Nimechoka kusindikiza wenzangu kwenye madini

Nimechoka kusindikiza wenzangu kwenye madini

Huko kama huna nyota na hio ishu kutoboa ngumu bila ushirikina na hata ukiwa na hio nyota inabidi kujilinda watu wakikusoma wanaweza wakakuvuruga waipate wao hio nyota mgodi uteme ndo maana kwa wachimbaji wadogo ndumba nje nje maana kuna wenye nyota inabidi wajilinde na kuna wale ambao hawana lazima watoe kafara mambo yaende, huko kunahitaji maamuzi magumu
 
Million 40 kwa biashara nyingine ni mtaji mkubwa sana na una uhakika wa hela kila siku

Ukiona unatumia uchawi kwenye biashara tambua unalazamisha kuwa hio sehemu sio sehemu yako
Hio ni kweli ,nyota yako kama inaendana na hio shughuli mambo yanajipa labda kama umechezewa, ila kama huna nyota ya hio shughuli kutoboa lazima uibe nyota za wengine, wanasema kafara ila ndo unakua unaiba nyota ya mwingine, we unaenda kwa mganga unatoa kafara yeye anakupa nyota ya mtu ambae keshamvuruga huko au kamuua kabisa
 
Mkuu,
Kama karasha unalo na mtaji upo nakusihi tafuta wenyeji wakupe ramani uanze kuchimba duara lako,au kama utashindwa kuchimbisha anza kununua mawe.

Ukiona huna uenyeji wa kutathimini mawe nakushauri anza kwa kununua fero mali ambayo inaweza kua inarudisha hata robo3 ya gharama na iwe inasoma ppm kuanzia 2.0.

Achana na utalaamu wa kwenye madaftari mkuu, ukija uku kwenye uhalisia kuna vitu tofauti kabisa.
 
Naomba uchukue ushauri huu Mkuu ambao na Baadhi wamekushauri hapo juu....

Sekta ya uchimbaji wa madini ni 'illusion' imezungukwa na kiini macho na ushirikina Mkubwa Sana Tena Sana.. ninapokwambia hivi ni experience from the field sio kuandika tu hapa JF.

Kama huamini kwenye kupata madini kwa ushirikina I can assure you wewe sio mchimbaji. Bila mganga Tena mganga mzuri hutoboi utafirisika na kua chizi. It's either ubadili kazi au ufate ushauri.

Hao ambao Mdau mmoja amezungumza hapo juu kwamba wazungu wanatumia teknolojia sijui Nini Nini, nakuhakikishia wao ni washirikina namba moja. Kumbuka tumeijua Freemason kupitia Sheikh Yahaya na hakuonesha imeanzia Tanzania , Bali imeanzia ulaya. So connect dots.

Wachina, Wahindi wote Wana tamaduni zao ambazo zinaashiria shiriki. Sema kwa huku kwetu inaonekana Uchawi. Kila duka la muhindi ametundika majani mlangoni lla wabongo tunasifia tu MO tajiri hujui Nini nyuma ya pazia ibada zao ni zipi.

So huo ndio ushauri wangu.. Ila Kumbuka...

GOD IS EVERYTHING
GOD IS ABLE
GOD IS ABOVE ALL
BELIEVE IN GOD
Acha kutengeneza njia za kutapeli watu. Freemason sisi tunaifahamu miaka mingi ago. Ungekuwa ushirikina ndo unawalipa hao wazungu wangekuwa hawana haja ya kununua vifaa ghali wanavyotumia ku detect yalipo madini. Wewe ni tapeli unataka kumtapeli jamaa.
 
Wanajamvi

Leo nimekuja, mwenzenu yamenifika shingoni

Nina miaka mitatu tangu nimeingi kwenye uchimbaji wa madini huku chunya mbeya,

Nimamiliki karasha, nimeshapoteza zaidi ya milioni 40 katika shughuli hii.

Huwa nnajitahidi kupima miamba kila hatua kama inavyoshauriwa lkn matokeo mara zote huwa kinyume na matarajio,

Mfano unaweza kupima mwamba ukaambiwa ni wastani wa ppm 8 lkn unachokuja kukipata ni wastani wa ppm 1

Wadau wengi hawataki kutoa siri ya wapi wanapitia ili kuhakikisha kile wanachotakiwa kukipata wanakipata,

Tafadhali sana, mwenye kujua namna nnaweza kupata msaada wa kweli tafadhali msaada hapo PM
Mkuu mimi niliwahi kuingia huko nikapigwq 50 million iliniumaa sana hapo iringa sadani
Sasa ikaniuma nikapiga hesabu narudishaje mzigo wangu nikajuaga wachimbaje wanatafuta sana zile gold detector kumbe.... nikaagiza china pc 100 ...moja nilinunua laki tano nikawa nauza million moja na laki mbili faida laki saba ....

