Nimebaki na elfu 4 tu kwenye m-pesa naona aibu kwenda kwa wakala kuitoa

Wakuu, kufulia kusikie tu kwa jirani aisee. Hapa nilipo nimefulia kiasi kwamba nimebaki na elfu 4 tu iko kwenye m-pesa. Sasa nataka kwenda kwa wakala kuitoa lakini naona aibu wakuu.
....tafuta wakala wa kiume.!
 
Uoga wako ndiyo umasikini wako ,mbona kawaida sana! Kheri wewe una Buku 4, unaweza ukapiga Songesha ukatoa zaidi ya hiyo ,wengine wanadaiwa kabisa M-pesa ni Negative.
 
Wakuu, kufulia kusikie tu kwa jirani aisee. Hapa nilipo nimefulia kiasi kwamba nimebaki na elfu 4 tu iko kwenye m-pesa. Sasa nataka kwenda kwa wakala kuitoa lakini naona aibu wakuu.
Ujahisi njaa ww bado.
 
Mkuu huko sio kufulia,Kuna watu huwa tunasota mpaka Mia mbovu kuipata mtihani sana
 
Eh ww mbn wengine huwa tunaenda na buku jero[emoji16]
 
Unaionea aibu pesa yako halali?kachukue aftatu yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…