k yako tuu hamna atakae amini, halafu mbaya uwe na ka sura ka kisanii sanii kama ka Mtanga, huchomoi
 
Wakuu, mchana huu mida ya saa saba nimeangusha Wallet ikiwa na pesa kiasi cha 300,000/= cash. Daaah, roho imeniuma sana aisee na haya maisha yalivyo magumu siku hizi.

Alafu ni mchango wa rambirambi ya msiba wa ndugu yetu aliyefariki kule Bagamoyo, watu 6 wamechangia ambapo kila mmoja alitoa 50,000/= na mimi nikiwa ni mmoja wao. Nikijiondoa mimi hapo ninabaki na deni la 250,000/=

Huu si ndio mwanzo wa kuonekana tapeli aisee? Wakuu, naombeni msaada wenu wa mawazo nifanyaje ili nirejeshe hizi pesa za watu?
Laki tatu unaweka kwa Wallet!? Hiyo ni wallet au handbag!?
 
Back
Top Bottom