Hata mimi ilikuwa inaniende fresh tu, ila mambo ya kiimani yaliponiingia nikaipiga chini.
Tena ubandidu haswa, ni udhulumati wa wazi wazi, mie ilikuwa sikukopeshi bila kuweka kitu bondi, tena naangalia thaman ya kitu chenyewe kwa wakati unachukua mkopo, vitu kama nyumba, hati, viwanja, sijui kadi ya gari na pikipiki, nilikuwa sichukui, nachukua vitu vinavyohamishika, vinakuja kukaa mtaani kwangu. Tunaingia mkataba, baada ya muda fulani, usipolipa kitu kinakuwa changu, wengi muda ulikuwa unaisha, sasa nifanyacho, namwambia alipe ile riba, kisha tuanze upya mwezi mwingine, mfano nimempa milioni kwa mwezi inabidi arudishe milioni na laki 3, mwezi ukiisha hana hiyo pesa, basi anipe laki 3, kisha tunarenew mkataba upya, namdai tena milioni na laki 3. Unakuta mtu anarenew mara 3 mpaka 4, kama kaweka gari yake, hapo naitembelea, nikiombea dua nisipate nayo majanga [emoji23]