Nimefukuzwa kazi kisa kugoma kumfatia bosi vitumbua vya mia tisa

Nimefukuzwa kazi kisa kugoma kumfatia bosi vitumbua vya mia tisa

Sipati picha vichwa vya magazeti
1. Atumbuliwa Kwa utovu wa nidhamu
2. Aliyekataa kwenda kumnunulia boss vitumbua atumbuliwa

3. Vitumbua vyamfukuzisha kazi mfanyakazi kiburi

4. Aliyechomekea shati la kung'aaa atimuliwa kazi
5. Kiburi champoza mfanyakazi aliyechomekea shati la kung'aaa
6. Mfanyakazi Kiburi akutana Boss Jeuri
 
...Mkuu, kwa hiyo ulikataa kwa sababu tu bosi alikutuma Vitumbua Tisa?
Angekutuma 'Baga'mbili ama Chapati Nne Ungekubali???[emoji16]
 
Pole sana ndugu, lakini nikuulize kidogo

Unaanzaje kugoma kufuata vitumbua na unafanyakazi kwenye kampuni ambayo bosi wake anaagiza vitumbua tena vya "itapendeza!". Siku nyingine landana na mazingira ya kazini.

Ok, chomekea musaidiane hapo nyumbani kuchoma vitumbua.
 
Habari zenu

Katika hali isiyo ya kawaida siku ya leo nimepewa rasmi barua ya kuachishwa kazi kwa kosa la utovu wa nidhamu

Shughuli ilianzia Alhamisi iliyopita mida ya saa tatu bosi aliniita ofisini na kuniagiza vitumbua vya mia tisa

Kwakweli kulingana na nilivyokuwa mimi mtu mzima nimevaa nimependeza, nimechana nywele vizuri kama kazi inavyotaka

Nilikuwa nimevaa yale mashati ya kuwaka waka yale ya tetroni na nimechomekea na kuvaa suruali ya kitambaa, kitendo cha bosi kuniagiza vitumbua vya mia tisa kwangu niliona kama ni fedheha kubwa sana kwasababu sio majukumu yangu na ni kama dharau kwangu,

Yaani mimi nitoke ofisisni niende nje eti nimeagizwa vitumbua? Nilimwambia bosi kuwa sitaweza kwenda maana nina kazi na niko bize.

Mimi nina mke na watoto uniagize vitumbua?

Ijumaa nilisimamaishwa kazi na leo rasmi nimeachishwa kazi

Hivi hii ni sawa kweli? nakusudia kwenda kwenye vyombo vya sheria
Bosi wako alikuwa wa kike au wa kiume?!
 
Kama ulikubali kipengele kwenye mkataba kinachosema "pamoja na kazi nyingine kama utakavyopangiwa na mwajiri wako", hicho ndicho kilichohalalisha kufukuzwa kazi.
Bila hearing, barua ya onyo, hapo hakuna uhalali wa kufukuzwa kazi.

Akienda mahakamani analipwa vizuri tu.
 
Hivyo vitumbua vya miamia vinauzwa wapi? Maana huku kwetu vitumbua ni mia mbili kimoja kwahiyo huwezi kupata vya mia tisa.
 
Aaah achana nae mimi nakuunga mkono kwa huo msimamo Bora Hata angekuagiza vya buku, maana vya mia tisa afu uanze kusubiri na hio chenji sh mia, afu mtu umevaa tetroni yako na jua likuwakie ufe bure.
Hahahaha, kwamba bora angemwagiza vya buku.
 
Mtumikie Kafiri ili upate mradi wako! Ungeenda tu kumnunulia vitumbua vyake.
 
Mkuu, Unachezea kazi!?

Ukiwa mwajiriwa huna tofauti na mtumwa hivyo huna budi kutii ili MKATE kwa familia uende kinywani.

Ulijiandaa kisaikolojia kabla ya kugoma kutumwa?

Kabla ya kumgomea bosi hukujua kitakachofuata baadaye ni nini?

NOTE: Usimshtaki bosi popote pale, Kama kuna kazi au shughuli nyingine hapo mtaani ifanye MKATE uende kinywani.

LAKINI:

Kama huna pengine pa kujishikisha, Nenda ukakiri kosa lako kwa bosi na umwombe msamaha atakusikiliza.

KWA MAANA: "Jawabu la upole huigeuza ghadhabu bali..." 15:1 METHALI
 
Habari zenu

Katika hali isiyo ya kawaida siku ya leo nimepewa rasmi barua ya kuachishwa kazi kwa kosa la utovu wa nidhamu

Shughuli ilianzia Alhamisi iliyopita mida ya saa tatu bosi aliniita ofisini na kuniagiza vitumbua vya mia tisa

Kwakweli kulingana na nilivyokuwa mimi mtu mzima nimevaa nimependeza, nimechana nywele vizuri kama kazi inavyotaka

Nilikuwa nimevaa yale mashati ya kuwaka waka yale ya tetroni na nimechomekea na kuvaa suruali ya kitambaa, kitendo cha bosi kuniagiza vitumbua vya mia tisa kwangu niliona kama ni fedheha kubwa sana kwasababu sio majukumu yangu na ni kama dharau kwangu,

Yaani mimi nitoke ofisisni niende nje eti nimeagizwa vitumbua? Nilimwambia bosi kuwa sitaweza kwenda maana nina kazi na niko bize.

Mimi nina mke na watoto uniagize vitumbua?

Ijumaa nilisimamaishwa kazi na leo rasmi nimeachishwa kazi

Hivi hii ni sawa kweli? nakusudia kwenda kwenye vyombo vya sheria
Kama unamkataba nenda mahakama ya kazi utafurahi mwenyewe.
 
Kumbe watanzania wengi Umaski I wetu unaanzia kwenye Fikra!? Nimegundua Kupitia comments humu.

Confidence,Self worth is Empty for most Tanzanians.
 
Back
Top Bottom