Huo uhaba wa dawa una zaidi ya miaka sasa . Hivi wafahamu pamoja na Serikali kujinasibu kuongeza bajeti ya dawa lakini kiuhalisia hiyo bajeti haitoki? Hivi unafahamu kwa zaidi ya miaka 2 Serikali haikupeleka pesa ya kununua dawa kutoka Hazina kwenda kwenye Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali? Hizo dawa zingenunuliwa kwa pesa ipi?
Hivi wafahamu pesa za Mfuko wa Afya ( Health Sector Basket Fund) hazikupelekwa Halmashauri almost mwaka wote wa 2020? Wadhani uendeshaji wa Idara ya Afya katika mila Halmashauri ya Wilaya (CHMT) na Sekretatieti za Mikoa ( RHMT) ulikuwaje?
Serikali itimize wajibu wake wa Msingi wa kuhakikisha MSD Kuna dawa za kutosha na pesa kwenye Vituo ziwepo za kutosha Kama utaona hivyo vilio
Kwa taarifa yako Serikali ya Magufuli imepeleka Fedha nyingi MSD kuliko kipindi chohote toka nchi ipate UHURU mwaka 1961. Kati ya July 2016 Hadi Mei 2019 Hazina walipeleka Tsh 314 Bilioni sawa na Tsh 104 Bilioni kwa mwaka. Mwaka 2015/16 wakati Serikali ya JK inaondoka walipeleka Tsh 30 Bilioni.
Katika historia ya MSD kipindi cha UMMY Mwalimu tulijionea kwa mara ya kwanza Waziri akiwa na mahusiano ya karibu sana na Mkurugenzi wa MSD Laurean Bwanakunu. Walikuwa na mahusiano ya kingono na kugawana Fedha kwa kupitia kwa Katwaza wa Bahari Pharmacy ambaye walikuwa wanampa mikataba mingi ya ku-supply dawa hasa vile vifaa vya kits za kujifungulia akina mama.
Haya ninayoyasema siyo majungu yako kwenye Ripoti ya Katibu Mkuu Hazina kutokana na special audit ya October 2019- February 2020. Na matokeo ya Special Audit hiyo ndiyo Rais JPM aliweza kumtumbua Bwanakunu kutoka nafasi ya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa MSD. Na hatimaye kufunguliwa mashtaka ya kuhujumu uchumi na TAKUKURU.
Mtaji wa MSD umekatika kabisa kwa vile kipindi cha Bwanakunu wamekuwa wananunua dawa zenye muda mfupi toka nje ya nchi hivyo basi kuna mrundikano wa madawa yapatayo Bilioni zaidi ya 30 ambayo yame EXPIRE.
Kwa mwaka 2019/20 kweli Serikali haikupeleka Fedha kwa kuwa ilikuwa inataka ijiridhishe kwa nini mtaji unaporomoka.
Lakini Bwanakunu hakupaswa kutumbuliwa peke yake bali hata Waziri UMMY Mwalimu alipaswa atumbuliwe pia. Nashangaa DOUBLE STANDARDS za JPM kumuacha na kumfanya Waziri wa Mazingira na Muungano.
Kama MSD imefeli na wamegundua tatizo Ni Mkurugenzi Mkuu basi na Waziri anahusika kwa vile alikuwa ANAMLINDA. Kama Tume ingekuwa imeundwa na UMMY Mwalimu na kugundua mauza uza ya Bwanakunu Basi Waziri angekuwa hana hatia. Lakini Tume iliundwa na Dotto James, Katibu Mkuu Hazina
Tumuache Dr Dorothy Gwajima afanye kazi, kamwe tusimfananishe na UMMY Mwalimu.