Nafanya biashara ya pesa mkuu. Kama zilivyo benki zote za biashara
riba zangu ni kwa siku 7 unaleta elfu 2 kwa kila elfu 10 unayochukua.
kuna wengine wanachukua kwa siku 3, 4 mpaka 5 lakini interest iko palepale.
View attachment 2160027
nakusanya hio hela kutoka kwa wakopaji wadogo wale wa teni teni every day.
Nashukuru Mungu mtaji umekua kwa kasi sana kutoka 100,000 mpaka sasa inagonga laki 6.
nakopesha wale ninaowajua kiundani.
nisiowajua wanaweka vitu bondi.
CHANGAMOTO
mpaka sasa changamoto yangu ni mtaji umepungua wakopaji wamekuwa wengi, tena wale LEGIT wanaoletwa na wateja WAKONGWE.
imagine kama jana kuna mmama kaletwa anataka laki 1, arudishe 120k leo.
nilishangaa sana lakn nilipouliza kiundani waliniambia wanaenda ku top up mkopo wao kwenye kikundi na huwa wanafanya hivyo ili WAPATE MIKOPO MARA 2.
Hii biashara inalipa ila inahitaji uwe mtu makini sana.
SIO KILA MTU NI WA KUKOPESHA
CHUNGUZA KABLA HUJAKOPESHA.
ULIZA ULIZA KWA WANAOMJUA
kokudo note something