Kama isingekuwa maharamia walioiteka CCM, hakika nchi hii ilikuwa kwenye njia nzuri ya kuelekea kwenye demokrasia kamili, haki na uhuru kamili. Bunge lingekuwa huru, mahakama ingekuwa huru. Fikiria wakati wa chama kimoja, watu walikuwa na uhuru wa kutaka Serikali 3, tena wakiongea kwa uhuru ndani ya Bunge. Na serikali ya Mwinyi iliridhia. Mwalimu Nyerere akawa mkali, akazuia kupitia vikao vya chama. Na msingi wake mkubwa ukawa kuwa CCM ilani yake wakati wa uchaguzi ilikuwa kuendelea na Serikali 2, hivyo haiwezi kubadili katikati ya muhula. Akawataka wanaotaka Serikali 3, wasubiri wakati wa uchaguzi, waende na hiyo hoja kwa wananchi. Nyakati hizo, Watu walikuwa wakibishana kwa hoja, hakuna aliyetekwa, hakuna aliyebambikiwa kesi wala kuuawa. Fikiria kwa hali ya sasa, kungetokea nini!! Kwa sasa viongozi wa CCM na Serikali, bila shaka kwa sababu ya kukosa weledi, akili kubwa, na kwa kukosa uwezo wa kujenga hoja, wanategemea kuwanyamazisha wote wenye hoja kinzani kwa kuwateka, kuwaua na kuwabambikizia kesi za uwongo! Wameua Mahakama, wameua bunge. Hili ni fundisho, watu wenye uwezo mdogo wa akili, wasio na weledi, wasioweza kujenga hoja, hawastahili kuwa viongozi, maana watatumia maguvu kila mahali, hata mahali palipohitaji akili, weledi na hekima.