Nimechoka kupokea wageni

Nimechoka kupokea wageni

Ishi kutokana na Bajeti na Utaratibu uliojiwekea.

Ndio maana wazee wetu walikuwa na Miradi kama Mashamba, Mifugo, Bustani nk. Ilikuwa ndugu wakifika kwake basi baada ya siku mbili tu, anawageuza wafanyakazi wa miradi yake. Na kutokana na Uvivu wengi waliondoka mapema sana na taarifa wakapeana.

Be a Man, Stay Taliban.
Daah hii Kalii aisee[emoji28]
 
Hakikisha hapo kwako kuna kazi za kutosha kama kuosha mabanda ya mifugo,kukata nyasi za mifugo,tafuta mashamba huko nje ya mji uwe unawapeleka kulima na kupanda

Okoka na muwe mnasali karibia masaa mawili kabla ya kwenda kulala iwe kila siku na lazima kila mtu awepo wakati wa kusali hata kama ni mgonjwa,tv weka chumban kwako,sebuleni liwepo sabufa la kupiga nyimbo za injili tu

Ukishindwa kabisa hayo yote,anza kuwala ndugu za mkeo kwa siri,ili ufaidi chakula chako

Fanya yote hayo afu unipe mrejesho
Hiyo ya kuokoka tu lzm watu wapoteane! 😂
 
nikikumbuka maisha yetu kabla ya mzee wangu kupoteza mali zake na namna baadhi ya jamaa zetu walivyotunyanyasa ingawa kuna wengine walituonyesha upendo mpaka kuja kusimama wenyewe. sasa ni miaka 17 nyumba yangu haikauki wageni na nashukuru Allah (t.w) riziki inapatikana na milango ya neema imefunguka.
 
Ni kweli kabisa wageni ni baraka. Lkn pia wanasema wema nao usizidi uwezo. Katika maisha tamaduni na malezi pia vinachangia. Kwa tamaduni na malezi ya jamii yetu huwezi kwenda kwenye mji alioolea dada yako au hata kaka yako kama huna sababu ya msingi.

Nakumbuka hata bibi yetu watoto zake walipooa na kuolewa anakwambia siwezi kwenda kwa wakwe zangu. Akienda basi labda kusalimia jioni anageuza,,,au kabda asikie wanaumwa.

Kuja wageni waje lkn unakuta wengine wanakimbia kusaidia kazi huko kwenye familia wanakuja mjini kukaaa tu.
Maisha ya sasa hivi ni kupambana na sio kwenda kukaaa tu kwa ndugu bila sababu za msingi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukishakuwa na familia, nunua vitu vya jumla. Mambo ya kununua unga kilo moja moja,wageni utawaona tu kero.
 
Back
Top Bottom