Nimechagua kumchukia Zitto Kabwe kutokana na kuwa na chuki na Hayati Magufuli

Nimechagua kumchukia Zitto Kabwe kutokana na kuwa na chuki na Hayati Magufuli

Wakuu nimekuwa na chuki sana na Huyu zito.
.
Namchukia sana kutoka rohoni mwangu.
.
Amekuwa na chuki sana na JPM kila akipata forum ya Kuzungumza anamzungumza Kwa mabaya JPM.
.
Unakuwaje na chuki na mtu ambae hawezi kukujibu Kwa lolote

View attachment 2215113
Nakushauri nawe kaa kimya wote mkitulia naye akaona hakuna wa kumjibu ataacha.
 
U nail it Mzee K
.
Ila Tunataka Kusema Zito haoni yanyoendelea Mpaka Sasa hapa nchini?
.
Je ishu ya kupandisha bidhaa awamu hii imekuwa too much, na sidhani km tunapaswa kutumia kigezo Cha Vita.
.
Leo Hii Zanzibar mafuta ni 2600+ ina maana wao anayachukulia dunia ipi?
.
Walichokifanya ni serikali kupunguza Kodi ili Bei isipande saana, Sasa kwasasa imekuwa hata bidhaa zinazozalishwa ndani na zilishazalishwa kitambo ziko kwenye magala wafanya biashara wanazipandisha tu hovyo.
.
Ni kama wamekosa mtu wakuwakalipia! Nondo Bai juu, saruji Bei juu, vyakula juu, mafuta juu, mabati juu, hata karatasi Bei juu duh! This is too much

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Moja ya matatizo yangu kuhusu criticism za Zitto, na hili linafanya hoja ya bias against Magufuli iwe na nguvu, ni ukweli kuwa Zitto hatoi criticism kwa Rais Samia na serikali yake.

Yani anajishughulisha sana kumsema rais marehemu, wakati tuna rais anayeishi sasa hivi ana madudu kibao.

Zitto anakuwa ni kama kashachagua kuwa anti Magufuli na pro Samia wakati Samia mwenyewe ni muendelezo wa Magufuli ila anajua kuuma na kupuliza tu.
 
Kwa nini swali liwe kaongea nini na sio kaongea nani?

Kwani hatuwezi kufanya analysis inayochanganya vyote (nini na nani)na kusema kwamba.

1. Zitto ametoa outbursts ambazo ziko emotional zaidi na zinaonesha ana bias against Magufuli.

2. Lakini, kuwa na bias against Magufuli hakukufanyi usiweze kusema ukweli kuhusu Magufuli. In fact in some cases bias dhidi ya mtu ndiyo inaweza kukufanya uchimbe deep na kugundua ukweli ambao watu wasio na bias hawawezi kuugundua.

3. Hivyo, hoja za mtu mwenye bias against Magufuli, zinatakiwa kuchunguzwa kwa kina zaidi kwa kujua kwamba si za mtu neutral, ni za ntu mwenye bias against Magufuli.

4. Hilo halimaanishi hoja hizo zitupiliwe mbali kwa sababu mtu ana bias against Magufuli.

5. Moja ya namna ya kuziangalia hoja hizi ni kuangalia watu wengine ambao hawana bias against Magufuli wamesemaje. Tunajua hoja ya serikali kukopa sana si ya Zitto tu, in fact hata watu waliokuwa wanamkubali Magufuli kama Spika aliyejiuzulu wamelisema hili. Kwamba serikali inakopa sana. Kwa hiyo hii si hoja ya Zitto tu. Rais mwenyewe kasema serikali imefanya miradi mingi kwa kukopa na kukopa kunazidi, ingawa hakujazidi sana. Hivyo suala la serikali kukopa ni fact, si spin ya Zitto tu.
Mkuu, hakuna anayepinga mikopo au mkopo haikuwepo enzi ya Mzee.

Tatizo ni moja tu, unakopa nini na kwa ajili ya nini. Hili ni tatizo kubwa sana la Nchi hii miaka mingi. Hatuna vipaumbele vinavyoeleweka.

Ni kweli Kwamba miradi yetu mingi tena ya kimkakati ambayo leo hii imekuwa chechefu tulikuwa tukifanya kwa pesa zetu za ndani kitu ambacho tulidanganywa?

