Nimefika salama Qatar kutokea Thailand kwa ajili ya kuangalia mechi za kombe la dunia

Championship

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2019
Posts
5,500
Reaction score
10,616
Nilipanga mwaka huu niwepo viwanjani live na nimefanikiwa kufika Qatar. Ilibakia kidogo sana nikose maana moja ya client wetu alipata changamoto ya mifumo kule Bangkok na ikabidi nisafiri wiki hii kuweka mambo sawa.

Miaka yote kwenye kombe la dunia huwa nazipenda Ufaransa, Ujerumani na Italia lakini mwaka huu nitapenda Argentina abebe ili Messi amalize na mafanikio ambayo ni ndoto ya kila mchezaji mkubwa.

Nategemea upinzani mkali kutoka Spain, England, Portugal, France, Belgium, Germany na Brazil. Ninaamini kama Argentina hatabeba basi bingwa atakuwa moja ya timu hizo.

Pamoja na kuwepo kwa Gabriel Jesus na Gabriel Martinelli ambao ni vijana wa chama langu la Arsenal, bado Brazil ndio timu nisiyoipenda zaidi ikifuatiwa na Portugal halafu England.

Kwa upande wa Afrika huwa napenda Nigeria na Cameroon ila mwaka huu nawapendelea zaidi Senegal na ninaamini wataliletea heshima bara letu kwa kufika nusu fainali ingawa Mane ana hatihati ya kutocheza.

Jamaa zangu wavaa kobazi huwa tunataniana na kuelimishana hapa jukwaani. Mnitakie heri maana huku nimepanga niondoke na watu watano wenyeji wa Qatar watakaotoa maisha yao kwa Bwana Yesu Kristo.

Qatar ndio nchi niliyowahi kufika mara nyingi zaidi hapa duniani ukiondoa Tanzania ambako ni nyumbani hivyo naifahamu pamoja na ukali wa sheria zao. Safari hii nitakuwa na muda wa kutalii kiasi na kupiga gombo. Hopeful hawataniweka kizuizini.😂

Natarajia wengi tutapata msukumo wa kujiandaa ili tukutane US, Canada na Mexico mwaka 2026.

Nawatakia world cup njema
 
Nilipanga mwaka huu niwepo viwanjani live na nimefanikiwa kufika Qatar. Ilibakia kidogo sana nikose maana moja ya client wetu alipata changamoto ya mifumo kule Bangkok na ikabidi nisafiri wiki hii kuweka mambo sawa.

Miaka yote kwenye kombe la dunia huwa nazipenda Ufaransa, Ujerumani na Italia lakini mwaka huu nitapenda Argentina abebe ili Messi amalize na mafanikio ambayo ni ndoto ya kila mchezaji mkubwa.

Nategemea upinzani mkali kutoka Spain, England, Portugal, France, Belgium, Germany na Brazil. Ninaamini kama Argentina hatabeba basi bingwa atakuwa moja ya timu hizo.

Pamoja na kuwepo kwa Gabriel Jesus na Gabriel Martinelli ambao ni vijana wa chama langu la Arsenal, bado Brazil ndio timu nisiyoipenda zaidi ikifuatiwa na Portugal halafu England.

Kwa upande wa Afrika huwa napenda Nigeria na Cameroon ila mwaka huu nawapendelea zaidi Senegal na ninaamini wataliletea heshima bara letu kwa kufika nusu fainali ingawa Mane ana hatihati ya kutocheza.

Jamaa zangu wavaa kobazi huwa tunataniana na kuelimishana hapa jukwaani. Mnitakie heri maana huku nimepanga niondoke na watu watano wenyeji wa Qatar watakaotoa maisha yao kwa Bwana Yesu Kristo.

Qatar ndio nchi niliyowahi kufika mara nyingi zaidi hapa duniani ukiondoa Tanzania ambako ni nyumbani hivyo naifahamu pamoja na ukali wa sheria zao. Safari hii nitakuwa na muda wa kutalii kiasi na kupiga gombo. Hopeful hawataniweka kizuizini.[emoji23]

Wale jamaa wa tupia kapicha nimewawekea hapo chini nikiwa Suvarnabhumi international airport pale Bangkok na nilipofika Hamad international airport hapa Qatar.

Suvarnabhumi international airport

View attachment 2420567

Hamad international airport

View attachment 2420568
Inaonyesha wazi kuwa wewe sio mtizamaji ni mwanga au mchawi wa mchana kweupe!
 
Back
Top Bottom