Nimefika mwisho wa kufikiri.... Nifanyeje? Naomba msaada wako

Nimefika mwisho wa kufikiri.... Nifanyeje? Naomba msaada wako

Nashukuru sana kaka nadhani hali hiyo nimeanza kuishi Sasa shida ni Moja tu kiongozi.. nina familia nahitaji kazi nipate walau uhakika wa kulisha hawa binadamu wa 2 wanao nitegemea
Kazi utapata mkuu

Everything is blessing in this life

Mshukuru sana Mungu kuwa Bora hata wewe una access ya taarifa na connection Kuna watu muda huu hata access ya taarifa hana na haujui anafanyaje .


So hiyo ni changamoto ila inaonekana inaweza kuwa solved
 
Mimi mwenyewe jobless tu nimetoka kumaliza chuo mwaka huu nipo mtaani nashindwa Jf tu huku nikisikilizia michongo yangu itiki In Shaa Allaah .

Ningekuwa na mchongo sina mbambamba mapema tu ningesaidia kwa namna yeyote ile kwani napenda kusaidia watu ila nipo mtaani nasubiri mchongo niliowekeza utiki nianze maisha ya utafurahi In Shaa Allaah
Haukufanikiwa kupata nafasi ya kusoma nnje mkuu? Kuna kipindi niliona unapambania hili
 
Mimi mwenyewe jobless tu nimetoka kumaliza chuo mwaka huu nipo mtaani nashindwa Jf tu huku nikisikilizia michongo yangu itiki In Shaa Allaah .

Ningekuwa na mchongo sina mbambamba mapema tu ningesaidia kwa namna yeyote ile kwani napenda kusaidia watu ila nipo mtaani nasubiri mchongo niliowekeza utiki nianze maisha ya utafurahi In Shaa Allaah
Pamoja kaka pendekezo langu kwako kutokana na uzoefu wangu. Natamani ujifunze fani nyingine nje ya ulichosomea shule. Kama ukiwa na leseni ya udereva itafaa sana nimekuja ku observe sasahivi...
 
Mwenzenu ni kijana miaka 28 mwenye mke na mtoto mmoja... Nimekua nikifanya biashara ya mpesa Kwa miaka takribani 15 tangu nikiwa nyumbani hata baada ya kutoka nyumbani niliendelea kufanya biashara hiyo.

Kama mjuavyo biashara hiyo ni miongoni mwa biashara zinazo windwa mwaka 2021 baada ya kufanyiwa majaribio ya kuibiwa mala kadhaa nilighafilka na kuamua kuondoka kwenda kutafuta changamoto kwingine pale ofisini nikamuacha mama. Kwa bahati mbaya sikufanikiwa mwaka 2022 mwishoni nikarejea tena pale pale site.

Mwaka 2023 nikafanikwa kupata mtoto wangu wa kwanza, MUNGU alikua mwema biashara ilishamiri Kwa mwaka huo tangu 2022-2024 mwezi wa 4 nilikua nimefunga milion 7 kutoka kwenye milion 1 ya mtaji.

Mwaka 2024 niliongeza huduma za kibank Kwa NMB hapo ndipo mambo yalianza kwenda mrama, biashara ikaanza kuyumba, wateja wakaanza kupungua bila sababu yoyote na hatimaye nikashindwa kulipa Kodi tena Kwa kukosa mtaji. Nikaishiwa.

Nikatengeneza Banda la mabati yaliyo tumika nikiwa na mtaji wa 200k nikaanza biashara hiyo eneo jingine mtaa wa pili nikauza mashine yangu ya NMB Kwa dada yangu nikapata mtaji nikauchoma tena ukaisha. Unajua kwanini uliisha.?

Huko nyuma nilianzisha biashara ya kukopesha bila vibali nililenga watu wachache wa eneo Hilo Hilo ndio sababu ya kutengeneza milion 6 Kwa mwaka mmoja pekee. Hata nilivo pata pesa ya mauzo ya mashine ya NMB nilidhani kwamba napaswa kukopesha tena ili ninyanyuke, awamu hii nikakopesha kienyeji zaidi ya uenyeji wenyewe, Kwa kua na ki mtaji kilikua kidogo jamaa mmoja kakimbia na 300k mwingine wakaanza kusumbua nikapata hasara nikaishiwa.

Just imagine biashara nikawa naiendeshea Kwa mtaji wa 200k humo humo ulipe Kodi, chakula uhudumie mtoto mke na Mimi mwenyewe ikafika pahala nikafeli, sehemu nilio kua nimeweka Banda niliomba na mwenye Banda kanipa kama msaada ila Sasa anapataka kanambia nitoe Banda langu anapahitaji Leo week ya 2 Sina hela ya kuhamishia hata Banda. Nahisi Nisha mkwaza ila Sasa nitafanyaje..?

