Nimechukizwa sana kuona Majeshi yetu yanaonesha umahiri wao kwa kubeba kilo 70 za mizigo

Nimechukizwa sana kuona Majeshi yetu yanaonesha umahiri wao kwa kubeba kilo 70 za mizigo

Watapigika vibaya sana hawa. Kama wahuni wa M23 tu wa hapo Congo wanawafyeka, Somalia watawamaliza.
Hahahaha na wauza madafu watahusika.... Lazima washinde...

Chezea jeshi la mama wewe
 
Niseme tu ukweli mimi nipo hapa 44 KJ Mbalizi wanasiasa ndio wanatuangusha sana Askari.Hata ndege vita tulizonazo pale airbase ya kizuka ni aibu
Wanasiasa wana wana tuangusha kila sector kuanzia Elimu, Afya mpaka huko Jeshini.

Kama hakuna siasa safi katika nchi, tutakua tuna laumiana tu ila hakuna sector itakua salama, hakuna
 
Unaona hizi akili finyu sasa?? Marekani alikuwa anapigana na Iraq, wako bara moja?
Sasa hapo kuna ambae tunafanana nae kwa chochote??

Na nimesema hapa Africa maana nje ya Africa ni haiwezekani. Hiyo vita hatuiwezi na haitakaa itokee.
 
Nimechukizwa sana kuona majeshi yetu yanaonesha umahiri wao wa kubeba kilo 70 za mizigo. Nilitegemea ktk zama hizi jeshi liwe linafanya vitu visivyohitaji nguvu bali viwe vinahitaji akili na maarifa zaidi.

Wenzenu huko duniani wanatengeneza supersonic missiles. Silently triggered guns, invisible drones, camouflaged warships, n.k. Ninyi mnahangaika kubeba mizigo??

View attachment 2974562
Mkoloni alituachia mbinu za kuendelea kumtawala mtu mweusi ili akiona hivyo aogope ku demand uhuru. Sasa jeshi letu linaona ndio mbinu za kivita karne hii ya Artificial Intelligence.
 
Jeshi letu ni jeshi Bora duniani likitanguliwa na Nchi Tano tu.Alisikika mmoja wa makamanda wa jeshi Hilo.
Sasa apo inategemea na Factors zilizo tumika, kama ni hizi za kubeba mizigo hata mm nakubali.

Kuna uvumi naskiaga unapita ety Tanzania iko mbele sana kwenye intellegensia, hua nabaki nacheka tu. How nchi ambayo inaweza kukaa na mtuhumiwa hata miaka 3 yuko gerezani, uchunguzi haujakamilika na hata ukikamilika mtuhumiwa anaachiwa.
 
Yaani nimesikitishwa sana na nilicho kiona leo pale uhuru stadium. JESHI MAMBO MENGINE YANGELIBAKI KUWA SIRI ZA JESHI TU. [emoji849][emoji36] Hebu imagine yale ma drone Iran yalivyo tulizwa wenge juzi na jeshi la Israel hebu imagine [emoji18] halafu angalia sisi [emoji23] si bora tufiche mambo mengine aisee.
Wangeimba nyimbo tu ingekua poa.
 
Wenz
Wanataka wanajeshi wakate mishahara yao wakanunue Missiles? If the policy aren't tight, How can JWTZ be good.
Wenzetu wamewekeza kwenye elimu, kisha wamewekeza haswa kwenye jeshi, viwanda n.k, sisi tunaleta masihara masihara tu. Kisha mtu anakuja kuwabeza jwtz eti waache ushamba, sasa wafanye nini na ndio walichonacho, hawawezi kutamba na hizo mig za miaka isiyojua watu.
 
Aaah wapi....
Nikatalie kwa uthibitisho sasa kaka sijaandika kwa ajili ya ubishani naimani hata nchi yako AIR DEFENSE SYSTEM hujui wanatumia ipi na hata fighter hata kugusa walau tairi hujafanya. Nipe uthibitisho na wewe tafuta utaona.
 
Alafu waandishi wa habari walivyo kuwa wanafiki wana andika kabisa eti BALAA LA MAKOMANDO WA JWTZ.
😂😂😂😂 Sasa hapo kuna balaa gani, au kubeba mizigo ya kilo 70 ndiyo balaa lenyewe.

Badala ya kuonyesha vifaa vya kisasa wao wana beba mamizogo ya kuvunja migongo.
Acha unafki bana SAS au hao NAVY SEAL katika pre course ya SF wanafanyaje? Au uingereza na marekani hawana advanced jet fighters na bombers au hizo drones ila kwanini wanini wana SF ambazo katika pre selection course hayo yotee yanafanyika wao wapumbavu sana?
 
Tupunguze ujuaji. Hakuna uvamizi usiohitaji infantry.
Hakuna vita isiyohitaji recon soldiers.
Hakuna vita isiyo na encirclement.

Hayo yote yanategemea nguvu, stamina ya muhusika.
Pale kabeba survivor kit ya mwezi mzima
 
Acha unafki bana SAS au hao NAVY SEAL katika pre course ya SF wanafanyaje? Au uingereza na marekani hawana advanced jet fighters na bombers au hizo drones ila kwanini wanini wana SF ambazo katika pre selection course hayo yotee yanafanyika wao wapumbavu sana?
Hao WAMAREKANI wanaonyesha kubeba mizigo tuu ?!
Si wana onyesha na technologies zao kwenye mambo mengine na vifaa vyao advanced. Hao wameonyesha nini zaidi ya mizigo ?
 
Halafu kuna kitu kimoja hamkijui mockers na haters commandos au hata special forces nyingine kazi yao ni kupambana kwenye unconventional warfare na mission zao ni ngumu hivyo ukakamavu ni prerequisite ya u-commando
 
Back
Top Bottom