Nimedhamiria kuacha Chuo ili nijiajiri

Nimedhamiria kuacha Chuo ili nijiajiri

Mkopo ninao, biashara nilikuwa nafanya japo ni ndogo ndogo hata pindi nipo chuoni ila hii ya kipindi hichi cha Corona kidogo ndo naona inaleta matunda kwani naendelea kuanzisha vitega uchumi vingine

Kama una boom endelea kusaini ulikwapue, semista ya mwisho saini kwapua boom kisha amua kimalizia Chuo au kula winga... hata ukipata hicho cheti kitakugharimu kutembeza bahasha tu.
 
Acha ujinga kijana kamalize kwanza chuo japo haina umuhimu kwa sasa usisome ili kuajiliwa tafuta vitabu na vipindi vya money management soma na uelewe harafu njo mtaan kupambana akili ikiwa imekomaa
 
Ushauri wa bure kabisa. Kama siku za karibuni uliwai kupita hata karibu na motivational speakers, ndugu pliz usiache chuo maana hizo sio akili zako ni akili za hao M.speaker ulio wasikiliza maana wale wanaweza kukupanga ukapangika kweli kweli na huku huna uwezo huo
 
We mtoa mada nakuhurumia sana Kwahiyo kumiliki mbuzi, nguruwe etc
Unaona tayari unayaweza maisha.

hao walio kudanganya uache chuo kawafungulie mashitaka mahakamani maana sio watu wazuri kwako.ukifanya huo ujinga wa kuacha chuo utakuja kujuta maisha yako yote.Nina mengi ya kusema ila naishi hapa.

NB: acha ujinga mkuu
 
Mleta mada umenikubusha mdogo wangu ali acha shule wiki moja kabla ya mtihani wa form four. Nilihangaika sana wapi!! Akafungua bucha. Sasa hivi ni Mwenyekiti wa wanywa gongo kijijini.
Hahahahahahah umwtisha mkuu! But mimi nilikuwa mtu mzima kama niliji control mwenyewe mpaka university afu leo hii nije kunywa gongo labda nirogweeee
 
nakubaliana na wewe, kwa utimamu wako usirud nyuma huko shle amna sehem wanagawa hela ila mtaan ukiweka goli vzur ela znakufata.
 
Watu wanafkir ku make money ni rahisi tu ila wanasahau ku maintain same standard!.

Unaacha shule unaenda kufuga mbuzi na nguruwe alaf una one last semester?[emoji23][emoji23]
 
  • Thanks
Reactions: amu
Back
Top Bottom