Nimechagua kumchukia Zitto Kabwe kutokana na kuwa na chuki na Hayati Magufuli

Nimechagua kumchukia Zitto Kabwe kutokana na kuwa na chuki na Hayati Magufuli

Ndiyo maana watu wanashangaa juhudi za makusudi za kumchafua marehemu badala ya kuweka energy hiyo kutatua matatizo yaliyopo na kupanga mipango ya baadae.

JPM alifanya yake, maisha na urais wake ni somo, kuna wanaomuunga mkono kwasababu tu aliwapa ujasiri, kuwatia moyo, uthubutu, ari na ile tu feeling kuwa inawezekana. Kauli kama sisi si masikini, au tunafanya bla blah kwa pesa ya ndani, zilikuwa designed kutia watu moyo. Unatakiwa utoke nje ya hilo boksi lako kuelewa kwanini wananchi wengi wa kawaida walimkubali sana na bado wanamkubali JPM.
Nadhani Ndio maana watu wametoka nje ya box na kujadili hiyo mikopo yake ambayo tunatakiwa kuilipa?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Nakubaliana na wewe labda, lakini ishu ni kwanini ulisema JPM aliipa familia yako nyumba? Lengo lilikuwa nini?
Kuna watu wamezoea siasa za maji taka na chuki binafsi.

Siasa za kulambana viatu kwa kuwa umepewa hiki au kile. Au unataka hiki au kile.

Siasa za chuki kwa sababu hujapewa hiki au kile.

Siasa za makundi na makabila.

Wakawa wananiweka huko.

Nikawaambia kwamba, huko sipo.

Kama ningekuwa mtu wa kufuata siasa hizo, mimi ningekuwa supporter mkubwa wa JPM.

Kwa sababu ni Msukuma kama mimi, halafu alikuwa mtu ambaye anapiga story regularly na mshua wangu tangu wakati bado JPM waziri, kwa hivyo JPM alikuwa mshua fulani yupo kwenye family network nikikutana naye namwambia mimi mtoto wa fulani anamjua baba yangu kipindi kirefu tu, pia, amefanikisha familia yangu kupewa nyumba Oysterbay.

Kuna mambo ya ndani sana JPM alikuwa frustrated kwenye serikali ya Mkapa alikuwa hawezi kusema kwenye vikao, lakini alikuwa akiongea na baba yangu anafunguka. Ndiyo maana nikasema kwamba, JPM angekuwa na amri hata uuzaji wa mashirika ya umma na nyumba za Oysterbay usingefanyika. Kwa sababu haya ni maongezi ambayo mimi nayajua JPM alishafanya na baba yangu, wote wakiwa wanapinga uuzwaji wa mashirika ya umma ulivyofanyika, wakati huo JPM akiwa waziri.

Kwa hiyo, kama hapa JF ningekuwa mtu wa kutokuangalia philosophical positions, ningekuwa mtu wa kuangalia JPM kanifaidishaje mimi na familia yangu tu, ukabila na urafiki, ningekuwa team praise, nisingemsema vibaya JPM.

Ningemtetea kufa na kupona kama "Mnamhala". Godfather fulani hivi Don Vito Corleone.

Lakini, kwa kuwa mimi si mtu wa kuangalia chuki binafsi wala mahaba binafsi, naangalia philosophical positions tu, naweza kumsema vibaya au kumsifia JPM, kwa hoja, bila kujali kwamba alikuwa na ukaribu na baba yangu, au ni Msukuma kama mimi, au aliipa familia yangu nyumba Oysterbay na kutujengea daraja la Tanzanite juu.

Naangalia principles tu, philosophically.

Sipo kwenye chuki wala mahaba kwa mtu binafsi.
 
Ni Imani yangu mkuu kwake najua hatarudi Tena ila anaishi moyoni Mwangu.... Karibu Umoja party
Wazazi wako hawamo moyoni mwako na hata umtumbukize vipi moyoni mwako hatarudi kamwe unapoteza muda wako bure hatarudi.
Nchi za dunia ya kwanza wote wale waliozifikisha nchi zao hapo zilipo hakuna anayesema "zidumu fikra zake", alifariki na waliobaki wanaendelea na yao.
 
