Nimefukuzwa kazi kisa kugoma kumfatia bosi vitumbua vya mia tisa

Nimefukuzwa kazi kisa kugoma kumfatia bosi vitumbua vya mia tisa

NI SAWA KABISA,

NENDA KACHOMEKEE HUO MSHATI WAKO BARA BARANI MJINGA MKUBWA
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]makasiriko yanini mkuu mwenzio ndo alijiona kapendeza sasa
 
Kuna mada nyingine mnatunga ili mje kupata attention hapa jukwaani, mwisho wa siku unaonekana mshamba

Maxence popote ulipo kwa sasa hizi senior member na expert member itapendeza kama mtu atapata kwa kulipia au kwa content anazoshusha hapa jukwaani!
Umeongea ukweli mkuu.
 
Hiyo busara itumike kwa nani? Mtuma vitumbua au mtumwa vitumbua?

Hivi ukiwa boss unaweza kufika officin ukamtuma officer wako vitumbua? Halafu ukamfukuza kazi sababu tuu hajaenda kukununulia vitumbua?

Huyu muafi kuna kitu hajasema Labda hiyo ilikua kati ya yale majukumu yake....

Au alikula vitumbua vya boss halafu akaambiwa akanunue vingine na yeye akagoma😂😂😂😂😂😂
Yeye s lazima aende angetuma ata mtu mwingine angetafuta boya wake nae amtume amwambie ametumwa na boss au angeenda kwa muuza vitumbua angempa ela tu afu amwambie alete yeye mwenyew kingine Kama ulivosema inawezakana kuna kitu kingine tofaut na vitumbua au inawezakana n chai tu na uwongo wake wa kutunga story alete kikiii
 
Siwezi kukumbuka link ya story ya miaka 6 au saba iliyopita.
Tafuta taarifa za ajali ya ndege kwenye milima ya alpes iliua watu zaidi ya mia. Fuatilia taarifa za rubani msaidizi aliyekuwa na miaka chini ya 30 wakati huo matukio aliyofanya siku chache kabla ya ajali.
Mojawapo ni kutumwa na rubani mkuu kazi anazodai yeye hakusomea kama anavyolalamika mtoa mada kutumwa vitumbua 9 kitu ambacho hakusomea.

Kwahiyo mtoa mada hiyo ni aina gani ya mtu?pamoja na mtoa mada
 
Nimeupenda msimamo wa boss wako! Dawa ya vijana jeuri ni hiyo tu hakuna namna! Hii inanikumbusha mwaka 2005 kibaka mmoja eti akaja na suti ofisini wakati sisi tulikuwa watu wa field, akajitia ujuaji kupiga suti eti anikoge mimi boss wake! Sasa kimbembe kikaja umeme ukakata na generator halina mafuta, gari nalo limetoka nje hakuna usafiri, ikabidi nimbebeshe dumu lakubebea mafuta na suti yake! Hebu piga picha dumu liko kwenye mfuko wa Rambo (enzi hizo) na suti yako! Nilimkomesha siku hiyo! Hakurudia tena kuvaa suti, nyoko kabisa!
Umejiona mjanja? Mbona mimi nimekuona punguani mmoja usiejielewa? Kwa hiyo kuvaa kwake suti kulikuuma sana? Ukaona umkomeshe mwenyewe kwa lugha nyingine umtie adabu.
 
Habari zenu

Katika hali isiyo ya kawaida siku ya leo nimepewa rasmi barua ya kuachishwa kazi kwa kosa la utovu wa nidhamu

Shughuli ilianzia Alhamisi iliyopita mida ya saa tatu bosi aliniita ofisini na kuniagiza vitumbua vya mia tisa

Kwakweli kulingana na nilivyokuwa mimi mtu mzima nimevaa nimependeza, nimechana nywele vizuri na nimechomekea

Nilikuwa nimevaa yale mashati ya kuwaka waka yale ya tetroni na nimechomekea na kuvaa suruali ya kitambaa nimechomekea, kitendo cha bosi kuniagiza vitumbua vya mia tisa kwangu niliona kama ni fedheha kubwa sana.

Yaani mimi nitoke ofisisni niende nje eti nimeagizwa vitumbua? Nilimwambia bosi kuwa sitaweza kwenda maana nina kazi na niko bize.

Mimi nina mke na watoto uniagize vitumbua?

Ijumaa nilisimamaishwa kazi na leo rasmi nimeachishwa kazi

Hivi hii ni sawa kweli?
Hiyo kazi ulikuwa unafanya si kazi na jnaonekana haina hela.

Umepewa nafasi ya kupata kazi nyingine yenye pesa zaidi.
 
Habari zenu

Katika hali isiyo ya kawaida siku ya leo nimepewa rasmi barua ya kuachishwa kazi kwa kosa la utovu wa nidhamu

Shughuli ilianzia Alhamisi iliyopita mida ya saa tatu bosi aliniita ofisini na kuniagiza vitumbua vya mia tisa

Kwakweli kulingana na nilivyokuwa mimi mtu mzima nimevaa nimependeza, nimechana nywele vizuri na nimechomekea

Nilikuwa nimevaa yale mashati ya kuwaka waka yale ya tetroni na nimechomekea na kuvaa suruali ya kitambaa nimechomekea, kitendo cha bosi kuniagiza vitumbua vya mia tisa kwangu niliona kama ni fedheha kubwa sana.

