Nimeangusha pesa ya rambirambi 300,000/= cash mchana huu

Nimeangusha pesa ya rambirambi 300,000/= cash mchana huu

Ushauri wangu waeleze ukweli kuwa umepoteza, hata usipoeleweka basi mwachie Mungu , pesa yenyewe ndogo ,Pili humu JF hawawezi kupitisha rambirambi kwa sababu ya imani juu yako
Ushauri mzuri sana huu. Thanks bro...
 
Kwanza nimecheka ila sio kwa uzuri nimewaza kwa usawa huu hiyo laki 3 ningeipata wapi mie.
Pili. Pole kiongozi ndo maisha lazima ulipe hamna namna
 
Wakuu, mchana huu mida ya saa saba nimeangusha Wallet ikiwa na pesa kiasi cha 300,000/= cash. Daaah, roho imeniuma sana aisee na haya maisha yalivyo magumu siku hizi huku mitaani.

Alafu ni mchango wa rambirambi ya msiba wa ndugu yetu aliyefariki kule Bagamoyo, watu 6 wamechangia ambapo kila mmoja alitoa 50,000/= na mimi nikiwa ni mmoja wao. Nikijiondoa mimi hapo ninabaki na deni la 250,000/=

Huu si ndio mwanzo wa kuonekana tapeli aisee? Wakuu, naombeni msaada wenu wa mawazo nifanyaje ili nirejeshe hizi pesa za watu?
Pole sana mkuu
 
Back
Top Bottom