Watetezi wa legasi mpumzike sasa
 
Kuna watu wamezoea siasa za maji taka na chuki binafsi.

Siasa za kulambana viatu kwa kuwa umepewa hiki au kile. Au unataka hiki au kile.

Siasa za chuki kwa sababu hujapewa hiki au kile.

Siasa za makundi na makabila.

Wakawa wananiweka huko.

Nikawaambia kwamba, huko sipo.

Kama ningekuwa mtu wa kufuata siasa hizo, mimi ningekuwa supporter mkubwa wa JPM.

Kwa sababu ni Msukuma kama mimi, halafu alikuwa mtu ambaye anapiga story regularly na mshua wangu tangu wakati bado JPM waziri, kwa hivyo JPM alikuwa mshua fulani yupo kwenye family network nikikutana naye namwambia mimi mtoto wa fulani anamjua baba yangu kipindi kirefu tu, pia, amefanikisha familia yangu kupewa nyumba Oysterbay.

Kuna mambo ya ndani sana JPM alikuwa frustrated kwenye serikali ya Mkapa alikuwa hawezi kusema kwenye vikao, lakini alikuwa akiongea na baba yangu anafunguka. Ndiyo maana nikasema kwamba, JPM angekuwa na amri hata uuzaji wa mashirika ya umma na nyumba za Oysterbay usingefanyika. Kwa sababu haya ni maongezi ambayo mimi nayajua JPM alishafanya na baba yangu, wote wakiwa wanapinga uuzwaji wa mashirika ya umma ulivyofanyika, wakati huo JPM akiwa waziri.

Kwa hiyo, kama hapa JF ningekuwa mtu wa kutokuangalia philosophical positions, ningekuwa mtu wa kuangalia JPM kanifaidishaje mimi na familia yangu tu, ukabila na urafiki, ningekuwa team praise, nisingemsema vibaya JPM.

Ningemtetea kufa na kupina kama "Mnamhala". Godfather fulani hivi Don Vito Corleone.

Lakini, kwa kuwa mimi si mtu wa kuangalia chuki binafsi wala mahaba binafsi, naangalia philosophical positions tu, naweza kumsema vibaya au kumsifia JPM, kwa hoja, bila kujali kwamba alikuwa na ukaribu na baba yangu, au ni Msukuma kama mimi, au aliipa familia yangu nyumba Oysterbay na kutujengea daraja la Tanzanite juu.

Naangalia principles tu, philosophically.

Sipo kwenye chuki wala mahaba kwa mtu binafsi.
Mkuu K, Umeandika Vyema Sana. Kama zito alikuwa anataka Kuzungumzia Mikopo Yote Kwa Nini Spika Ndugai alivyotoka hadharani na Kukemea Mikopo Wakati Bunge Lilipitisha Tozo, Kwa Nini Zito hakuwahi Kuzungumzia Mikopo ya Hangaya inayokopwa Kila Kukicha Yeye Yuko Busy na Mikopo Ya JPM Pekee?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Nimejaribu kukuelewa, lakini maneno yako na historia ya michango yako haisapoti ulichoandika hapo juu. Katika michango yako mbalimbali kuhusu hayati JPM unaji-contradict sana. Nitaishia hapo

Kwa nyongeza tu, wewe unaona ni sahihi Mkapa alivyowapa ninyi na wengine nyumba za serikali? Kwa kipindi kile, unadhani ilikuwa sahihi kuuza makampuni ya umma na kuua TiPPER?? Unadhani JPM alikuwa sahihi kupinga au Walau kuwa frustrated kwa hayo maamuzi?
Nimeandika hapo juu kwamba moja ya maongezi ya JPM na baba yangu yalikuwa ni kupinga uuzwaji holela wa mashirika ya umma. Na mimi nipo katika msimamo huo, moja ya mambo niliyokubaliana na JPM.

Kimsingi uuzwaji wa mashirika ya umma, hata kwa kufuata ilani ya CCM, ulitakiwa kufanywa kwenye mashirika yaliyoshindwa kujiendesha kwa faida.

Mkapa akapitiliza kuuza kila kitu. Mpaka mashirika yenye faida. Kwa kufuata kanuni za kwamba serikali ijitoe kuendesha mashirika, soko huria litawale.

