Nimechoka kupokea wageni

Nimechoka kupokea wageni

Inawezekana umenzisha uzi wa kufurahisha kijiwe, lakini hili ni tatizo lililopo hasa uswazi. Nilikuwa nasikia haya kutoka kwa watu lakini likaja kunikuta. Na kama halijakukuta unaweza kudhani ni rahisi sana kulitatua kumbe hapana.... hasa kama una mke mwenye kichwa fyongo.
Ugomvi hauta isha
 
Shemeji tunakuja wiki ijayo tutarudi nyumbani mwezi wa 7 wewe jiandae na hatutaki madagaa na maugali ya kila siku.

Ahaaaaaa sijui nimecheka nini ila kwetu ndugu wa mwanamke hawazululi kwa mkwe , akienda ni kwa nadra sana.

Mleta mada mke wake ni msukuma familiya nzima wanahamia kwa mkwe ila ndo upendo wenyewe.
 
Hellow Africa

Dah ninaishi na wife huu mwaka wa nne sasa ila kero kubwa wageni hawakauki hapa nyumbani ndugu zake wanaingia na kutoka kiasi kwamba mtu huwezi kuweka akiba yako.

Juzi kaja mgonjwa wa vidonda vya tumbo Jumapili huwa tuna kawaida ya kupika pilau yeye tukampikia ndizi lakini wapi eti kaenda kugombania ukoko wa pilau na mwanangu wa mwisho mpaka kaja kuniambia chumbani.
Nchi ngumu Sana hii
 
Kuna wengine watakunafkia hapa kujifanya wema sana ila kiukhalisia kwenye familia zao hata mgeni hakanyagi..!!

Ishi kulingana na budget iliyo ndani ya uwezo wako usitumie nguvu kubwa sana kuwafurahisha watu huku unateseka (mshumaa),

Habari mbaya ni kuwa at the end of the day baada ya kuwa hu-save wala kufanya maendeleo yoyote wewe ndiye utaonekana looser, hakuna mtu atakumbuka kile uli sacrifice kwa ajili yao..!! Shauri yako..!!

Mac Alpho
You stole my words.
How could you? See you in court 🙂
 
we jamaa bana., perheps tuna perspective tofauti lakini , ndugu ni baraka. Pengine Lizki yao ipo kwako. the moment wanakata nayo inakata.... wafurahie tu.
 
Shida n kwamba unakaaa mwanza unao na shughuli zako zipo shinyanga nauli shy-mwanza afu 7 lazima waje kugombania ukoko Olea mbali unaolea songea unakaa shinyanga nauli tu elfu 80k nani aje akiwa anakuj ajipange kwa nauli utapunguza hizo kero

Mbili lazima uwe na voice of command anakuj mdog wangu kunisalimia no kma umemiss nikupe nauli ukamsalimie

Tatu wew unawez ukawa unapambn familia yako ile vizuri wanawake wanatabia ya kuonyesha kwa ndugu zao kuwa wameolewa mahali safi sometime snaps za misosi zinawek status sas wakij wagenii badili meals ya mlo achan na vitu vizuri kbsaa utakuja kuniambiaaa
 
we jamaa bana., perheps tuna perspective tofauti lakini , ndugu ni baraka. Pengine Lizki yao ipo kwako. the moment wanakata nayo inakata.... wafurahie tu.
Wew wasema ikukute usichukulie pw pesa akun siku iz
 
Nataman niwanywee pombe
Ha haa umenikumbusha kaka (cousin) yangu mmoja aliwafanyia hivyo shemegi zake.

Yeye alikuwa ni mpiga maji mzuri sasa kila siku akirudi nyumbani kumejaa wageni mashemegi. Matokeo watoto wanalala ukumbini na mashemegi wanajitanafasi chumba cha watoto. Nyumba zenyewe za Dar vyumba viwili.

Siku moja aliamua kwenda kuuchapa vizuri na alipofika nyumbani mlangoni alianza kuwashambulia kwa maneno makali, kwa nini hawakai makwao kwa waume zao au wazee wao wanakuja pale kumjazia nyumba. Wale mashemegi walichukia sana na siku ya pili walifunga virago kurudi makwao.

Mke wake pia alijifanya kuchukia lakini alimwambia kama unaona mimi nimekosea na wewe funga virago uelekee kwenu, ikabidi mama anyamaze tu. Basi tokea siku hizo nyumba ile walikuwa wakiipisha kwa mbali sana.

Hii alinihadithia mwenyewe nikamuuliza kama alijisikia vibaya kwa kuwatimua mashemegi kivile. Aliniambia nilikuwa sina jinsi bajeti ilikuwa haitoshi tena ikabidi nijitoe akili ili mambo yangu yaende.
 
Hellow Africa

Dah ninaishi na wife huu mwaka wa nne sasa ila kero kubwa wageni hawakauki hapa nyumbani ndugu zake wanaingia na kutoka kiasi kwamba mtu huwezi kuweka akiba yako.

Juzi kaja mgonjwa wa vidonda vya tumbo Jumapili huwa tuna kawaida ya kupika pilau yeye tukampikia ndizi lakini wapi eti kaenda kugombania ukoko wa pilau na mwanangu wa mwisho mpaka kaja kuniambia chumbani.
UKweni wapi?
 
Back
Top Bottom