DOKEZO Nimefuatilia suala la matumizi ya Elimu Bila malipo kiukweli Serikali ifuatilie kwa kina, kuna kitu…

DOKEZO Nimefuatilia suala la matumizi ya Elimu Bila malipo kiukweli Serikali ifuatilie kwa kina, kuna kitu…

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Nashauri serikali iweke mifumo IMARA ili fedha za elimu bure zitumike Kama malengo yalivyo na siyo kuachia wakuu wa shule wazitumie tofauti na matakwa ya serikali.

Baadhi ya shule zimekuwa tegemezi, fedha zikitoka hazijulikani zinatumika wapi, watoto karibia shule nzima wanakaa chini, ukarabati haufanyiki.

Hakuna vifaa vya kutosha mfano kuna shule moja kata ya LUSU huko Nzega DC inapokea kiasi cha SHILINGI laki NNE kila mwezi lakini kuanzia darasa la awali hadi la saba wanakaa chini, hakuna mipango tena ya kukabiliana na tatizo hilo wanategemea serikali mpaka itakapogundua tatizo hilo.

Nashauri serikali ifanye jitihada za haraka ZAIDI ifuatilie matumizi ya fedha za walipa Kodi hadi mashuleni. Ukaguzi ufanyike mara kwa Mara. Utaratibu wa manunuzi ubadilishwe.
 
Back
Top Bottom