Watu wengi hawakuoenda hili, tukiwamo mimi, baba yangu na JPM.Lakini kura hazikutosha kumpinga Mkapa.

Kwa hivyo miminsikufurahia zoezi zima la uuzwajinwa mashirika ya umma, hususan yale yaliyokuwa yanajiendesha kwa faida. Yenye hasara mwaka hata mwaka nilikuwa open yauzwe.

Hizo contradictions unazosema ninqzo inabidi uziweke wazi tuzichambue.

Kwa sababu unaweza kuona contradiction sehemu ambayo hakuna contradiction umeshindwa kuelewa tu, au mimi nimeshindwa kujieleza, au ume rukia conclusion kwamba naelekea kusi wakati naelekea kaskazi.
 
Wazazi wako hawamo moyoni mwako na hata umtumbukize vipi moyoni mwako hatarudi kamwe unapoteza muda wako bure hatarudi.
Nchi za dunia ya kwanza wote wale waliozifikisha nchi zao hapo zilipo hakuna anayesema "zidumu fikra zake", alifariki na waliobaki wanaendelea na yao.
MKuu hoja ya Wazazi wangu imefikaje Hapa?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Wakuu nimekuwa na chuki sana na Huyu zito.
.
Namchukia sana kutoka rohoni mwangu.
.
Amekuwa na chuki sana na JPM kila akipata forum ya Kuzungumza anamzungumza Kwa mabaya JPM.
.
Unakuwaje na chuki na mtu ambae hawezi kukujibu Kwa lolote

View attachment 2215113
Umechagua kumchukia Kama naye alivyo chagua kumchukia Magu! Kila mtu akaye na uchaguzi wake!
 
Kuna kauli za Zitto amechemka, kama ile kauli ya kusema wanaompenda Magufuli wakazikwe naye Chato ni ujinga.

Lakini, kwenye kukopa, hili ni kweli, hata ukisikiliza mazungumzo ya Tido Mhando na rais SSH, rais kalitaja hili.

Kwa hivyo, kwenye hilo Zitto yuko sawa.

Tuache kuongozwa na hisia, twende kwa data.
SSH alikuwa vice na Vice wa SSH alikuwa financial wa serikali ya JPM walikubali vp mikopo hii. Na leo wao ndio tumewapa nchi yetu.

Mikopo mingi JPM alichukua AfDB na tumewaona watawala hawa wa Sasa wakisaini mikataba na Rais wa bank hiyo miezi 2 iliyopita. Kujenga Dom ring road yenyewe imekaaje?. JPM alikuwepo hapo?

JPM alisema yeye si mwanasiasa mzr lkn Sasa naona ndio hatuna wanasiasa wala watawala. Twende tu.
 
Mkuu K, Umeandika Vyema Sana. Kama zito alikuwa anataka Kuzungumzia Mikopo Yote Kwa Nini Spika Ndugai alivyotoka hadharani na Kukemea Mikopo Wakati Bunge Lilipitisha Tozo, Kwa Nini Zito hakuwahi Kuzungumzia Mikopo ya Hangaya inayokopwa Kila Kukicha Yeye Yuko Busy na Mikopo Ya JPM Pekee?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Mimi huwa sipendi sana ku dismiss hoja za watu kwamba zinatokana na chuki binafsi, bias au conspiracy theory.

Kwa sababu haya ni mambo magumu sana kuthibitisha (kwa mfano, unajuaje hii ni bias au chuki binafsi, na si ujinga wa mtu tu?).Pia, kumsingizia mtu mambo haya ni kashfa kubwa sana, ukimsingizia mtu kimakosa unaharibu sana mambo. Sipendi kabisa kumtuhumu mtu kirahisi rahisi.

Lakini, kwa Zitto kuwa na selective criticism akimuandama Magufuli tu, hata pale ambapo labda ni kweli Magufuli alikosea, halafu asimseme kabisaaa rais SSH, hapo anawapa msemo wale wanaosema kwamba Zitto ana chuki binafsi na Magufuli na tofauti zake si za kifalsafa tu.

Mimi kwa kumbukumbu zangu sijawahi kumsikia Zitto akimsema vibaya SSH, wakati SSH ana mapungufu mengi tu naye.
 