HApo nyuma nilipata bahati ya ki KAZI Cha wiki 2 nikaokoa 150k ila bro alie niitia hiyo KAZI anafahamu nacho pitia hivyo aliamua kunipa tu kazi hiyo ili nipate chochote kitu. Ilikua kazi ya usimamizi machimboni "ifugandi" KAZI ile niliifanya Kwa uaminifu na Kwa bidii kubwa hatimaye nikaimaliza.

Nimerudi home hela ikakata Kwakua tayari nina familia 150k si kitu Kwa familia inayo pitia ukata.. nikaomba KAZI ya saidia fundi tukaipiga Kwa siku 3 msingi, KAZI ilikua ngumu nusu nivunjike mguu maana jiwe la msingi lilinizidia nguvu wakati tumelibeba kwenye machera likaporomoka na kugonga miguu wangu kwakweli lilikua ni jabari la jiwe. Mungu mwema aliniokoa Kwa mapenzi yake. Nilichubuka Mikono nikatokwa na vidonda mikononi Kwa siku tatu nikachoka Chaka Chaka.

Kwanza niliwaza au pengine mm ni mzembe na mvivu je ningekua jeshini ningefangaje .? Mawazo yale niliyatumia kujitia moyo wakati ambao natarajia kubeba niwe, rahasha kumbe nilikua miongoni mwa watu walio jitahidi ujezi wa msingi wa mawe hua si Lele mama mafundi na vibarua wengi ealiukataa.

Wiki Moja Sasa nipo nyumbani Sina hata sh 100, katika wiki Moja hii jirani yangu ambae familia zetu Zina ukaribu ni fundi, na nifundi haswaa nimemuomba KAZI bila mafanikio si kwamba Hana KAZI anazo ila ikifika asubuhi ananichenga anaondoka bila taarifa. Hii awamu ya 3 Sasa. Sishangai Kwakua niliwah msikia live akimwambia mkewe kua hawezi kwenda na Mimi kazini kujenga Kwakua tutakosana hua najiuliza Kwanini tukosane. Ingawa jamaa ana mapungufu mengi maana ni wale jamaa waongea matusi sana pengine anajijua alivyo ndio maana kaona kuliko tukosane Bora tujenge heshima Kwa kutonipa KAZI. Lakini si anajua kua Sina maisha why asinipe kunisaidia.?

Any way nimepata wazo na nimeanza kulifanyia kazi: simu ninayo tumia Sasa ni infinix hot 40i nimeamua kuiuza Kwa sh 180k nipate mtaji nirudi kwenye biashara. Tayari nimetangaza kwenye groups akitokea mtu wa kuinunua basi nitatoka nje ya mitandao ya kijamii asipo tokea nitakua naingia humu na tutaendelea kuwemo.

Ingawa kabla ya kuchukua maamuzi haya niliwaza nina Facebook page ambayo Iko monitized ambapo nilipewa mwaliko mwezi ulio isha nina dollar 1.47 tu maana Sina muda wa kupost na Sina pesa je nikiuza simu si wataniondoa kwenye orodha ya watu wanao lipwa.?

Kwenye pita pita Facebook nimejiunga magroup mengi ya kitalii ambapo niliwaza kama ningekua nime settle nina utulivu ningepata muda mzuri wa kujifunza mengi kuhusu utalii na Kwakua nina page ambayo maudhuhi yake niya Mpira ila nina page nyingine ninayo post mambo ya vivutio vya Tanznaia kwakweli inamuitikio si ninge kua mshauri na pengine nyota ingewakia huko.?

Kiukweli nimeomba kazi kwenye taasisi nyingi karibu 7 changamoto ni fani, najilaumu sana kwamba nilibweteka Kwakua ofisi yangu huko nyuma iliniaminisha kwamba inaweza kinivusha kutokana na ubusy wa kuihudumia nikaisahau. Sasa ni baba mwenye mke na mtoto ndio natambua umuhumu WA kuwa na fani mjini.

Lakini KAZI skua naomba zenye fani, nimeomba kazi yoyote ofisini office assistant, kazi yoyote ambayo mm naweza kuifanya bila kua na fani yoyote. / kama Kuna mtu anaweza jitolea kuokoa jahazi mm ni MWEPESI kujifunza naweza kufanya KAZI huku najifunza tafadhali niokoe.