Ni Kwamba Magufuli as President (as he then was) alikopa kwa siri mikopo mikubwa tena Commercial lakini akipeleka kwenye miradi.?

Ni Kwamba Hoja ya Zitto haina tofauti na hoja nyingi za sasa za wachumi wengi ambao hata kipindi kile waliminywa wasiseme?
.
What I know ni kwamba Magufuli hakuwa Mungu. Ni binadamu. Hata anavyokosolewa leo ni kutekeleza moja ya utatu wa ubinadamu wake tu basi Ila Tumkosoe Kwa hekima

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Huwezi kujua ugumu wa maisha unaoyokana na mikopo umiza ya jiwe,sababu unaishi kwa shemeji yako ana kulaza sebuleni.
Nyie kweli ni mapopoma mnahamisha magoli kwamba maisha magumu yasasa nikwasababu ya mikopo ya hayati magu? Huo ujinga kawaelezeni wajombazenu vyeti feki.
 
Hapa pia kwa kiasi flani unajisema mwenyewe. Hivi kwa maoni yako, Magufuli alifanya mazuri mangapi? Tuanzie hapo
Kuna watu wana kushangaa wewe kuwa, pamoja na mapungufu ya JPM, lakini unashindwa kuona mazuri yake mengi.
Tatizo langu na Magufuli si kwamba hakufanya mazuri.

Tatizo langu ni kwamba hata alipofanya mazuri, aliyafanya vibaya, na hivyo hata kusifia inakuwa vigumu.

Yani Magufuli ni mtu aliyeweza kuja na overall ideas nzuri nyingi.

Mifano michache, kubana makampuni ya madini ilikuwa idea nzuri sana. Execution ilikuwa horrible.

Kutetea wakulima wa korosho wapate bei nzuri na kujaribu kuwabana middle men ninsehemu ya kazi za serikali kwenye regulation. Execution ilikuwa horrible.

In principle, infrastructure projects are very much needed. Tazama executiin watu wanavyojengq madaraja kama la Tanzanite, viwanja vya ndege Cahato na kununua ndege bila hata business plan, horrible.

Kurudisha nidhamu serikalini ikikuwa idea nzuri sana. Lakini nidhamu yenyewe imerudishwa kwa woga bila mpango endelevu. Horrible.

Kwa hivyo, kwangu mimi Magufuli ana matatizo ya execution hata pale anapokuwa na the right vision.

Ila pia, kauli zisizo staha kwa Watanzania na Magufuli zilipotolewa na Zitto, kwamba wanaompenda Magufuli wakazikwe naye Chato, nilizilaani na kusema hizo si sawa, zinagawanya watu na sioni tija yake. Hivyo sikutetea chuki binafsi dhidi ya Magufuli.
 
Hayo mambo ya Marekani tuwaachie wenyewe, sisi hayatuhusu, hapa tunazungumzia bongoTZ.

Mambo mengi yalifanyika kwa hela za ndani na mikopo ikiwepo. Ni uongo kusema kuwa kulikuwa na propaganda ya kusema “kila kitu” kilifanyika kwa pesa ya ndani. Kushindwa kwako Kwa makusudi (najua wewe ni mtu smart sana) kuona kuwa huo ni uongo, inasikitisha sana.
Ukishakuwa unafadhiliwa na Marekani huwezi kusema mambo ya Marekani hayakuhusu. Unatakiwa kuwa na utashi angalau kujua huyu Mmarekani anafanyaje kunifadhili mimi na mimi nisiwe mfadhili wake kibajeti? Ukishindwa hilo unapepea umasikini wa milele.

Na ni ukweli usiofichika kwamba serikali na hususan rais Magufuli alijitapa sana kwamba tunafanya miradi kwa pesa zetu wenyewe.

Sasa hivi rais Samia kaanza kufunguka kutueleza kwamba tunakopa sana tu.
 
