Habari za mida wakuu!
Japo nipewa ushauri wa kuendelea na masomo ili nimalize semester moja iliyobaki lakini kusema kweli roho yangu bado haitaki kwenda kusoma make nimenogewa kwenye ujasiria mali japo sijaanza kuingiza pesa ndefu sana. Lakini natambua ipo siku nitaingiza kiasi kikubwa sana.
Na hata baada ya Mh. Rais kutoa kauli kuwa vyuo vitafunguliwa juni 1, 2020 nilipambana ndani ya wiki moja nikawa nimepata 76,500 kama nauli ya kunirudisha chuoni huko kanda ya kaskazini jana akatokea jamaa mmoja anauza mbuzi 4 kwa Tsh. 60000 nikaamua kujitungua hivyo nikatumia nauli kununua mbuzi.
Mimi rohoni mwangu saivi nafurahi sana nitakapo kuwa mfugaji mkubwa sana na nimeanza kwa mifugo tofauti tofauti kama nguruwe 2, mbuzi 4, na kuku chotara mitetea 5 na jogooo 1.
Kusoma ni utumwa. Overa