Nimeomba kazi hizo kwenye makampuni ya cargo na logistics, kampuni za uuzaji magari n.k sijaitwa, nimeomba vibarua mgodini sjaitwa. Nasubiri neema ifunguke nahisi nimefika hatua ya mwisho ya kufikili. Natamani nitoke nikapambane nje ya circle yangu lakini nina home tie tayari natamani nipate sehemu ya uhakika kwamba nikitoka niwe na uhakika kwamba naweza kuwalisha wanangu angalau Kwa hatakwa uchache hapo ndipo najikosoa kwamba natoka naenda wap, kufanya Nini nafikia Kwa nani je wiki ya kwanza,2,34 mwezi nitakua Nisha pata Cha kulisha walio nyumbani.?

Wakati huo unaweza hayo unakutana mitandaoni mwijaku kazawadiwa gari ya milion 80, nawaza dah hawa watu si niliwah watumia email ya kuomba kazi ya kibarua chochote katika ofisi zao, na nikatoka ofa ya kuwa advertise kwenye ki page changu Kila napo post lakini wapi.!

Any way, sinaga huruka ya uongeaji saana nadhani nimetoa ya Moyoni Kwa uchache wake.... Ndugu zangu naombeni kazi, naombeni kazi, Kuna muda mwanangu anachemka naishia kumpa Panadol tu Kwakua najua nikienda maabara au hospital ingeweza kuchukua 10+ ambayo ni bajeti yangu ya kula Kwa siku 4 nachangua kumpa Panadol walau awe na uhakika wa chakula,ingawa afya ni muhimu... Hayo maumivu kama baba unajisikiaje kushindwa kumtibu mwanao.?

Ndugu zangu naombeni kazi, connection yoyote au hata msaada wowote.

Ingawa niliwaza kua niuze siku nitakua na sh 150k kama atatokea WA kununua Kwa Bei hiyo. Nikope 200k niwe na 350k nitumie 60k kuhamisha Banda na kulipia Kodi kwingine nibaki na angalau 250k nianze huduma ya mpesa. Ama ninunue computa used nianze kubun series huku najifunza ujuzi mwingine kupitia kompyuta hiyo.

Angalia namna unavyo weza kunisadia Mungu akuguse nakukaribisha PM,

Naelewa si vyema kuanika mawasiliano yangu hadharani Lakini mm Sasa ni nani kwenye dunia hii.?

unaweza kunipigia namba 0744666115..
Upo mkoa upi,
 
Ok, jirani na flame yangu kulikua na ofisi ya mikopo ambapo nilichukua uzoefu kidogo namna wanavyo oparate biashara hiyo na ilinipa matokeo. Nakili kosa kwamba kule niliko hamia nilikosea Kwa kuwapa hela kienyeji zaidi nafikili ilitokana na presha ya kutaka ku recovery mapema.

By the way kilicho tokea ni funzo kaka na historia haisifiwi tuangalie wakati huu.

Naomba mchongo wa kazi mkuu mm ni mwaminifu na mchapa kazi, nipo tayari kufanya kazi yoyote na popote
 
Haukufanikiwa kupata nafasi ya kusoma nnje mkuu? Kuna kipindi niliona unapambania hili
I'm waiting for a visa approval now , kila kitu kimeenda sawa nimeshakubaliwa nasubiri Visa tu kwa sasa ndio inachelewa nchi za zilizoendelea ulimwengu kwanza kutoa Visa ni process ndefu . Pesa yangu yote M2+ nimeweka huko nasubiri matokeo tu , wakinifelisha naanza maisha upya nikiwa na sifuri
 
I'm waiting for a visa approval now , kila kitu kimeenda sawa nimeshakubaliwa nasubiri Visa tu kwa sasa ndio inachelewa nchi za zilizoendelea ulimwengu kwanza kutoa Visa ni process ndefu . Pesa yangu yote M2+ nimeweka huko nasubiri matokeo tu , wakinifelisha naanza maisha upya nikiwa na sifuri
Ungetaka India ni fasta tu mkuu
 
Pamoja kaka pendekezo langu kwako kutokana na uzoefu wangu. Natamani ujifunze fani nyingine nje ya ulichosomea shule. Kama ukiwa na leseni ya udereva itafaa sana nimekuja ku observe sasahivi...
Nilivyomaliza tu sikutaka kukaa Bure nilienda Veta kusoma driving sasa nina cheti kabisa cha udereva , niliona udereva mzuri sana haswa kwa michongo ya kwenda mambele ukizingatia nilishatafutaga passport mapema toka nipo chuo
 
Back
Top Bottom