Nimechoka kupokea wageni

Daah hii Kalii aisee[emoji28]
 
Hiyo ya kuokoka tu lzm watu wapoteane! 😂
 
Mtoa Uzi utakuwa mchaga sio Kwa roho mbaya hivo,,, wachaga ndo wenye roho ya kwanini na uchoyo plus ukabila na hawataki kabisa ndugu wa mwenza wake waje
 
nikikumbuka maisha yetu kabla ya mzee wangu kupoteza mali zake na namna baadhi ya jamaa zetu walivyotunyanyasa ingawa kuna wengine walituonyesha upendo mpaka kuja kusimama wenyewe. sasa ni miaka 17 nyumba yangu haikauki wageni na nashukuru Allah (t.w) riziki inapatikana na milango ya neema imefunguka.
 
Ni kweli kabisa wageni ni baraka. Lkn pia wanasema wema nao usizidi uwezo. Katika maisha tamaduni na malezi pia vinachangia. Kwa tamaduni na malezi ya jamii yetu huwezi kwenda kwenye mji alioolea dada yako au hata kaka yako kama huna sababu ya msingi.

Nakumbuka hata bibi yetu watoto zake walipooa na kuolewa anakwambia siwezi kwenda kwa wakwe zangu. Akienda basi labda kusalimia jioni anageuza,,,au kabda asikie wanaumwa.

Kuja wageni waje lkn unakuta wengine wanakimbia kusaidia kazi huko kwenye familia wanakuja mjini kukaaa tu.
Maisha ya sasa hivi ni kupambana na sio kwenda kukaaa tu kwa ndugu bila sababu za msingi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukishakuwa na familia, nunua vitu vya jumla. Mambo ya kununua unga kilo moja moja,wageni utawaona tu kero.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…