Yaani mimi nitoke ofisisni niende nje eti nimeagizwa vitumbua? Nilimwambia bosi kuwa sitaweza kwenda maana nina kazi na niko bize.

Mimi nina mke na watoto uniagize vitumbua?

Ijumaa nilisimamaishwa kazi na leo rasmi nimeachishwa kazi

Hivi hii ni sawa kweli?
Ukiwa kazini huwa hatuangalii una familia wala nini. Ndio maana halisi ya kazi. Na huenda ilikuwa kipimo tu.
Nimewahi kufanya kazi sehemu fulani wiki ya kwanza ya ajira ilikuwa kusafisha mazingira kwa kuondoa majani wakati tumetangaziwa kazi nzuri tu. Tuliajiriwa kwa pamoja kama watu 20 hivi. But waliondoka watu 12 tukabaki 8 baada ya hapo tukawa kwenye vitengo vyetu na pesa tamu kabisa.
 
Safi Sana,huo ndio uanaume. Sawa kazi ni mzuri lakini isikufanye upoteze utu wako. Pambana tafuta shughuli yako mwenyewe ya kujipatia kipato huwe huru. Babu yangu kafa kwa heshima hakuajiriwa,baba mzazi tumemzika kwa heshima hakuajiriwa na mmi mwenyewe Sina mpango was kuajiriwa.
Bro tupeane maujuzi inbox
 
Umejiona mjanja? Mbona mimi nimekuona punguani mmoja usiejielewa? Kwa hiyo kuvaa kwake suti kulikuuma sana? Ukaona umkomeshe mwenyewe kwa lugha nyingine umtie adabu.
Unajua kimaadili kuna mavazi ya baadhi ya shughuli? Na zingine ukienda tofauti watu wanakuona kituko? Sasa kazi yetu ilikuwa inabagua nguo yeye kanajidai kujua ili anikomeshe, mbona alikoma mwenyewe! Mpaka amekuja kutoka hakuwahi kuvaa tena suti, nyoko!!
 
Habari zenu

Katika hali isiyo ya kawaida siku ya leo nimepewa rasmi barua ya kuachishwa kazi kwa kosa la utovu wa nidhamu

Shughuli ilianzia Alhamisi iliyopita mida ya saa tatu bosi aliniita ofisini na kuniagiza vitumbua vya mia tisa

Kwakweli kulingana na nilivyokuwa mimi mtu mzima nimevaa nimependeza, nimechana nywele vizuri na nimechomekea

Nilikuwa nimevaa yale mashati ya kuwaka waka yale ya tetroni na nimechomekea na kuvaa suruali ya kitambaa nimechomekea, kitendo cha bosi kuniagiza vitumbua vya mia tisa kwangu niliona kama ni fedheha kubwa sana.

Yaani mimi nitoke ofisisni niende nje eti nimeagizwa vitumbua? Nilimwambia bosi kuwa sitaweza kwenda maana nina kazi na niko bize.

Mimi nina mke na watoto uniagize vitumbua?

Ijumaa nilisimamaishwa kazi na leo rasmi nimeachishwa kazi

Hivi hii ni sawa kweli?
Nafahamu yawezekana umeandika ili kufurahisha watu. Lakini Soma hapa chini, Itakusaidia.

Tito 3:1-2
"Uwakumbushe watu kunyenyekea kwa wenye uwezo na mamlaka, na kutii, na kuwa tayari kwa kila kazi njema;
wasimtukane mtu ye yote, wasiwe wagomvi, wawe wema, wakionyesha upole wote kwa watu wote."

Tubu dhambi yako ya kukataa kuitii mamlaka iliyoko juu yako.
 
Mkuu kama umekubal kuajiriwa bas jaribu kadri uwezavyo kufuata matakwa ya boss wako vinginevyo utaangukia pua kilasiku
 
Kwahiyo mtoa mada hiyo ni aina gani ya mtu?pamoja na mtoa mada
Ni aina ya mtu anayejumlisha hadhi yake kwenye kazi. Akipewa majukumu ambayo anaweza kufanya mtu mwingine, hudhani kashushwa sana. Anaweza kuharibu kwa makusudi hata kazi ya taaluma yake ili kutuliza moyo wake kwa sababu ya kuhisi kudharauliwa kwa kupewa kazi anayodhani si hadhi yake.
 
Au labda mtoa mada aliombwa kitumbua cha ukwel ila anajaribu kupunguza ukal wa maneno kwa kutaja vitumbua vya mia Tisa,haiingii akilin boss kubwa akakuagiza vitumbua vya miamia tena kwa msisitizo wa kurudishiwa mia yake anataka tisa tu
vitumbua vya kunywea chai
 
Mkuu kama umekubal kuajiriwa bas jaribu kadri uwezavyo kufuata matakwa ya boss wako vinginevyo utaangukia pua kilasiku
kwaiyo wewe bosi akikuagiza ukamfatie nyanya sokoni unaaenda?
 
Back
Top Bottom