Habari zenu
katika hali isiyo ya kawaida siku ya leo nimepewa rasmi barua ya kuachishwa kazi kwa kosa la utovu wa nidhamu,
shughuli ilianzia alhamisi iliyopita mida ya saa tatu bosi aliniita ofissini na kuniagiza vitumbiua vya mia tisa,
kwakweli kulingana na nilivyokua mi mtu mzima nimevaa nimependeza, nimechana nywele vizuri na nimechomekea,
nilikua nimevaa yale mashati ya kuwaka waka yale ya tetroni na nimechomekea na kuvaa suruali ya kitambaa nimechomekea, kitendo cha bosi kuniagiza vitumbua vya mia tisa kwangu niliona kama ni fedheha kubwa sana
yaani mimi nitoke ofisisni niende nje eti nimeagizwa vitumbua? nilimwambia bosi kua sitaweza kwenda maana nina kazi na niko bize,
ijumaa nilisimamaishwa kazi na leo rasmi nimeachishwa kazi
hivi hii ni sawa kweli?