Wakuu nimekuwa na chuki sana na Huyu zito.
.
Namchukia sana kutoka rohoni mwangu.
.
Amekuwa na chuki sana na JPM kila akipata forum ya Kuzungumza anamzungumza Kwa mabaya JPM.
.
Unakuwaje na chuki na mtu ambae hawezi kukujibu Kwa lolote

View attachment 2215113


Kusema ukweli wa mambo ndio chuki??!!, sasa hebu tuambie Zitto alipaswa asemeje katika jambo hilo la Mikopo ya kibiashara aliyoingia Magufuli ili Zitto asionekane kwamba anayo "chuki" dhidi ya Magufuli??!!---- Hebu tuambie ilimpasa asemeje katika hali hiyo??
 
Nakubaliana na wewe Kwa sehemu kubwa, ila sentensi ya mwisho hapo imeonyesha tena unconscious bias yako naweza kusema dhidi ya JPM. Eti Samia anajua kuuma na kupuliza, kweli?? Wakati toka aingie kauli zake kuhusu umeme wa elfu 27, bei ya mafuta, kupanda bei bidhaa na kadhalika ni kauli ambazo ni za kuuma na kusagia chumvi kwenye kidonda. Wewe una mapenzi kiasi na Samia na chuki dhidi ya JPM. Unajaribu kuwa fair, lakini mwisho wa siku dhamira yako ndani kabisa ina kuumbua.
Mimi JPM kaipa familia yangu nyumba Oysterbay na alikuwa anaongea na baba yangu tangu alivyokuwa waziri.

Hivyo kwenye suala la chuki binafsi sina sababu ya kuwa na chuki binafsi naye.

Ni tofauti za kifalsafa tu.

Huyo Samia simjui. Alivyoingia kwenye siasa mimi nilikuwa nishaondoka Tanzania. Mimi nawajua familia za Nyerere, Mwinyi na Mkapa. Hao wengine wamekuja too late for me.

Ninavyosema Samia anajua kuuma na kupuliza ni pale ambapo anawapiga tozo halafu mnamlilialilia anapunguza, anajua kuwapiga kiswahili cha "yale mambo yetu bado yapo" bila kuongeza mishahara, anajua kuwa infantilize nchi nzima mmefanywa watoto mpaka rais anaita watu "mwanangu", nanyi mnamuita mama kama hamna mama zenu vile.

Ni hivyo tu.

I really do not see a fundamental difference between Samia and Magufuli, apart from the cosmetic and theatric performatives.
 
Sijapenda Zitto alivyosema wanaompenda Magufuli wakazikwe naye Chato.

Hii kauli ya Zitto ni mipasho ya mtaani ambayo haifai kutamkwa na kiongozi wa hadhi yake.


Kwanini lugha hiyo inaiita mipasho??!!, kipindi fulani wapinzani NCCR waliposhika kasi ya kuchukua nchi Nyerere aliulizwa kuhusu hao NCCR ya akina Mrema na Mabere Marando kuchukua nchi na alijibu: "I can not leave this country to the dogs", aliongea maneno kama hayo kama nakumbuka vyema, sasa pima kati ya hizo lugha mbili ya Zitto na ya Mwalimu ipi ni ya kimipasho??!!
 
Rudia tena kusoma ulichoandika! Ni dhahiri kuwa hutakuja kuelewa kwanini watanzania wengi walikubaliana na kumpenda JPM.

Kama nilivyosema awali, mambo ya Marekani tuwaachie wenyewe, hapa tunaongea siasa za ndondo cup, siyo premier league.

Hao Marekani wenyewe ile version yao ya wamachinga, zile tent [emoji904] communities chini ya overpass na pembeni ya mabarabara wameziacha kama zilivyo. Lakini sisi tumewafukuza wamachinga eti kusafisha miji ili “wazungu” wasione “uchafu.” Wakati Leo miji Kama Seattle, Phoenix, Tacoma, Minneapolis na kadhalika inavunda kwa uchafu na watu kuishi kwenye make shift tents [emoji904]
Sawa basi, tuache Marekani. Kwanza Marekani si nchi, ni idea.

Are Tanzanians overly fixated on the past at the expense of not planning for the future?

Why are we still so fixated on Magufuli while there is a current sitting president with a lot of issues to focus on?
 
HIVI UNAPATA WAPI NGUVU YA KUZUNGUMZA JAMBO BILA HATA YA KUWA NA DATA?

