Emmanuel Nchimbi ametangaza kustaafu siasa na utumishi wa umma.
Katika taarifa yake ya leo, amesema amemwandikia Rais Samia Suluhu Hassan kumjulisha uamuzi huo, akieleza kuwa anatimiza ahadi aliyowahi kutoa kwamba siku Rais atakapohitaji Makamu mwingine wa Rais, angeachia nafasi hiyo.
Uamuzi huo utaanza kutekelezwa tarehe 4 Septemba 2026.
Ameishukuru Rais Samia, CCM na Watanzania kwa imani na ushirikiano waliompa katika utumishi wake, akisema ataendelea kuwa raia mwema wa Tanzania.