Binafsi sipo upande wowote ila mtu kuacha chuo inategemeana na malengo aliyonayo, kitu gani kinachomfamya aache chuo?
Mtoa mada kama una malengo fulani (achana na ulivyonavyo kwasasa) ambayo unaona shule yako haitakuwa na mchango wowote hapo unaweza kuacha ili kuanza kufanyia kazi suala hilo.
Ila kama hali uliyonayo kwasasa kutokana na hivyo unavyomiliki ndio sababu kubwa kwako ya kuacha chuo, aisee usijaribu, huo ni muda wa mpito na ikitokea ukapata hasara either magonjwa au uwezo wa kutunza hiyo mifugo isiwepo utakumbuka sana huu wakati na kujuta laiti ungemaliza tu chuo.
Kiujumla kama una malengo ambayo ukiyafanyia kazi kwa moyo wote na upo kujitoa kwa namna yoyote, chukua hatua. Ila kama malengo yako ni ya kusuasua bora umalizie chuo.
NB: Malengo yako, maono yako ya mbele kiujumla ndiyo jambo la msingi, jithathmini kama unaona una wasiwasi wa aina yoyote juu ya yale unayotarget, nenda kamalize chuo.
Niliacha chuo, ila nilikuwa na malengo ambayo leo siwezi juta kuacha kwangu chuo mpaka keshokutwa.
Malengo uliyonayo, usimfikirie mtu yeyote, jifikirie wewe na uwe tayr hata kesho mambo yakiwa magumu uwe tayari kulipa kwa maamuzi unayoyafanya leo.
Narudia mkuu, malengo yako na strategies zitakazokufikisha hapo ziwe well defined.
Mtaani huku siyo rahisi kama unavyodhani, ukipata leo lazima uwe na akili ya kutambua kuwa piga ua garagaza kesho utakosa hiyo ipo huwezi ikwepa.
Ukipata jifunze kuweka ili kesho ukikosa bado una namna ya kuendelea kuishi.
Shule ni muhimu sana, but you'll never escape from your destiny!!