Nimefika safari yangu, wife hajaniuliza hata kama nimefika salama

We ndie wakumjulisha kuwa umefika yeye ndo akuambie pole na safari.
Au na wewe nilisumbufu anashukuru kuondoka kwako
 
Hatujui chanzo cha gumzo Lao nyumbani, ila kitendo cha mkewe kuwa online anachati na watu wengine bila kumjulia hali mumewe ni dosari. Hata sms tu inatosha, ni bora hata kama asingeijibu fresh tu
Ndani ya nyumba kuna mengi, mleta uzi naona ana shida, kanuni ni moja tu" mpende mke, atakuheshimu". Msingi wa upendo ndani huanza kwa mme kwa kuwa ndie alianza kumpenda mwanamke hata kabla huyo mwanamke hajafaham kama anapendwa, baadae ndipo alipomfuata na kumjulisha(kumtongoza).

So from there, mwanamme inabidi ampende daima mke wake.

Huyu mwanaume ni kama ana mentality ya kunyenyekewa kwa lazima. Upendo haulazimishwi, atengeneze upendo kwa mke wake, asipojibiwa kwa upendo mkubwa zaidi ya anaouonyesha, basi mwanamke atakuwa na shida.

Kwa sasa mwanamme ndio mwenye makosa. Basi angefikiria huo mgogoro aliouacha nyumbani ndio sababu akaishia hapo kuliko kuanza kuji-stress mwenyewe
 
Wee nawe mpuuzi ulioa ili iweje... Embu achana na huyo mwanamke... Fukuza arudi kwao baki na watoto... Wanawake ni chombo cha STAREHE...
 
Wajinga sana,sasa kama umesafiri kwa nini usimjulishe mwenzio mama nimefika salama,tabia za wanaume wanaopenda kubembelezwa bembelezwa.
 
Uzuri mmoja mpka tufike huko utakuta wanaume halisi tumeshakufa walibaki ni mabunga na wapaka poda tu watajuana wenyewe 😁😁😁😁
 
Kweli vijana wenye ndoa mnaishi apa duniani kama digidigi poleni sana wakuu.
 
Uzuri mmoja mpka tufike huko utakuta wanaume halisi tumeshakufa walibaki ni mabunga na wapaka poda tu watajuana wenyewe 😁😁😁😁
Hapana tayari tushafika Huko ndio maana unaona siku hizi malalamiko mengi yanatokea upande wenu 😁😁
 
Ofcoz tulikuwa na kamgogoro flani wakati naondoka.

Lakini ni masaa 14 toka nifike in my destination ila wife hata hajanipia kunijulia hali ila whatsapp yuko mudo wote namuona online.

Nifanyaje wakubwa?
Fanya mambo yako wife wako pia ni binadam anaghafirika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…