Nimechaguliwa kujiunga na AZANIA SECONDARY SCHOOL A-LEVEL 2023 wanaoijua mnisaidie hapa

Nimechaguliwa kujiunga na AZANIA SECONDARY SCHOOL A-LEVEL 2023 wanaoijua mnisaidie hapa

Dogo langu me nimepiga Azaboy O level (Lebo nyeusi), advance nikaenda mkoani shule Fulani ya ufundi. Washkaji wengi tulikataa kuendelea kusoma Azaboy, kwasababu mabraza wetu tulikuwa hatufurahishwi na performance zao.

Kufika mkoani, shule yenyewe mixture ukijumlisha tumetoka uboizini, misheria kibao, mademu wenyewe wabovu tu. Tukaanza ku compare na Ile shule na Azaboy, tukaona Azaboy Kuna potential ya kupiga marks za umaarufu kuliko pale. Tuliofaulia pale wote tulirudi Azaboy.

Dogo langu unachopaswa ukijue, Azaboy Ina walimu wengi uwezo mdogo. Kuna walimu Wametufundisha o level Wana mental issues, unachokiona kwenye matokeo ya necta ni kwasababu wanafunzi wanaopelekwa pale ni "machizi kusoma"
 
Yah kwa kombi yako hyo fosi bweni pale sema cjajua kwa sasa ila kipnd chetu raia walikua wanalala darasn tu na fresh asbh kukikucha godoro linaekwa juu ya dali na magodor yalkua mawili tuu so weng mnaishia kulala kwmy meza huku mnasom
Dah! Mkuu umenikumbusha Maisha ya utravela
 
Dogo langu me nimepiga Azaboy O level (Lebo nyeusi), advance nikaenda mkoani shule Fulani ya ufundi. Washkaji wengi tulikataa kuendelea kusoma Azaboy, kwasababu mabraza wetu tulikuwa hatufurahishwi na performance zao.

Kufika mkoani, shule yenyewe mixture ukijumlisha tumetoka uboizini, misheria kibao, mademu wenyewe wabovu tu. Tukaanza ku compare na Ile shule na Azaboy, tukaona Azaboy Kuna potential ya kupiga marks za umaarufu kuliko pale. Tuliofaulia pale wote tulirudi Azaboy.

Dogo langu unachopaswa ukijue, Azaboy Ina walimu wengi uwezo mdogo. Kuna walimu Wametufundisha o level Wana mental issues, unachokiona kwenye matokeo ya necta ni kwasababu wanafunzi wanaopelekwa pale ni "machizi kusoma"
"machizi kusoma" hapo una maana gani mkuu?

shukurani.
 
"machizi kusoma" hapo una maana gani mkuu?

shukurani.
Ili uende Azaboy Kwa o level,lazima uwe na wastani wa A. Pili assume mwalimu Hana msaada wowote kwako, sijui kichwa chako kipoje, ila Mimi topics karibu zote za PCM nilikuwa nakava mwenyewe.

Enzi zetu kuanzia 4m4 Hadi 4m6 tulikuwa matravela (kulala madarasani au unaenda kugongea Kwa washkaji hostel).

Uzuri mazingira ya kule kila kitu unachohitaji kama mwanafunzi ili ufaulu vizuri kipo. Ni juu Yako na kichwa chako kitakavyokutuma, na ukitaka Bata ndo usiseme
 
Ooh! nimekupata.
 
Nilisoma hapo Azaboy advance ECA 2008-2010,tulikuwa tunakaa pale Hostel pembeni kuna watoto wa Zanaki na nyuma watoto wa Jangwani.

By that time Azaboy ilikuwa zaidi ya chuo kikuu Uhuru kama wote,hakuna Mwalimu anamfatilia mwanafunzi.
Tulikuwa tukiamka ni kwenda Maktaba ya Taifa au Ubalozi wa USA kusoma.
Kula kama una hela unaenda kula pale Muhas na wanafunzi wa chuo.

