Nimeanza Biashara ya Kukopesha, naomba ushauri

Poa.
 
Mimi wanakimbia nikiwaambia 20% riba kwa siku 14 hii ipoje kwako
Kwangu sikimbiwi mkuu sana sana mimi inafikia hatua naishiwa hela kabisa ya kukopesha.

Jana tu mtu kachukua elfu 90 anadai ni emergence anairudisha leo saa 3 (ni mmama tunaivana sana) anairudisha kwa riba Tsh elfu 8.

asubuhi napokea sms kama hii. Riba ni ile ile ishaeleweka na watu hawaipingi

cha msingi uweke msimamo wako.

mi kuvumilia wiki 2 siwezi aisee
 
Sidhan kma utaweza kuiendesha long term na kwa ukubwa kwa hiyo strategy
Mkuu kwangu imefikia hatua sasa natafutwa, na wanajipangia riba wenyewe.



huyu alichukua jana 90,000
akarudisha 98,000 leo tarehe 24.3.2022

Aliniomba laki 1 nikawa sina ndo nikampa 90.

kairudisha hio kisha ananitumia sms anataka 30k.

riba wamejiwekea 3,000 kesho saa tano naifuata.

mambo ya long term or short term tumuachie Mungu mkuu.

Nipo kwenye gem toka mwaka jana na mpaka sasa nalisongesha tu cha muhimu kwa watu nisiowaamini huwa nabeba vitu naweka bondi.
 
Nimejaribu kuweka Tangazo mtaa wa pili kwamba nakopesha.

duh nimepigiwaa simu hizo mpaka nimechoka!

Msimamo wangu uko pale pale, sitoi hela bila kitu kuwekwa bondi.

baada ya hapo ndio tunaandikishana.
Hahaha duh
 
Sidhan kma utaweza kuiendesha long term na kwa ukubwa kwa hiyo strategy
Kwa Taarifa Yako,
Hii Biashara nimeiwekea Malengo Ya mwaka huu 2022, ilete pesa sio chini ya milioni 1 na nusu net profit (riba)

nitaendelea nayo sana hata kama nikihama huu mtaa ninaoishi.

nishajua chocho za kuwapatia hawa wanaokopa sana.

π’Žπ’‚π’π’†π’π’ˆπ’ π’Žπ’‚π’Œπ’–π’– 𝒉𝒂𝒔𝒂:
mpaka ije ifike December 2022 nimepanga kununua kiwanja cha laki 7 na kuanza ujenzi wa chumba na sebule Haraka.

na inawezekana kwa sababu,

napata faida ya Tsh 40,000 mpaka 65,000 kwa wiki.

ikiendelea hivyo baada ya miezi 8 ntakua na NP of 1,280,000 kwa average ya 40,000 kila wiki.

pembeni nako nafanya udalali sana.

huu mwaka lazima nitimize malengo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…