Bush Dokta
JF-Expert Member
- Apr 11, 2023
- 24,831
- 45,154
Huko unakosema kuna fursa kuna watu kibao wako huko na hawajatoboa na hizo fursa.Nililetaga Uzi wangu kuhusu biashara ya spare nahisi mwaka jana,
nilienda kuongea na rafiki yangu akanishauri nifungue vitu vya urembo wa magari, Kwa kweli nilianza kwa ugumu sana nikiwa bado sielewi vitu vingi.
Mkoa wa Tabora ni mkoa mkubwa sana, changamoto Kwanini bado maendeleo ni machache ni sababu ya miundombinu ilikuwa mibovu, kwa sasa kidogo panaanza kufunguka.
Nilileta Uzi wa makontena ya kuhifadhia ndizi bado sikupata muitikio mzuri sana, japo kuna mtu nipo naongea nae kwa sasa ananielekeza baadhi ya mambo.
Ukifika Katavi, Kahama, Geita utaona kuna fursa nyingi sana.
Binafsi nililemaa sana kukaa kariakoo, lakini hivi sasa kila siku akili inapanuka kukutana na watu tofauti tofauti na fursa ni nyingi.
Karibu mkuu.
Usione watu ukadhini ni wajinga.
Ukisikia Kilo ya Mahindi Tanga au Mbarali Mbeya ni Tsh 500 tu.
Ukienda Dar kilo ya Sembe ni Tsh 2000.
Unaweza kujiuliza kwanini watu wa huko hawafanyi viashara ya Mahindi kupeleka Dar?