Iko hivi; watumishi walilipwa mshahara wa mwezi uliopita tarehe 22/23 hivyo ilivyofika June 22/23 tayari ni siku 30/31 yaani mwezi.
Hivyo, wako sahihi acheni kuwatoa ufahamu kwa kutumia tarehe zenu.
Iko hivi.
Mshahara uliolipwa 22/23 May ulikuwa mshahara wa May. May yote, kuanzia May 1 mpaka May 31.
Mshahara huo si wa mpaka May 22/23.
Mshahara huo serikali ilikuwa na muda wa kuulipa mpaka mwisho wa mwezi wa May.
Ila serikali iliwahisha kulipa mshahara wa May kwa wiki moja ili kuhakikisha process zote za payroll zinakamilika kabla ya mwisho wa mwezi kufika, ili isi violate standing order ya kulipa mshahara by mwisho wa mwezi
Kwa hiyo, usianze kuhesabu siku 30 baada ya May 22/23 ili kulipwa mshahara wa June.
Serikali ina muda mpaka June 30 kulipa mshahara wa June.
Moja ya matatizo ninayoyaona ni kwamba watu wanahesabu siku 30 kutoka tarehe waliyolipwa mshahara wa May wakitegemea walipwe mshahara wa June katika siku hizo 30.
Standing order ya serikali kuhusu mishahara haijasema mshahara utalipwa ndani ya siku 30 baada ya mshahara wa mwisho kulipwa.
Standing order ya serikali imeweka mwisho wa mwezi kama deadline ya serikali kulipa mshahara.
Deadline hiyo kwa mwezi June haijafika bado, ndiyo kwanza tupo June 25. Serikali inaweza kulipa mshahara June 30 na bado ikawa haijavunja standing order hii.
Kwa kifupi, mshahara unatakiwa kulipwa mwisho wa mwezi, kama mwisho wa mwezi haujafika bado, wafanyakazi hawana haki ya kulalamika mshahara umecheleweshwa.
Angalia standing order ya serikali section ya kulipa mishahara imewekwa hapa post #290.