Jioni mnaenda Don bosco kucheza basketball ball au kwenda kuangalia mchezo wa golf kule Gymkan.

Asubuhi tunakimbia kuzunguka UN road,masaki na kuishia GYMkan beach pale tunaoga tuna rudi kusoma.

Usiku kuanzia SAA 4-7 tunazunguka mnazi mmoja, karikaoo na posta kuangalia Madada poa

Weekend tunaenda casinos za posta na kwenda sinza kwenye club za miziki.
Azaboy ilkuaga bata sn binafsi sikushangaaga niliposikia kuna kipnd iliingia top last[emoji28]
 
Hongera , lakin haujasema je wewe ni mwenyeji wa hapo hapo Dar es salaam au unatokea mkoa na shule ndyo umekuleta jijini ??... Kwanini nimekuuliza

1)kama umetokea mkoa kaaa uelewe Dar es salaam hamna shule ya bweni ya serikali namaanisha shule zote maarufu Dar kama
  • Azania
  • Tambaza
  • kabasila
  • chang'ombe
  • jangwani
  • Benjamini na nyingine nyingine wadau watanisaidia

Siyo shule za bweni , hivyo basi kuna hostel za watu binafsi ambazo huwapangisha wanafunzi kwa gharama fulani , mfano zipo ambazo kwa mwezi ni tsh 20000 mbaka 45000
Hizi za 20000/= moja zina kunguni wengii sanaa hili lazima nisa lakini pia siyo nzuri sana kwa mwanafunzi kujisomea kumbuka kwenye hizi hostel uhuru ni wakutosha unaweza hata usikanyage darasani mwezi mzima na hamna atakae kuuliza hapo msala utakuwa kati ya wewe na walimu wa shuleni kwenu

- kwasababu Azania ni boys sina tatizo ila ingekuwa chang'ombe au kibasila kule hapa ningekushauri ukasome sanaa ufuate kilichokupeleka mimi nimeshuhudia wengi wakipoteza direction kutokana na maisha ya hostel maana huko ni kawaida kukuta jamaa na demu wake wote wanasoma darasa moja wanaishi kama mume na mke . Sasa kivumbi huja wakipigana chini hivyo mwenzangu na mimi kama na wewe ni wakuigaiga kufeli nje nje ..

Yapo mengi lakini machache ni hayo
Azania siku hizi kuna mabweni Chief
 
Kama kichwa cha uzi kinavyosema, mimi nimemaliza form four mwaka jana hivyo form five selections zimetoka na nimechaguliwa kwenda Azania sec

Hivyo najua humu kuna watu wanaishi hapo karibu au wamesomea pale naomba mnipe hali ya maisha ya pale, ufaulu wake, n.k

Natokea mikoani na itakuwa mara yangu ya kwanza kuishi Dar

Combination nimechaguliwa kusoma PCM

Natanguliza shukurani
Karibuni wajibu

Funny boe
Nakupongeza kwa hilo, Azania ni Day School , je umeshajianda ki-saikolojia kukimbizana na masomo huku ukiwa Day tena kwa jiji kama la Dsm? Na wewe umechaguliwa kusoma PCM?

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
 
Wakongwe tuliopambana Advanced Physics, Chemistry, Biology, Pure Math tunakuzoom tu hata utanie au usitanie..

Tafuta nyuzi zinazohusu Advanced Physics humu uone shuhuda za watu jinsi walivyohenyeshwa na Phyz
[emoji1][emoji1][emoji1], hatari na nusu..mnyama Phy!

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
 
Azaboi ya sasa sio kama ya Zamani shule nyingi za Dar A_level siku hizi ni za kawaida sana inahitaji msuli kazi haswa kwa wewe PCM ukiyumba kidogo tayari ushapotea.
 
Chai ,bweni za kimchongo mfano Azania haichukui wanafunzi wote kuna kundi kubwa wanaishi nje ,Tambaza hostel kwa girls pekee.
Duuuh hatari mbna, hata sikuwa najua, nkawa najua kwa advance bweni wote.
 
Back
Top Bottom