Kipindi cha JPM huyu jamaa alikua na hali mbaya sana kisiasa sasa hv ndio anarecover kwa hiyo ana chuki zake binafsi na hajui njia ya kutokea zaidi ya kumdiss Magu
 
Hana akili huyo achana nae.

Anasem miradi ya JPM, hiyo miradi ya Magufuli ni ipi? Ni mali yake binafsi? Iko chato nyumbani kwa Magufuli hiyo Miradi?

Ukweli gani anataka huyo mrundi? Kwani mikopo ni mara ya kwanza nchi hii tumechukua? Mbona haijawahi kua na faida yoyote. Angalau Magufuli alikopa kujenga Bwawa la Nyerere, kujenga SGR nk. Alitaka afanyeje?

Zitto ni mtu asie na akili sio wa kumsikiliza.
Ila dah Jiwe alikuwa Fisadi, muongo na muuaji
 
Wazalendo tulishampuuza. Alishapewa mzinga wake yupo busy kulamba asali. Hana budi kumpondea JPM aliyewabania wapigaji wote.
Mkuu Rais gani alikuwa mpigaji na muuaji zaidi ya Jiwe?
 
Anazungumza na elites au kundi gani ktk jamii?? Mikopo ya jpm inamuumizaje yeye??

Kauli kama hiyo hawezi kuizungumza mbele ya wanazuoni. Anaifanya siasa kama sanaa tu bila kuingiza sayansi ndani yake.
Mjeuri/msaliti tulishamdharau watu wa kanda ya ziwa
 
Wakuu nimekuwa na chuki sana na Huyu zito.
.
Namchukia sana kutoka rohoni mwangu.
.
Amekuwa na chuki sana na JPM kila akipata forum ya Kuzungumza anamzungumza Kwa mabaya JPM.
.
Unakuwaje na chuki na mtu ambae hawezi kukujibu Kwa lolote

View attachment 2215113
Mwacheni awe na chuki hamjui wasiojulikana kipindi cha jpm walimkosakosa mara ngapi
 
Ishu moja kubwa katika kauli zako ni wewe kusema JPM aliwapa nyumba Oysterbay (lakini kumbe ni Mkapa), halafu uliwahi kusema kuwa hukumpenda JPM kwasababu ya kudhoofisha real estate na kufanya nyumba yenu ya Oysterbay (ya serikali) kupungua thamani na labda kukosa kodi. Kimsingi nadhani umeshindwa ku-reconcile hizo issues, mara nyingi unajichanganya….

Mkapa ndiye aliyepitisha uuzwaji wa nyumba.

Kulikuwa na bodi maalum.kwa kazi hiyo.

JPM akapora mchakato wote yeye ndiye akawa ana nguvu sana katika kugawa nyumba, utakumbuka alimpa mpaka hawara yake nyumba na mdogo wake ambaye hakustahili alipata nyumba.

So, my point ni kwamba, mimi ningekuwa katika siasa za wasaka tonge, ningekuwa ni mtu wa kumshukuru sana JPM kwamba kafanikisha sisi kupata nyumba Oysterbay.

There is no contradiction there. Kuna watu tulikuwa tunakaa nao mtaa mmoja Oysterbay mimi nilifikiri zile nyumba zote wamepewa, nikaja kukuta si kweli.

Kuhusu kutompenda JPM kwa kudhoofisha real estate market, labda unipe direct quote, mimi sipo kwenye kumpenda au kumchukia mtu. If anything naweza kuelewa kusema kwamba policies na tactics za JPM zinaangusha real estate market na hilo si jambo zuri kwa uchumi wa nchi.

There is no contradiction there.

JPM alikuwa na policies nyingi tu mbovu, kusema hilo haina maana namchukia JPM.

Unlike some, I can separate the individual from the policies.

Hili ni tatizo kubwa sana la siasa za Afrika.

Watu hawawezi kutenganisha mtu na sera za mtu.

In fact, I will go even further and say most people have a big challenge as far as abstract thinking, critical thinking and logical thinking are concerned.

Ndiyo maana watu wanashindwa kujadili sera, wanajadili watu.

Na ukikosoa sera unaambiwa una chuki na mtu.

Na wengine wanachanganya chuki binafsi na siasa za sera.

I should like to think that I am far above that.
 
Back
Top Bottom