kush moker
JF-Expert Member
- Feb 11, 2016
- 579
- 367
Push up,nishaanza nazo soon jogging itaanza
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ha ha ha ha hamna mzee hata wewe unaweza, usipige nyingi kwa mara moja. Anza hata tano halafu unaongeza taratibu. Mimi nikitaka kurudisha mwili shati likae napiga push ups tu mwezi mmoja tu nisharudi. Mimi namshukuru Mungu nikitaka ku-gain wait nafanya mazoezi nisipofanya napoteza kg hadi tano kwasababu hata kula sili sisikii njaa.
Duh si mchezo 100 kwa mpigo! Mimi napiga 30 au 40 mara kumi. Ndani ya nusu saa.Ni kweli anatakiwa aanze kidogo kidogo asiforce akaleta shida zingine. Mimi nilianza mwaka jana Jan push ups 5 kwa mpigo ilikuwa ngumu sana. Nimeendelea taratibu nikiziongeza kila mwezi taratibu mdogo mdogo. Kwa sasa, baada ya miezi 18 ninapiga 90-100 kwa mpigo. Plan yangu ni kupiga 150 kwa mpigo ikifika Dec 2018.
Soweto..Arusha.Timu yako iko wapi? Nilikuwa napiga bball jtan na ijumaa ila nilisimama kwa muda nategemea kurudi.
Ushaanza hata kidogo?
Duh si mchezo 100 kwa mpigo! Mimi napiga 30 au 40 mara kumi. Ndani ya nusu saa.
Hongera mkuu endelea hivyo hivyo.Yes ni 100 kwa mpigo kutoka 5 nilipoanza.Ila umenichallenge kwamba badala ya kupiga 100 tu kwa mpigo asbh na jioni ninaweza kupiga hata 200 kwa mafungu mawili ya 100 100 asbh na jioni nikawa nimeimprove kwa 100%.
Sasa zuri zaidi, nimethibitisha beyond doubt kwamba mazoezi ni muhimu sana kwa afya ya mwili. Mfano, kabla sijaanza mazoezi, nilikuwa naumwa kichwa mara kwa mara kiasi kwamba Panadol zilikua sehemu ya maisha yangu, ilikuwa lazima niwe nazo za dharura kwenye draw ofisini, bag nikisafiri etc etc. Lakini kwa sasa siumwi tena kichwa hovyo hovyo na hizo Panadol ni karibu mwaka sasa sijazitumia-hili kwangu ni bonge la achievement especially knowing kwamba chemicals zina madhara kwa mwili. So ninawaencourage wale ambao hawajaanza mazoezi shime waanze sasa kwani hakunaga kuchelewa kwenye maisha.
gym tunaenda ku-show off na kutizama misambwanda ya wadada vibonge wa mjini.Hata mi napigiaga chumbani tu, nashangaa wanaohangaika na Gym
Hongera sana.Mazoezi ni dawa nzuri sana ya magonjwa mbalimbali pamoja na ubongo kufanya kazi. Mimi nafanya jogging kwa dk 15, viungo kwa dk 15 na pushups kwa dk 15. Nilianza mwaka 2002 nikiwa 33yrs bado naendelea sasa hivi nipo 49yrs. Napenda kufanya 4-5 days a week. Tupende mazoezi jamani