Nimefika safari yangu, wife hajaniuliza hata kama nimefika salama

Nimefika safari yangu, wife hajaniuliza hata kama nimefika salama

Ofcoz tulikuwa na kamgogoro flani wakati naondoka..
Lakini ni masaa 14 toka nifike in my destination ila wife hata hajanipia kunijulia hali ila whatsapp yuko mudo wote namuona online.

Nifanyaje wakubwa?
Tuliposema kataa ndoa ulituona mafaaaaaaala
 
Familia wote mkijifanya much know hamuwezi kufika popote,mi huwa nashangaa inakuwaje mtu mnagombana mpaka unasafiri unaacha mgogoro,I wish initokee hata siku moja make hapa kwangu hata lisaa halipi ugonvi umeisha.
Kiburi kikishaingia ndani ya nyumba ni hatari sana na ni hatari zaidi kama wote ni watu msiokubali kujishusha ili mambo yakae sawa. Kupishana kupo kama binadamu lakini 14 hrs inapita bila mawasiliano na ni wanandoa hii ni hatari. Hapo mwenye kufanya ujinga akidhani anamkomoa mwenzie ndio anapata mwanya.
 
Ofcoz tulikuwa na kamgogoro flani wakati naondoka..
Lakini ni masaa 14 toka nifike in my destination ila wife hata hajanipia kunijulia hali ila whatsapp yuko mudo wote namuona online.

Nifanyaje wakubwa?
Mtumie meseji kuwa nimefika salama. halafu endelea na hicho kilichokupeleka kwenye hiyo safari
 
Ofcoz tulikuwa na kamgogoro flani wakati naondoka..
Lakini ni masaa 14 toka nifike in my destination ila wife hata hajanipia kunijulia hali ila whatsapp yuko mudo wote namuona online.

Nifanyaje wakubwa?
Wewe ndiye mwenye makosa, ulipofika ulimjulisha kuwa umefika? Ulimjulisha kuwa umefika salama? Kama hujafanya una makosa, fikiria makosa yako kwanza, naona wewe unapenda kupokea, hutaki kutoa
 
hapa umeongea ki mlengo wako, the way ulivyofikiri na the way unavyofikir na unavyoona JADDA.
Huwa siongei kimtazamo wangu, kwa sababu ningekuwa naongea kimtazamo wangu basi wanaume wote mngefurahi, mimi huwa naongea uhalisia uliopo tu
 
Ofcoz tulikuwa na kamgogoro flani wakati naondoka..
Lakini ni masaa 14 toka nifike in my destination ila wife hata hajanipia kunijulia hali ila whatsapp yuko mudo wote namuona online.

Nifanyaje wakubwa?
Piga chini mkuu, utakufa mapema kwa stress
 
Hata kama wamekwazana mke mwema lazma awe na hofu ya mumewe, yeye yupo nyumbani salama, mumewe kaenda kutafta riziki yeye kamlia buyu... hio ni redfag kubwa sana
Wa kwanza kulaumiwa ni mwanaume kwanza kasafiri nyumbani kaacha mgogoro na mpaka anafika anakaa kimya akisubiri mkewe amuanze hii si sawa. Hata mkewe kakosea pia masaa 14 bila mawasiliano na mumewe si vizuri. Wote wana makosa jamaa akiwa anaongoza kukosea.
 
Kuwa online ndo kuonyesha ana chat mda wote, huenda kawasha data alafu anaendelea na mambo mengine. Jaribu kumpigia umjulie hali kisha umwambie juu ya safari yako. Vumilia tu mkuu, haihitaji uwe na hasira wala mashaka.
 
Tatizo n nn hapa?? Kuwa online ama kutokukucheck??
Uliekua na safar n ww, so, kama umefika mjuze umefika. Mambo madogo haya.
 
Wa kwanza kulaumiwa ni mwanaume kwanza kasafiri nyumbani kaacha mgogoro na mpaka anafika anakaa kimya akisubiri mkewe amuanze hii si sawa. Hata mkewe kakosea pia masaa 14 bila mawasiliano na mumewe si vizuri. Wote wana makosa jamaa akiwa anaongoza kukosea.
Hatujui chanzo cha gumzo Lao nyumbani, ila kitendo cha mkewe kuwa online anachati na watu wengine bila kumjulia hali mumewe ni dosari. Hata sms tu inatosha, ni bora hata kama asingeijibu fresh tu
 
Back
Top Bottom