Nimebaki na elfu 4 tu kwenye m-pesa naona aibu kwenda kwa wakala kuitoa

Nimebaki na elfu 4 tu kwenye m-pesa naona aibu kwenda kwa wakala kuitoa

Wakuu, kufulia kusikie tu kwa jirani aisee. Hapa nilipo nimefulia kiasi kwamba nimebaki na elfu 4 tu iko kwenye m-pesa. Sasa nataka kwenda kwa wakala kuitoa lakini naona aibu wakuu.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
JamiiForums-95035089.jpg
 
Wakuu, kufulia kusikie tu kwa jirani aisee. Hapa nilipo nimefulia kiasi kwamba nimebaki na elfu 4 tu iko kwenye m-pesa. Sasa nataka kwenda kwa wakala kuitoa lakini naona aibu wakuu.
Pesa yako mwenyewe, unaona aibu kuitoa kwa wakala?? Wewe una matatizo ya Akili
 
Mi nishwahi kuingia kwenye hivi vimin bank nikatoa buku nikasepa
Fresh tu, si hela yako bana. Mtu anawaonea aibu watu ambao wala hawamsaidii kwa lolote. Kujishtukia ni ugonjwa mkubwa sana wa akili.
 
2011 nikiwa chuo mshkaji wangu alibakiwa na 6000 bank nmb...af mfukon hana hata 100 ya kuvuka kurud kigamboni akona kama noma acha iwe noma akazama ndani kwenye foleni kutoa hela kwa teller maana Atm 5000 ilikua lazima ibaki na 1000 haitoki kwa mashine.
Bank teller alimshangaa ila mchiz akakaza sura...nilicheka sana aliporud hostel na kunipa hii habari
 
Kweli tumetofautiana
Yani nione aibu kutoa elf 4?
Hata buku natoa as long as ni yangu sijamwomba mkopo wakala
 
Mimi kuna siku nlkua natoa buku 3
Nkakuta mdada yupo pale kwa wakala haondoki
Na mimi nikasema hapa kama nanunua condom
Sitaki huduma had nibaki peke yangu

Ghafla akaongezeka mteja mwingine wa 3
Akasema naomba kutoa pesa mpesa
Wakala akamuuliza kiasi gani
Akajibu elfu 2

Nkasema hiiiiii kumbe mimi ni tajiri
Nkamwambia wakala natoa pesa hapa af 3
 
Pole sana mkuu unaweza kutoa ata elfutatu mkuu ni kawaida hakuna atakayekushangaa
 
Back
Top Bottom