Nimefukuzwa kazi kisa kugoma kumfatia bosi vitumbua vya mia tisa

Nimefukuzwa kazi kisa kugoma kumfatia bosi vitumbua vya mia tisa

muafi

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2015
Posts
2,557
Reaction score
6,128
Habari zenu

Katika hali isiyo ya kawaida siku ya leo nimepewa rasmi barua ya kuachishwa kazi kwa kosa la utovu wa nidhamu

Shughuli ilianzia Alhamisi iliyopita mida ya saa tatu bosi aliniita ofisini na kuniagiza vitumbua vya mia tisa

Kwakweli kulingana na nilivyokuwa mimi mtu mzima nimevaa nimependeza, nimechana nywele vizuri kama kazi inavyotaka

Nilikuwa nimevaa yale mashati ya kuwaka waka yale ya tetroni na nimechomekea na kuvaa suruali ya kitambaa, kitendo cha bosi kuniagiza vitumbua vya mia tisa kwangu niliona kama ni fedheha kubwa sana kwasababu sio majukumu yangu na ni kama dharau kwangu,

Yaani mimi nitoke ofisisni niende nje eti nimeagizwa vitumbua? Nilimwambia bosi kuwa sitaweza kwenda maana nina kazi na niko bize.

Mimi nina mke na watoto uniagize vitumbua?

Ijumaa nilisimamaishwa kazi na leo rasmi nimeachishwa kazi

Hivi hii ni sawa kweli? nakusudia kwenda kwenye vyombo vya sheria
 
Watu mnapitia magumu sana, ila pole sana. Kwa hiyo umefukuzwa kazi pasipo kuambiwa nini kimepelekea wewe kuachishwa kazi?
 
Back
Top Bottom