NI KICHWA CHA MWENDAWAZIMU PEKEYAKE TU NDIO KINAWEZA HAYA MAMBO

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Hapa pia Kiranga umeongea uongo! Miye nakusoma sana kwenye threads tofauti kwa miaka.
Nadhani umesahau pia kuwa uliwahi kusema kuwa, JPM alisababisha familia yako wakawa wanakosa kodi ya pango Oysterbay kwenye nyumba yenu kwasababu ya sera zake! Ulionyesha kuwa hii pamoja na mengine, imechangia sana wewe kumchukia JPM. Halafu hapa unasema ulimpenda kwasababu aliwapa nyumba hahaha, basi tufanye ngoma droo! Kuwa fair brother, ona mazuri pia na mshukuru mungu.

It is a matter of economic fact kwamba JPM aliangusha real estate market. Hilo si suala la chuki binafsi. Ni ukweli wa mambo. Na wala sijasema namchukia JPM kwa sababu hiyo.

Kusema JPM kaangusha uchumi wa real estate Tanzania si kusema kwamba namchukia JPM katukosesha kodi, that is a logical non sequitur.

After all familia yangu haitegemei nyumba ya Oysterbay na tunaweza kuishi vizuri bila kupangisha nyumba ile zaidi ya mwaka. Tuna nyumba nyingi ndani na nje ya nchi kwenye biashara ya real estate so that is not an issue.

You are trying to railroad me in a way that is irrelevant.
 
Ndiyo maana watu wanashangaa juhudi za makusudi za kumchafua marehemu badala ya kuweka energy hiyo kutatua matatizo yaliyopo na kupanga mipango ya baadae.

JPM alifanya yake, maisha na urais wake ni somo, kuna wanaomuunga mkono kwasababu tu aliwapa ujasiri, kuwatia moyo, uthubutu, ari na ile tu feeling kuwa inawezekana. Kauli kama sisi si masikini, au tunafanya bla blah kwa pesa ya ndani, zilikuwa designed kutia watu moyo. Unatakiwa utoke nje ya hilo boksi lako kuelewa kwanini wananchi wengi wa kawaida walimkubali sana na bado wanamkubali JPM.
Hayo ni mambo ya dini sasa, ambayo mimi sikubaliani nayo.

Unawajaza watu ujinga kwamba tunafanya miradi kwa pesa zetu, kumbe umekopa mpaka kope.
 
Ni maneno yako, ulisema mwenyewe hapa JF kuwa alifanya kodi ikaporomoka au kukosa kabisa wapangaji.

Mfano, miye binafsi pamoja na mengine, nilimpenda sana JPM kwasababu ya hiyo hiyo real estate industry, aliifanya ikarudi kwenye uhalisia kwani ilikuwa kama bubble flani hivi unrealistic. Kwangu mimi kipindi cha Magufuli Kilikuwa ni kipindi cha kununua na kuwekeza kwenye real estate! Kwahiyo majanga yako, yalikuwa fursa kwangu na wengine waliyoona kile nilichoona!

Am not railroading you or anything, I think you are a good sports and a formidable debater. Don’t take anything personal!
My point ni kwamba sina sababu ya kumchukia JPM personally.

Tatizo letu ni kwamba, watu wakitajirika, tunafikiria ni vipi tutawashusha wawe masikini, badala ya kufikiri ni vipi na sisi masikini tutakuwa matajiri kama wao.

Hii mentality ya kulogana kwa sababu mtu kajenga nyumba nzuri ipo sana Tanzania.

Na hii ni mentality ambayo Magufuli aliitumia sana.

Na ikamfanya apendwe na Watanzania wengi.

Kwa sababu Watanzania wengi wana fikra za kimasikini kama Magufuli.

Fikra za "tukose wote".
 
L

Najua pia si shabiki wa dini, niliweka hiyo ku-prove hiyo response hahaha.
Anyways, miye baba yangu akikopa ili nipate mahari ya kuoa, sitapenda kama akiniambia hilo au kutangaza kwa majirani. Ni bora tu iwe siri yake, as long as ana plan nzuri ya kulipa deni.
Unapenda uongo mtamu kuliko ukweli mchungu[emoji1787][emoji1787][emoji1787].

Kama unajua au hujui, wewe ni shabiki wa dini.
 
Back
Top Bottom