Nimechoka kusindikiza wenzangu kwenye madini

Utarudi kawaida au utafanya namna?
 
Kwa mtu mwenye mtaji wa milion 60 unamshauri kwa uzoefu wako awekeze sehemu ipi kwenye sekta ya madini?
Swali Zuri. Kwa uzoefu wangu kama ni upande wa huku Chunya.
1. Bora upambane upate eneo lenye mwamba mkubwa usiopungua Mita 1 ukubwa wake hata likianzia kusoma PPm 3 kwenye Mita 4,5 kwenda chini. Hakikisha pambania hilo eneo kama lina leseni kubwa za Shanta,halafu linamikiwa kienyeji. Ombea chap Leseni yako kwa jina lako. Yaani unakuwa na Leseni ndogo ndani ya Leseni kubwa. Yule mwenyeji utamalizana nae tu kabla ya kuanza kazi. Muhimu katia Leseni yako baada kujua pana mwamba na unasoma hivyo. Uzuri wa kufanya kazi sehemu yako ni kuepuka kumfanyia kazi mtu unaingia gharama kubwa lakini mawe anachukua 30% akiwa amekaa tu hajui gharama. (Hilo ni sehemu ya hasara).
MUHIMU. Wakati wa kuchukua sampling ya kwenda kupima maabara ikiwezekana simamimia huo uchimbaji kwa karibu sana au chukua wachimbaji wageni kabisa wa eneo hili HAPA NDIO WENGI TUMEPIGWA. UKICHUKUA WENYEJI WA ENEO HILO WATAKUNYUNYIZIA SAMPLE SAMPLE ZENYE DHAHABU UNGA UNAOENDA KUPIMA ILI IKAKUCHANGANYE PPM KWENYE VIPIMO. KUMBE UHALISIA SIO HUO.

2. Wekeza kwenye kuchimba,huku ukiwa umefunga kalasha lako. Jitahidi funga kalasha sehemu iliyopita umeme. Funga la kutumia umeme sio mafuta.

3. Simamia mwenyewe kwa karibu. Kila sehemu fuatilia kwa karibu kuanzia uchimbaji na kalashani

4. Nenda kupima sample kila baada ya Mita 5 ya urefu wa duara lako.

5. Sehemu ya mwisho ya kuwa makini ni Elution.
 
Umenena vyema mkuu,
 
Hiyo 40 sidhani kama alikua nayo cash, nadhani ile kidogokidogo kwa kipindi chote alichokaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…