Uchaguzi 2020 Nimefanikiwa kushawishi ndugu zangu kumpigia kura Tundu Lissu

Uchaguzi 2020 Nimefanikiwa kushawishi ndugu zangu kumpigia kura Tundu Lissu

Salaam,

Kama kichwa cha habari kisemavyo hapo juu binafsi nimefanikiwa kuwashawishi watu kadhaa kuongeza ushindi kwa Tundu Lisu.
Nilianza na mke wangu ambae yeye kajiandikisha hapo kiwalani nikamweleza ameelewa na kuahidi atampigia kura.

Nikarudi kwa mama mdogo wangu huyu yeye alikuwa na biashara nzuri tu kipindi cha mkwere akajenga na kajumba na kufanya mambo kadhaa yeye mwenyewe ila wakati huu biashara hakuna na huwa anaomba nimpige tafu kwenye ada ya mwanae mmoja yeye nimemwambia unaona tofauti ya awamu iliyopo na ile ya mwanzo kasema ndio mwanangu nakusikiliza wewe.

Nikarudi kwa mama wakwe zangu wawili huwa wananipiga vizinga mara kwa mara na wao nimewaambia msipopiga kura kwa Tundu tusijuane wameelewa nao.

Mama yangu yeye hana noma kabisa nataka kumalizia kwa wadogo zangu wawili na baba nimalize kazi kwa upande wa ndugu.

Lengo la kuleta huu uzi ni kuwapa moyo vijana wenzangu tuwashawishi wanaotuzunguka na ccm waache kutubeza kwamba tunashinda mitandaoni huku sisi sio wapiga kura na hatuna ushawishi huko vijijini.

Ombi: naomba mniunge mkono wakuu kwa pamoja tutaweza kuangusha CCM.
Mimi nilishadanya hii kirambo Sana mabadiliko yanatuhusu wote
 
binafsi sijawai kupiga kura ila Lissu amenishawishi muda mfupi sana, ni aina ya kiongozi wa upinzani ambaye muda mrefu Tanzania ilikuwa inamhitaji dhidi ya hawa mabeberu waliotawala nchi toka 64, wale kina slaa, lowasa maalim seif hawamuoni huyu jamaa ni Lissu ni strong leader, sasa naamini upinzani unaweza shika dola
 
Miaka 60 bado watu wanakunywa matope badala ya maji je hayo ni Maendeleo? Hebu kuweni serious na hii nchi.
Usistaajabu hata USA wenye miaka 200 na zaidi bado wanashida ya maji...maendeleo huwa yanakuja kwa mipango na suala la maji limeshughulikiwa vizuri kuanzia awamu ya nne na sasa awamu ya 5 wanafanya vizuri zaidi.

Mpigie kura Dr. Magufuli atatua changamoto zetu za kimaendeleo.

JPM ANATOSHA
CCM USHINDI NI JADI
 
Back
Top Bottom