Uchaguzi 2020 Nimebadili maamuzi, wacha watuone wajinga tu ila na mimi kesho naenda Kupiga Kura

Brian Spilner

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2016
Posts
1,915
Reaction score
5,750
Kulingana na uhalisia wa mambo, sikuamini kama kuna hata chembe ya haki na nguvu ya kura yangu. Ila kama na wao wameogopa kiasi hiki, basi na mimi nitapiga kura, wacha iibiwe, wacha iharibiwe.

Sehemu kubwa ya Morogoro mjini umeme umezimwa tangu asubuhi. Labda kama wamerudisha dikika hizi, wanalengo gani, wanajua wenyewe.

Mitandao ya kijamii ndio kama mnavoiona.

Kama ulinotice, kuna muda simu za kawaida na msg zilikua hazitoki kabisa mchana.

ITV walikata matangazo ya Aljazeera

Star TV Wamekata matangazo ya BBC.

Inaweza kura yangu isiwe na msingi sana, lakini kama kuna watu wanaweweseka kiasi hiki, na wao ndo wanaojitamba, basi kipo wanachokihofia.

Nitapiga kura na nitaiachia nature iamue matumizi ya kura yangu. Ikienda kwa niliempigia sawa, ikiibiwa sawa, ikiharibiwa sawa.

Nafahamu kuna watu hawakupanga kupiga kura kulingana na hali iliyozoeleka. Nashauri tukapige kura, hata wasipoiruhusu kura yako iamue, wataelewa uhalisia uliopo mtaani, pengine wanaweza utumia uhalisia huo kwa namna chanya.

UPDATE
Pichani (Find the attachment) ni uthibitisho wa nilichokiamua.
Sio kwamba sielewi uwepo wa hujuma, sio kwamba sielewi Commission ni mtetezi wa maslahi ya chama, sio kwamba sioni yanayojiri kwenye vituo mbali mbali ila nimepiga.

Kituo nilichopigia kura kuna mawakala wawili tuu, wakati kuna ushiriki wa wagombea kutoka vyama vinne. Silaumu mtu kuhusu mawakala, sijui wamekwama wapi, hata waliopo sijui ni wa chama kipi na kipi. Ila pamoja na viashiria vyote, bado kura nimepiga.

Nimesafiri mpaka Dodoma kata ya chamwino, Area A ili nitimize hili.
View attachment 1614527
 
Hongera sana kwa kubadili maamuzi yako dakika za mwisho. Ni Lissu na Devotha Minja bila shaka ndiyo machaguo yako sahihi kwa hapo Moro town.

Mimi msimamo wangu uko pale pale. Sitapiga kura hiyo kesho. Ila nawatakia uchaguzi mwema wapenda mabadiliko wote nchini.

CCM and Company Limited must go!
 
Tell your friends too to tell yheir friends to kama mlivyofanya 2015 na kura hazikuyosha bado
 
Hongera sana kwa kubadili maamuzi yako dakika za mwisho. Ni Lissu na Devotha Minja bila shaka ndiyo machaguo yako sahihi kwa hapo Moro town.

Mimi msimamo wangu uko pale pale. Sitapiga kura hiyo kesho. Ila nawatakia uchaguzi mwema wapenda mabadiliko wote nchini.

CCM and Company Limited must go!
Ninasikia Devota anaweza akamstaafisha mtu siasa za bungeni hapo Moro mjini,vp kunaukweli gani
 
Nipo guest jiran na kituo nilichojiandikisha kupiga kura ,nimetoka mkoani kuja dar kwa kazi maalumu ya kumchinja MTU ,wacha kula ziibwe wacha wachakachue ilaa salamu wataipata huko ikulu watakaa wakatafakar vizur na kutenda mema
 
Hata mimi baada ya kutafakari, nilihitimisha kama wewe.
Waibe, wachakachue, waharibu kura, watajijua wenyewe.
Naenda kupiga kura.
 
Kulingana na uhalisia wa mambo, sikuamini kama kuna hata chembe ya haki na nguvu ya kura yangu. Ila kama na wao wameogopa kiasi hiki, basi na mimi nitapiga kura, wacha iibiwe, wacha iharibiwe.

Sehemu kubwa ya Morogoro mjini umeme umezimwa tangu asubuhi. Labda kama wamerudisha dikika hizi, wanalengo gani, wanajua wenyewe.

Mitandao ya kijamii ndio kama mnavoiona.

Kama ulinotice, kuna muda simu za kawaida na msg zilikua hazitoki kabisa mchana.

ITV walikata matangazo ya Aljazeera

Star TV Wamekata matangazo ya BBC.

Inaweza kura yangu isiwe na msingi sana, lakini kama kuna watu wanaweweseka kiasi hiki, na wao ndo wanaojitamba, basi kipo wanachokihofia.

Nitapiga kura na nitaiachia nature iamue matumizi ya kura yangu. Ikienda kwa niliempigia sawa, ikiibiwa sawa, ikiharibiwa sawa.

Nafahamu kuna watu hawakupanga kupiga kura kulingana na hali iliyozoeleka. Nashauri tukapige kura, hata wasipoiruhusu kura yako iamue, wataelewa uhalisia uliopo mtaani, pengine wanaweza utumia uhalisia huo kwa kwa namna chanya.

Umeme Upo mwingi na Mimi hapa nautumia sijui wewe upo Morogoro ipi.
Halafu Umeme saa hizi unaathiri nini kwenye kutoa tiki kwa Magufuli?
Kapige kura basi.
 
Kulingana na uhalisia wa mambo, sikuamini kama kuna hata chembe ya haki na nguvu ya kura yangu. Ila kama na wao wameogopa kiasi hiki, basi na mimi nitapiga kura, wacha iibiwe, wacha iharibiwe.

Sehemu kubwa ya Morogoro mjini umeme umezimwa tangu asubuhi. Labda kama wamerudisha dikika hizi, wanalengo gani, wanajua wenyewe.

Mitandao ya kijamii ndio kama mnavoiona.

Kama ulinotice, kuna muda simu za kawaida na msg zilikua hazitoki kabisa mchana.

ITV walikata matangazo ya Aljazeera

Star TV Wamekata matangazo ya BBC.

Inaweza kura yangu isiwe na msingi sana, lakini kama kuna watu wanaweweseka kiasi hiki, na wao ndo wanaojitamba, basi kipo wanachokihofia.

Nitapiga kura na nitaiachia nature iamue matumizi ya kura yangu. Ikienda kwa niliempigia sawa, ikiibiwa sawa, ikiharibiwa sawa.

Nafahamu kuna watu hawakupanga kupiga kura kulingana na hali iliyozoeleka. Nashauri tukapige kura, hata wasipoiruhusu kura yako iamue, wataelewa uhalisia uliopo mtaani, pengine wanaweza utumia uhalisia huo kwa kwa namna chanya.
Acheni ujinga wa kujitekenya na kucheka wenyewe. Mbona Moro umeme upo tu wala haujakata.

Mtajificha chooni wakati wa matokeo
 
Back
Top Bottom