Nimeanza Biashara ya Kukopesha, naomba ushauri

Per BOT guidance and regulations,mkopeshaji lazima awe na leseni toka BOT. Kama huna na Mimi nakuja kukopa sikurudishii hili twende mahakamani. Hiyo biashara utafirisika na kukosa pesa zako. Kuna loopholes nyingi za kukuzika pesa zako.
Zingatia haya yaliyo semwa hapa.
 
NI riba ya kinyonyaji aisee .
Ila shida za mtu ndo zinamleta kwenye mkopo huu.
Kuna Jamaa yangu alikuwa anakopesha kwa 15% mwezi...ila Jamaa wakamdhulumu pia wakamchomea anafanya black business..alihangaika naona amerudi tena.

Wape riba kwa wiki hata 20%
all In all hii biashara haitadumu jitahidi ufanye jambo la maana angali bado mapema
 
Ni sawa na kusema bank hazina maisha
 
NI riba ya kinyonyaji aisee .
Ila shida za mtu ndo zinamleta kwenye mkopo huu.
Kuna Jamaa yangu alikuwa anakopesha kwa 15% mwezi...ila Jamaa wakamdhulumu pia wakamchomea anafanya black business..alihangaika naona amerudi tena.

Wape riba kwa wiki hata 20%
all In all hii biashara haitadumu jitahidi ufanye jambo la maana angali bado mapema

Ni sawa na kusema bank hazina maisha
Protection+insurance
 
Duh 10000 kila siku analipa jero. Kweli masikini atabaki kuwa maskini daima milele amina
𝐍𝐢 𝐤𝐮𝐛𝐰𝐚 𝐬𝐚𝐧𝐚 𝐚𝐦𝐚 𝐧𝐝𝐨𝐠𝐨 𝐬𝐚𝐧𝐚?

𝐤𝐢𝐥𝐚 𝐬𝐢𝐤𝐮 𝐣𝐞𝐫𝐨 𝐤𝐰𝐚 𝐬𝐢𝐤𝐮 7 𝐢𝐧𝐚𝐤𝐮𝐰𝐚 3,500 𝐦𝐤𝐮𝐮

𝐤𝐰𝐚𝐧𝐠𝐮 𝐧𝐢 2000 𝐤𝐰𝐚 𝐰𝐢𝐤𝐢.
 
Maana yangu ni kwamba kwa mwezi hiyo ni interest ya 50%. It's all about business nimeshangaa tu sikuwahi fikiri kama kuna ukopaji wenye interest kubwa hivyo
 
kitaani huku wamama hawajui hizi calculation ye ilimradi jambo lake limeenda kwa mkopo wako mtakutana kwenye rejesho
mfano mama mmoja anafanya biashara ya samaki. Anachukua laki 1 kwangu kila wiki. Nishamzoea.

analeta 20,000 kila jumatatu.

Na huyo ni mama mchungaji.

Jana nimepitia kitabu changu cha madeni nimekuta kuna laki 5 nje.

nimejiuliza sana hivi nikizimwa hapa ntakuwa.mgeni wa nani😅😅😅
 
Bora sana kukopesha kwa watu kama hawa kuliko kuziweka kwenye kibubu zikae mwaka bila kuzaliana.

Risk ni kubwa sana, watu nisiowajua huwa nawaambia walete mali zao waweke bondi.

na wanaleta kweli
 
Kwahiyo hiyo anayofanya sio jambo la maana?
 
Itafute na askari(polisi) kwa ajili ya kutishia kwa wale wanaochelewesha
 
Ushuru wenyewe tunalipa 200 sokoni ndio iwe jero kila siku?
 
Sijui imani ipi inaruhusu riba. Kwa uoande wangu kitu asichokidhiria mola wako hakina faida kwako. Unaweza ukafaulu duniani na akhera ukawa mweny khasara. Fanya kazi isiyo na mushkel
Tuko Duniani Wacha tufaidi vya Duniani kwanza,tukifika ahera tutajua cha kufanya
 
Mnawapata wajinga,kwa nini wasikope kwenye mitandao ya simu?

Pesa ya riba mbaya sana,niliwahi kopa 700k kwa makubaliano ya kulipa riba ya 15% kwa mwezi kwa kila Salio hadi umalize.

Hadi namaliza ndani ya miezi 3 nilipa riba na principal zaidi ya mil.1 na laki hivi.

Kuanzia hapo nikaapa sutokuja tena Kukopa pesa za riba iwe Benki au kwa mtu.
 
Huwezi kuzimwa yote,ni nadra Sana ukazimwa mtaji plus riba,unaweza recover 450 plus
 

Hivi kuna mtandao kurupu unakupa milioni mzee!?

Riba ni mbaya nami nakubali hilo, hata aliyetuumba katukataza kwenye hilo. Kifuoi kuna shida mtu anakuwa kataitiwa kisawa sawa, sasa hapo mtu aliposhikwa hana namna ndio unamgonga ni pesa fulani haramu mnoo.
Kuna katuni fulani panya mmoja kanaswa na mtego panya wenzie wamepanga foleni ya kumla uroda, ukicheki ile utaelewa.

Riba ni mbaya, mbaya, mbaya kupita maelezo na hapo ndio ilipotiwa uharamu, badala ya kumsaidia mtu unamnyonya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…