Nimechoka kupokea wageni


Ukiona hivyo, basi ktk ndugu wako na mkeo, ww ndio una maisha mazuri walau... Ila nashangaa kwanini unalalamika hivyo, mwanaume jitume tu bana, waje wale, walale, wapatie na nauli kidogo na matumizi wakiondoka sio mbaya.
 
Nunua gunia la mahindi na maharage weka ndani,

Nunua magogo magumu weka hapo nje na shoka kali

Wakija wapasue kuni halafu ni ugali maharage kila siku, wataondoka wenyewe
Hi ni kiboko haswa😂😂😂
 
Kuna wengine watakunafkia hapa kujifanya wema sana ila kiukhalisia kwenye familia zao hata mgeni hakanyagi..!!

Ishi kulingana na budget iliyo ndani ya uwezo wako usitumie nguvu kubwa sana kuwafurahisha watu huku unateseka (mshumaa),

Habari mbaya ni kuwa at the end of the day baada ya kuwa hu-save wala kufanya maendeleo yoyote wewe ndiye utaonekana looser, hakuna mtu atakumbuka kile uli sacrifice kwa ajili yao..!! Shauri yako..!!

Mac Alpho
 
Aseee hii tabia iliwahi kumtokea mdogo wangu. Dogo ni mfanyakazi na anapenda sana kulima, alinunua mashamba makubwa, hivyo alivyoona wanazidi akaanzisha utaratibu wa kulima, wakija anawaacha kama siku mbili baada ya hapo asubuhi anawaamsha kwenda shamba. Alooo! Kundi la kwanza lililokutana na Hali hiyo ya shamba walienda kuwataarifu wenzao, mpaka Leo ndugu huwa hawaji kwa Dogo bila sababu maalumu.
 
kama una mbwa fungulia
 
Mkeo Ni Msambaa tu
 
Unaweza ukawa hauko hv unavyotusimulia hpa lkn watu wa hv wapo
 
Mitazamo tofauti mi naona ni baraka kama mwanaume basi pambana na ishi ndani ya bajeti yako...Kila kitu kina baraka zake kama huamini katika kukirimu mgeni badi watimue ..
 
Mke wako alipaswa aolewe na mtu kama mchungaji kidogo wangeendana, mambo ya wageni kila saaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…