Nakubaliana na wewe labda, lakini ishu ni kwanini ulisema JPM aliipa familia yako nyumba? Lengo lilikuwa nini?
Kuna watu wamezoea siasa za maji taka na chuki binafsi.
Siasa za kulambana viatu kwa kuwa umepewa hiki au kile. Au unataka hiki au kile.
Siasa za chuki kwa sababu hujapewa hiki au kile.
Siasa za makundi na makabila.
Wakawa wananiweka huko.
Nikawaambia kwamba, huko sipo.
Kama ningekuwa mtu wa kufuata siasa hizo, mimi ningekuwa supporter mkubwa wa JPM.
Kwa sababu ni Msukuma kama mimi, halafu alikuwa mtu ambaye anapiga story regularly na mshua wangu tangu wakati bado JPM waziri, kwa hivyo JPM alikuwa mshua fulani yupo kwenye family network nikikutana naye namwambia mimi mtoto wa fulani anamjua baba yangu kipindi kirefu tu, pia, amefanikisha familia yangu kupewa nyumba Oysterbay.
Kuna mambo ya ndani sana JPM alikuwa frustrated kwenye serikali ya Mkapa alikuwa hawezi kusema kwenye vikao, lakini alikuwa akiongea na baba yangu anafunguka. Ndiyo maana nikasema kwamba, JPM angekuwa na amri hata uuzaji wa mashirika ya umma na nyumba za Oysterbay usingefanyika. Kwa sababu haya ni maongezi ambayo mimi nayajua JPM alishafanya na baba yangu, wote wakiwa wanapinga uuzwaji wa mashirika ya umma ulivyofanyika, wakati huo JPM akiwa waziri.
Kwa hiyo, kama hapa JF ningekuwa mtu wa kutokuangalia philosophical positions, ningekuwa mtu wa kuangalia JPM kanifaidishaje mimi na familia yangu tu, ukabila na urafiki, ningekuwa team praise, nisingemsema vibaya JPM.
Ningemtetea kufa na kupona kama "Mnamhala". Godfather fulani hivi Don Vito Corleone.
Lakini, kwa kuwa mimi si mtu wa kuangalia chuki binafsi wala mahaba binafsi, naangalia philosophical positions tu, naweza kumsema vibaya au kumsifia JPM, kwa hoja, bila kujali kwamba alikuwa na ukaribu na baba yangu, au ni Msukuma kama mimi, au aliipa familia yangu nyumba Oysterbay na kutujengea daraja la Tanzanite juu.
Naangalia principles tu, philosophically.
Sipo kwenye chuki wala mahaba kwa mtu binafsi.