Aseee niliuza zikaisha baada miezi minne nikawa na kama million 40 ....zingine zilibaki....nikaachana na hiyo biashara😄😄😄

Dhahabu ni biashara ya utalaam wa hali ya juu...... ila bahati pia ....hakuna uchawi huko utapigwa

Waliofanikiwa huko wamekaa muda mrefu na uvumilivu hiyo biashara fanya huku una biashara nyingine sio ya kutegemea kulisha familia itakuua presha
 
Mkuu mimi niliwahi kuingia huko nikapigwq 50 million iliniumaa sana hapo iringa sadani
Sasa ikaniuma nikapiga hesabu narudishaje mzigo wangu nikajuaga wachimbaje wanatafuta sana zile gold detector kumbe.... nikaagiza china pc 100 ...moja nilinunua laki tano nikawa nauza million moja na laki mbili faida laki saba ....

Aseee niliuza zikaisha baada miezi minne nikawa na kama million 40 ....zingine zilibaki....nikaachana na hiyo biashara[emoji1][emoji1][emoji1]

Dhahabu ni biashara ya utalaam wa hali ya juu...... ila bahati pia ....hakuna uchawi huko utapigwa

Waliofanikiwa huko wamekaa muda mrefu na uvumilivu hiyo biashara fanya huku una biashara nyingine sio ya kutegemea kulisha familia itakuua presha
Kuna namna umetupanga hapa

Sent from my SM-M135FU using JamiiForums mobile app
 
Mkuu,
Kama karasha unalo na mtaji upo nakusihi tafuta wenyeji wakupe ramani uanze kuchimba duara lako,au kama utashindwa kuchimbisha anza kununua mawe.

Ukiona huna uenyeji wa kutathimini mawe nakushauri anza kwa kununua fero mali ambayo inaweza kua inarudisha hata robo3 ya gharama na iwe inasoma ppm kuanzia 2.0.

Achana na utalaamu wa kwenye madaftari mkuu, ukija uku kwenye uhalisia kuna vitu tofauti kabisa.
Sio rahisi kama unavyovikiri mkuu,

Sent from my SM-M135FU using JamiiForums mobile app
 
Vidono muhimu si umeona umefika Ujiji kitu kimejipa umepanda cheo. Fanya haraka unioe kipenzi tuwe tunawanga pamoja

Hii umeongea kiutani ila imenipa hisia kali sana!! Kuna watu tunawaona mijini wanatamba ila siri ya wayafanyayo wanayo wawili tu (mke na mume), ndiyo raha ya kufanana.

Haya, sie tumeoana mie kwa waganga we mlokole!! Vitagongana tu, hamtoboi kamwe!!

Aminia kipenzi!! Tutawanga kinoma ila kama hatupati utajiri wa kufikia kununua Boeing "zetu" private kuloga sitaki!!!
 
Fckn bulshit... Is there any point out there I convinced a guy to follow my suit? Or I advised him to contact me in anyways, fck off... Think before reacting... I spoke my mind the truth of what I know and I encountered in my struggling safari way back. Acha upumbavu!

You have panicked. Just because i have alerted the guy to be careful. Now i see i was right. You are just a fucken scammer and you aint gonna get nothing coz i have just exposed you. Now go get some milk to calm yourself down. 😁
 
Sio rahisi kama unavyovikiri mkuu,

Sent from my SM-M135FU using JamiiForums mobile app
Siyo navyofikiri, nakushauri hivo kwa uzoefu me mwenyewe ni mpambanaji mwenzio nipo uku geita napambana na sijawahi kuua kiasi hicho cha fedha.

Na mtaji wangu si zaidi ya milion 30, Siwezi kuacha hii kazi maana siifanyi kwa matarajio makubwa zaidi ya kutafuta faida inayokidhi mahitaji yangu mpk itakapofika bahati yangu(kuhila).

Na apa napoandika nipo elution nategemea kushusha leo na matarajio yng ni gram 500 tu.

Punguza matarajio makubwa mkuu na kila anaekushauri apa usidhani amekaa dukani au ofisini, wengine tupo apo ulipo acha ubishi chukua kinachokufaa kisichokufaa acha.
 
Gram 500 ni ndogo mkuu?

Ukitaraji gram 500 ukapata gram 150 utarudisha gharama?
Hicho ndo kinatukuta wenzio,

Sent from my SM-M135FU using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom