Unaweza kueleza kwa jinsi nyingi tu, lakini ishara za mazungumzo yako ni za kichawa. Haupo fair katika ukosoaji wala uungaji mkono wako. Of kozi, huwezi kuliona hilo kwasababu ndivyo ulivyo.
Hayo mengine ya mindset, depth na dimensions nakuachia wewe, ila jaribu pia kuwa na ngozi ngumu. Upo kwenye social media hapa na siasa ni contact sports!
Unaongelea "ishara za mazungumzo yako" kwa sababu huna data.
Una speculate. Una jump to conclusions. Huna ushahidi.
Kwa nini unaongelea "ishara za mazungumzo yangu" wakati mazungumzo yote yapo hapa JF?
Kwa nini usinukuu moja ya posts zangu tuchambue na mimi nikuoneshe kuwa sipo hapa kumpigia jaramba mtu?
Huwezi kuweka nukuu ya maneno yangu nilipomtetea SSH kwa namna ambayo unaweza kusema mimi ni chawa wa SSH.
Lakini, mimi naweza kukuwekea post yangu ya leo leo, masaa machache tu yaliyopita, nilipomrekebisha kada wa CCM aliyekuja hapa kupotosha habari za SSH kuongoza vizuri Tanzania kwenye bei ya mafuta.
Nikaweka data za dunia na kusema kwa nchi zenye bandari za ukanda wetu Tanzania ina bei ya mafuta kubwa zaidi.
Tena kada wa CCM alivyoona nimemshinda kwa data akajifanya kujibaraguza kwamba tunasema kitu kimoja, nikamrekebisha kumwambia hapana, logically.
In fact hata katika uzi huu nimeandika hapo juu kwa nini Zitto hamkosoi zaidi SSH, anashikilia kumkosoa JPM ambaye kashajifia zake? Sasa hapo nakuwaje mtetezi wa SSH?
Sasa mimi chawa gani wa SSH ninayewarekebisha makada wa CCM wanaopotosha ukweli kwa kumsifia SSH?
Kama unataka kunishambulia, nishambulie kwa data specific. Usiende kwa mihemko ya maneno matupu.