Nimefika mwisho, madeni yamenichosha!

Nimefika mwisho, madeni yamenichosha!

Serikali yenyewe ina daiwa Matrilionea una ogopa nini,kwanza unatakiwa ujipongeze una akili zako timamu ndio maana una kopesheka mkuu.
 
Acha kukopa ,waliokuzaa wakulipie hayo madeni.
Walionizaa hawajui ninachopitia, hata ni huruma kuwaambia, umri wa uzee, afya zao ndo haswa mtihani wetu. Siwezi kuongeza na hili langu. Nashindwa kumwambia yeyote.
 
Kila siku ni afadhali ya Jana. Sitamani hata kukuche, nimechoka mwili na roho, madeni yananimaliza, bora nipumzike nizikwe nayo.
Pole lakini tatizo halisolviwi kwa kulikimbia mkuu... Pambana kwa maana hata ukifa bado madeni yako yatakua pale pale.
 
Kausha damu au bank mkuu?
Ni ndugu na marafiki. Siyo kausha damu .....Sasa ninaposhindwa kuwalipa, nakosa chakuwaeleza zaidi. Nimejaribu kuuza shamba langu la miti Lina ekari kama 5, miti Ina miaka 10....hakuna mteja. Shamba lingenisaidia kufunga hii habari yote.
 
Mimi nadaiwa million 13..


Ila nakatwa kila mwezi so hainihumi sana maana Toka nianze kufuga KUKU na enjoy sana nakupa ukweli wana faida asikudaganye mtu Mimi shuhuda
Mie madeni yangu yanaweza fika 40+ lakini sina hata wasiwasi na mie pia nadai jumla 68+
 
 
Back
Top Bottom