Nimedhulumiwa MilionI 10, siku ya Tano sasa sijapata Usingizi

Pole mkuu! Siku hizi marafiki ama ndugu linapokuja suala la pesa wanageuka kuwa mashetani. Ila amini kilicho riziki hakiliki kama kitalika ujue lazima kitokee sehemu ilipoingilia.
 

Sio wa kuzaliwa nae pekee ndio umwamini la!
Usimwamini mtu yoyote, labda Sana mama yako mzazi maana chochote atakachofanya mama bado hakitaweza kulipia mahangaiko aliopata juu yako.

Mimi nadhani huyo ndugu ungemuacha tu maana siku za mwanadamu sio nyingi na pamoja na uchache huo zimejaa fadhaha na mahangaiko, hatafika mbali. Lakini maumivu ya dhamiri atakayopata hayatakuwa na mfano.

Wewe Sasa kwa kuwa haukutenda ubaya kwa ubaya Basi wema utakulipa malipo makuu yenye heri na baraka, lakini pia kisa hiko kisikufanye uingie woga wa kufanya ishu nyingine Kama hizo kwa sababu ya kudhulumiwa, hayo hutokea mara moja moja Sana katika Safari ya mwanadamu ya utafutaji, bahati nzuri hali hizi hukuacha na funzo na hamasa zaidi pamoja na wema, maadam tu hautalipa kwa ubaya.
 
Mali siku zote huwa haiujui undugu wala Urafiki wala ujirani wala undugu wa kidini
 
Sina cha kukushauri ila nasikitika kwanini binadamu bado mnaaminiana? Aisee
 
Sisi ni marafiki, alikua na kazi nzuri baadae akafukuzwa alishuka sanaa sanaa, akaanza upya... hii project yeye ndio mwanzo alini invite kwakua alikua hana hizo sifa zote timilifu zilizokua zinahitajika.
Mkuu unanichosha zaidi unapozidi kumwita rafiki. Mtu kashakusnitch huyo Ni tapeli tu aliyekuwa anakutumia in the name of "Rafiki".

Halafu Kama kweli rafiki yako unakosaje kuwa na mawasiliano na familia yake let's say ndugu zake hapo angalau ujue wanapoishi ama uwe na namba zao.

Anyways pole kwa kutapeliwa. Kwenye pesa trust nobody, hakuna ndugu wala urafiki Yani wote ikija kwenye pesa assume unadeal na mtu usiyemjua.
 
Katika issue za hela usimwamini mtu, hakikisha mkataba uko wazi hela inalipwa kwenye account ya kampuni au kama hakuna akaunti then ilipwe kwenye joint akaunti, ungeondoa hiyo shida. Binadamu wengi, sio wote kwenye hela wanageuka wanyama.

Nakushauri wewe usiweke sana hiyo ishu kichwani kwani kukosa usingizi ni tatizo waweza kufa. Sasa ufe wakati hela inatafutwa? Huyu jamaa hafiki popote ni tamaa tu.
 
Umenikumbusha mbali sana,
Jinsi mhindi alivonizika 20M zangu, na wadau wakanigeuka kuwa nimepata hela nikala na mzungu wao nikawatosa.
 
Hata aliyezaliwa na wewe usimuamini mkuu
 
ANY WAYS KOSA ULILOFANYA KUBWA NI KUMUAMINI MTU AMBAE SIO MZAZI WAKO AU DADA AU KAKA YAKO...
Angekua ni mzaz wako au ndugu wa tumbo moja ungeweza msamehe ila kwavile huna undugu nae, Akishindwa kukulipa pesa zako MTOE UHAI au MTIE ULEMAVU UTAKAO MFANYA ALALE KITANDAN MAISHA YAKE YOTE.
Usiogope Ubaya Ubaya, Malipo ni hapahapa duniani...
 
Hao waasia watakuwa wamemuua halafu msala utakuangukia wewe, kwahiyo kuanzia sasa jihesabu uko Segerea kama sio Ukonga
 
Watu wa hivyo haiwachukui hata mwaka wanarudi na malalamiko mengi sana
Utamuona tena akiwa kafulia ile mbaya ila uongo utakuwa mwingi sana
Wa hivyo nimewaona sana
 
Duh!! Hongera sana hela zote lakini bado una nguvu hata kuandika, mimi nilidhulumiwa laki moja na nusu niliweweseka karibu mwezi wote...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…