Nimefanikiwa kuacha kunywa soda

Nimefanikiwa kuacha kunywa soda

Nimefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuacha pepsi, najua sitaweza kuikwepa 100% lakini walau isiwe uraibu. Naweza kunywa moja kwa wiki toka 3 kwa siku, naona maendeleo mazuri ikiwemo kuongeza ufanisi katika kufikiria lakini pia hata performance ya game,
 
Kweli mkuu ila tunatakiwa kula kwa kiasi. Ukubwa wa ugali inabidi iwe saizi ya ngumi yako. Sisi tunakula ugali mkubwa kiasi kwamba mtu aliyekaa upande wa pili humuoni. Tunakula ugali huku tumevua shati kuhakikisha ugali unaisha. Tunatakiwa tule ugali kidogo ila mbogamboga na matunda kwa wingi.
Kumbuka wengine tuko tinde kwenye majaruba ya mpunga,kula ugali size ya ngumi ni matusi makubwa,au unadhani wote tuko mjini
 
Mimi ni shahidi wa hili mzee wangu amefanikiwa kubalance sukari kutoka 22 Hadi 6 kwa kuacha kula wanga tu anatumia mbogamboga matunda na aina zote za protein. Ni kweli tumedanganywa sanaa
Asante mkuu kwa ushuhuda huu. Utasaidia wengi
 
You can't be serious ati kuacha soda ni zoezi gumu..😂
Hichi mbona kitu rahisi sana, mkuu Kama kuacha soda mpaka upambane vipi uraibu wa pombe je..? Punyeto vipi..?
Mkuu jitahidi uache aisee mi kinywaji Cha kiwandani nilichobakiza sahivi ni grand malt hii sidhani Kama nitaiacha japo huwa siinywi Mara kwa Mara..😅
Kuacha kwake sio rahisi kama wewe unavyofikiria,uraibu wa soda ukikuingia hauna tofauti na ule wa pombe...
 
Yes ni muhimu kupunguza sukari na wanga hasa vinywaji vya kiwandani kama aoda na juisi zenye sukari nyingi. Unaweza ukanywa juisi ya miwa kwani ni nzuri kiafya kama imetengenezwa kwenye mazingira ya usafi, lakini ni bora ule matunda kwani yana virutubisho vingi
 
Kupitia uzi huu na mm naenda kuacha kabisa, si mnywaji sana but hata hyo kdg naenda kuiua rasmi.
 
Mwaka 2017 nikiwa chuoni niliamua kuacha kunywa soda na soft drinks zote baada ya kupima sukari na kukuta ikiwa juu kiasi.

Sasa imetimia miaka 4 bila kunywa na nimezoea kabisa. Najihisi kuwa na afya njema sana na wala sitamani zaidi ya kuwaonea huruma wanaotumia. Asante Mungu!
kwa sasa sukari yako umepima ikoje?
nakushauri punguza pia matumizi ya vyakula vya wanga, jenga tabia ya kufanya mazoezi walau Dak 30 na iwe walau kwa wiki mara 3.
 
Mwaka 2017 nikiwa chuoni niliamua kuacha kunywa soda na soft drinks zote baada ya kupima sukari na kukuta ikiwa juu kiasi.

Sasa imetimia miaka 4 bila kunywa na nimezoea kabisa. Najihisi kuwa na afya njema sana na wala sitamani zaidi ya kuwaonea huruma wanaotumia. Asante Mungu!
Aaaah, hapo ni sawa kama unaumwa ni haki yako kuviacha! Nilifikri umeacha hivi hivi tu!
 
You can't be serious ati kuacha soda ni zoezi gumu..😂
Hichi mbona kitu rahisi sana, mkuu Kama kuacha soda mpaka upambane vipi uraibu wa pombe je..? Punyeto vipi..?
Mkuu jitahidi uache aisee mi kinywaji Cha kiwandani nilichobakiza sahivi ni grand malt hii sidhani Kama nitaiacha japo huwa siinywi Mara kwa Mara..😅
Usifanye mchezo kuacha ulevi wa sukari.
 
Soda sinywi juice ya kutengeneza nyumbani nakunywa ambayo haina sukari ...pepo limebaki kwenye gambee hii kitu kuacha nimeshindwa acha niendelee kunywa
Hata matunda yana sukari hivyo hata hizo juice za matunda nyumbani si salama sana kunywa kwa wingi kwa baadhi ya watu.
 
Hata matunda yana sukari hivyo hata hizo juice za matunda nyumbani si salama sana kunywa kwa wingi kwa baadhi ya watu.
Yule Prof Janabi alisema ni hatari Sana kunywa juice zilizochanganywa na matunda mbalimbali maana kila tunda Lina sukari yake kwa kiwango tofauti tofauti.
 
Aisee Sina huu ulevi sukari si shida kwangu! Yani mi nashangaa sukari inaulevi gani mpk iwe ngumu kuacha! 😂
Ni kwa sababu labda hauna huo ulevi ni sawa na ambaye si mnywaji wa pombe anavyomuona mlevi ila ulevi wa sukari ni mbaya kuliko unavyofikiri na ubaya sukari haipo tu kwenye soda juice au chai pekee. Tafuta kitabu kimoja kinaitwa Suicide by sugar humo utaelewa hatari ya hii kitu.
 
Back
Top Bottom