Pole ndugu mleta ,nyakati unazo pita sote tunapitia hivyo ila wewe umedhubutu kusema , hongera, hata kama huta pata msaada wa moja kwa moja lakini miongoni mwetu hatakosekana mmoja wa kukuombea dua , naomba kuwa mmoja wapo wa hao.
Mwenyezi Mungu mwenye huruma na upendo akutangulie, akukutanishe na mtu mmoja ambaye ataibadilisha leo yako ,na familia yako naam na yupo njiani kukutana nawe maybe miongoni mwetu.
Hata hivyo usiumie sana wala kufadhaika , kama jana ilikua ngumu sawasawa na leo nayo ilipita hata leo itapita hivyo hivyo kadhalika na kesho na hata kesho yake hadi nyakati ngumu zipie, sala dua maombi yangu kwa Mungu ujaliwe kuvuka salama ndugu yangu.