Nimedhamiria kuacha Chuo ili nijiajiri

Kigorohe

Senior Member
Joined
May 21, 2019
Posts
160
Reaction score
255
Habari za mida wakuu.

Japo nipewa ushauri wa kuendelea na masomo ili nimalize semester moja iliyobaki lakini kusema kweli roho yangu bado haitaki kwenda kusoma make nimenogewa kwenye ujasiria mali japo sijaanza kuingiza pesa ndefu sana. Lakini natambua ipo siku nitaingiza kiasi kikubwa sana

Na hata baada ya Mhe. Rais kutoa kauli kuwa vyuo vitafunguliwa juni 1, 2020 nilipambana ndani ya wiki moja nikawa nimepata 76,500 kama nauli ya kunirudisha chuoni huko kanda ya kaskazini jana akatokea jamaa mmoja anauza mbuzi 4 kwa Tsh. 60000 nikaamua kujitungua hivyo nikatumia nauli kununua mbuzi.

Mimi rohoni mwangu saivi nafurahi sana nitakapo kuwa mfugaji mkubwa sana na nimeanza kwa mifugo tofauti tofauti kama nguruwe 2, mbuzi 4, na kuku chotara mitetea 5 na jogooo 1.

Kusoma ni utumwa. Overa
 
Motivational speakers wanasemaje?

Binafsi nakuunga mkono, elimu uliyonayo inakutosha na unaweza usiitimie maishani... shuleni unasomeshwa Kinjekitile Ngwale tangu awali hadi Chuo na hakuna sehemu utaitumia maishani.
 
Motivational speakers wanasemaje.?

Binafsi nakuunga mkono, elimu uliyonayo inakutosha na unaweza usiitimie maishani... shuleni unasomeshwa Kinjekitile Ngwale tangu awali hadi Chuo na hakuna sehemu utaitumia maishani.
Mauq atamuambia atafute mke Ili awe na mahusiano mazuri na mkewe (gym/jogging ya pamoja) na watoto wanunuliwe nguo mpya kila wiki atakua bilionea.
 
Nakushauri kama mtu mwenye uzoefu. Tafadhali maliza shule. Nilipokuwa nasoma niliona miaka 4 ni parefu sana. Nimeajiriwa kwa kweli siamini kwamba imepita miaka 14 tangu nimalize chuo. Utakaa mtaani mpaka utachoka.

Najua kwamba sasa unataka ule uhuru wa kuwa nje ya masomo na kujitegemea. Mimi hivyo hivyo nilikuwa naota ni lini nitamaliza chuo niachane na kusikiliza lectures asubuhi hadi jioni. Lakini mwezi 1 tu baada ya kumaliza shule nilijikuta nimechoka na maisha ya mtaani. Hivyo kwa sasa usisikilize sana hisia zako, bado ni za kitoto.

Maliza shule kabisa tena faulu vizuri. La sivyo utakumbuka nafasi hii miaka michache tu ijayo na itakuwa imepita. Bill Gates na wengine waliacha chuo lakini walipohojiwa walikiri kwamba walifanya makosa, pamoja na kwamba ni mabilionea.
 
Kwanza hongera sana kwa uamuzi wako wa busara wa kujiajiri. Ushauri wangu ni kwamba, maliza kwanza masomo ndugu. Huo mrengo uliouchukua wa ujasiriamali ni mzuri sana. Lakini usikatishe masomo. Ukimaliza wewe endelea na ujasiriamali, Mungu atakusaidia utafika mbali.
 
Man, ulikua unasoma kozi gani na mwaka wa ngapi? Una boom? Umewahi fanya biashara yoyote before au kufuga?
Mkopo ninao, biashara nilikuwa nafanya japo ni ndogo ndogo hata pindi nipo chuoni ila hii ya kipindi hichi cha Corona kidogo ndo naona inaleta matunda kwani naendelea kuanzisha vitega uchumi vingine
 
Nakushauri kama mtu mwenye uzoefu. Tafadhali maliza shule. Nilipokuwa nasoma niliona miaka 4 ni parefu sana. Nimeajiriwa kwa kweli siamini kwamba imepita miaka 14 tangu nimalize chuo. Utakaa mtaani mpaka utachoka...
Sawa sawa mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…